Je! fedha ni jawabu la mambo yote? (Mhubiri 10:19).

Je! fedha ni jawabu la mambo yote? (Mhubiri 10:19).

Jibu: Tusome,

Mhubiri 10:19 “Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko, Na divai huyafurahisha maisha; NA FEDHA HULETA JAWABU LA MAMBO YOTE”.

Kulingana na huu mstari je ni kweli fedha ni jawabu la kila kitu?.

Jibu ni La! Fedha haitoi jawabu la mambo yote, kama ndio basi fedha ingeweza kununua uzima wa milele, hivyo kusingekuwa na haja ya Bwana Yesu kutoa uhai wake kwaajili ya uzima wa roho zetu.

Lakini biblia inatufundisha kuwa tumekombolewa kwa damu ya Yesu na si kwa fedha.

1 Petro 1:18 “Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu

19 bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo”.

Vile vile fedha haiwezi kutibu kifo, wala kununua amani, kwasababu wapo watu wenye pesa nyingi lakini hawana amani n.k.

Lakini kama hivyo ndivyo kwamba fedha si jawabu la mambo yote, kwanini bi lia iseme no jawabu la mambo yote?.

Ili kupata jibu la swali hili ni vizuri tukausoma mstari huo kwa kutafakari kwa kina sehemu za kwanza za mstari huo na zile za mwisho.

Mstari huo unaanza kwa kusema.. “Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko” na unandelea kwa kusema… “Na divai huyafurahisha maisha”…na unamalizika kwa kusema “NA FEDHA HULETA JAWABU LA MAMBO YOTE”.

Sasa swali ni mambo gani hayo ambayo fedha inaleta majibu yake?.

Jibu: Ni mambo hayo yanayotajwa hapo juu, maana yake yahusuyo karamu hizo ziletazo kicheko zenye ulevi…. na si mambo mengine tofauti na hayo.

Na kweli mambo ya kidunia karibia yote jawabu lake ni fedha, maana yake ukiwa na fedha utaweza kuyafanya au kuyapata, na ukizikosa fedha pia unaweza kuyakosa.

Anasa zote za kidunia zinahitaji pesa, na wanaotaka anasa wanazitafuta pesa kwasababu hilo ndio jibu lake.

Lakini wana wa Mungu, hawaishi kwa fedha wala fedha si jawabu la mambo yao yote…bali Damu ya Yesu ndio jawabu la mambo yao yote.

Wana wa Mungu hata pasipo pesa wanaweza kuishi vizuri kabisa, na pia hawana tabia ya kupenda fedha, bali fedha yao ni Damu ya Yesu katika Roho Mtakatifu.

Je upo ndani ya agano la damu ya Yesu au Mungu wako ni fedha?.

Waebrania 13:5 “Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa”

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Aibusu midomo atoaye jawabu la haki (Mithali 24:26)

KUOTA UNAPEWA PESA, KUNA MAANISHA NINI?

Pesa za bindoni ni nini?(Marko 6:8)

MFANO WA MAMBO HAYO NI UBATIZO.

KANUNI YA KUOMBA NA KUPOKEA.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments