KUOTA UNAPEWA PESA, KUNA MAANISHA NINI?

KUOTA UNAPEWA PESA, KUNA MAANISHA NINI?

Awali ya yote ili upate ufasaha wa ndoto yako, na kuepuka kudanganywa na kila aina ya tafsiri mtu yeyote anayoweza kukuletea, awali ya yote unapaswa ufahamu ndoto yako inaangukia katika kundi lipi,

Yapo makundi makuu matatu (3) ya ndoto:

  1. Kundi la kwanza: ni zile ndoto zinazotokana na Mungu,
  2. kundi la pili: ni zile zinazotokana na adui(Shetani)
  3. kundi la tatu: ni zile zinazotokana na mtu mwenyewe,

Ndoto zinazoangukia katika kundi hili la tatu ndizo zinazootwa na watu mara kwa mara kila siku na kama mtu asipoweza kuzitambua atajikuta anahangaika nazo, na huku hazina maana yoyote ya kumsaidia, kwasababu ni ndoto zinazokuja kutokana na shughuli anazozifanya kila siku au mazingira yanayomzungumka muda wote hivyo hizi huwa hazibebi  ujumbe wowote..

Kwahiyo ni rahisi ubongo wake kuchukua yale matukio anayoyofanya kila siku na kuyatengenezea matukio yanayofanana na hayo katika ndoto usiku na kuota, ukijiona unaota hivyo basi puuzia ndoto hizo

Ikiwa unahitaji kufahamu kwa undani juu ya makundi haya basi pitia somo hili kwanza >>>> NITAJUAJE KAMA NDOTO NI YA MUNGU AU YA SHETANI?   kisha ndio tuendelee,

 Kwamfano ndoto za namna hii za kujiona unapewa pesa, utakuta mtu mmoja kazi yake kila siku ipo kwenye pesa kama vile benki au mfanyabiashara ambaye muda wote analipa na kulipwa pesa, hivyo kuota anapewa pesa linaweza kuwa ni jambo la kawaida kwake kutokea katika ndoto zake za kila siku, kwasababu ubongo ulishajiengenezea ulimwengu kama huo.

Lakini ikitokea umeota ndoto katika mazingira, ambayo hayaendani na wewe kupewa pesa, au umeota ndoto hiyo na ukaiona si ndoto ya kawaida, au ulikuwa katika maombi ya kumwomba Mungu kitu Fulani na imekuja na uzito Fulani hivi, au amani Fulani hivi, basi fahamu kuwa upo ujumbe unapaswa kujifunza ndani yake.

Kumbuka kibiblia Fedha inawakilisha chombo cha kuletea jawabu.

Mhubiri 10:19 “Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko, Na divai huyafurahisha maisha; Na fedha huleta jawabu la mambo yote”.

Hivyo Mungu kukuonyesha katika ndoto, unapewa fedha, ni ishara kuwa amekupa jawabu la ombi lako, na hivi karibuni utapata haja yako..Ila tilia maanani kitu kimoja hapo biblia inaposema, fedha huleta jawabu la mambo yote haimaanishi  kuwa inaleta majibu mpaka kwenye mambo ya rohoni hapana, fedha haiwezi kuleta uzima ndani ya mtu wala haiwezi kununua upendo..lakini kama ukichunguza hapo utaona mistari hiyo inalenga mambo ya ki mwilini..kama vile shughuli za karamu, nguo, chakula, nyumba, gari, biashara, ambavyo hivi kimsingi vinahudumiwa na fedha..

Pia tazama..

1  Kuota ajali.
2 Kuota upo nchi nyingine.
3 Kuota unajifungua
4 Kuota upo makaburini
5 Kuota unacheza mpira
6 Kuota unaanguka
7 Kuota upo kanisani
8 Kuota umeachwa na gari
9 Kuota unang’oka meno
10 Kuota unaanguka

Lakini tukirudi kwenye hiyo ndoto ya pesa vile vile usitegemee sana kuwa atatumia njia hiyo hiyo uliyoiona kwamba kweli kuna mtu atakujana  kukupa wewe fedha hapana, inaweza ikawa hivyo au isiwe hivyo, anaweza  kutumia njia pengine ya kuirutubisha kazi yako unayoifanya sasa hivi ,au ukapata kibali mahali Fulani pengine kazini kwako, ambapo boss wako atakulipa vizuri zaidi kuliko sasa hivi, au ukapata mkopo wa kufanya biashara yako n.k.Na kama ukijiangalia ndio utagundua vitu vya aina hiyo hiyo ndio ulivyokuwa unamwomba Mungu…

Hivyo ametumia ndoto ya fedha kama ishara ya kukuonyesha kuwa maombi yako ameyasikia,..Lakini usitazamie kuwa mtu anayemwomba Mungu mambo ya rohoni kama vile uzima wa milele, au Roho Mtakatifu, au nguvu za Mungu, ataonyeshwa ndoto za namna hiyo kama jibu la maombi yake hapana.. Mungu atamwonyesha Maono ya rohoni, pengine usishangae mtu kama huyo kuona maono ya mbinguni, au kukutana na malaika ndotoni, au kuisikia sauti ya Mungu ikisema naye, au kuota anahubiri au anafundishwa biblia n.k…

Hivyo kaa katika matarajio huku ukiulinda ukamilifu na utakatifu  katika kazi yako, ndipo Mungu ataitimiza ahadi yake juu yako. Lakini kama wewe upo nje ya Kristo ukaota ndoto kama hiyo, fahamu kuwa ni ishara mbaya nayo ni ishara ya upotevu zaidi..utakwenda kufanikiwa lakini ni ili upotee..

Mithali 1:32 “Maana kurudi nyuma kwao wajinga kutawaua, Na kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza”.

Usisibirie udanganyifu wa mali au mafanikio vikuangamize..Mrudi Muumba wako mapema, tubu dhambi zako kwa kumaanisha kabisa kuziacha, ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi kwa Jina la YESU KRISTO ikiwa bado hukubatizwa kisha anza kumwangalia Mungu ili yeye atembee pamoja na wewe katika njia zako zote.

Ubarikiwe.

Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Mithali 1:32

kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza.

Mada Nyinginezo:

TOFAUTI KATI YA NDOTO NA MAONO NI IPI?

USHUHUDA WA RICKY:

MTETEZI WAKO NI NANI?

FUATILIA NDOTO HII, UTAJIFUZA KITU.

NOTI YA UFALME WA MBINGUNI.

LULU YA THAMANI.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
14 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Lung'wecha jackson
Lung'wecha jackson
1 year ago

Nini maana ya kuota uko kwenye maji au kwenye bwawa

Brian otieno
Brian otieno
1 year ago

Mimi in Brian kutoka nchini Kenya na ningependa munisaidie kuwa naota ndoto za ushetani kwaba nimepewa pesa nanika kataa kupokea,hilo linaweza kuwa mini hasa

nando mahay
nando mahay
1 year ago

Kumradhi naomba mawasiliano Yako Nina shida ya kiroho zaidi ambayo siwezi kuongea public.. ubarikiwe🙏

Peter 0tiso
Peter 0tiso
2 years ago

Am Peter from Kenya,,, Naomba kujua maana ya kuota nalipwa Deni ,,,na
pia kuota ukila mahindi ya kuchemsha ±254725610676

Christian Mgombezi
Christian Mgombezi
3 years ago

Nini maana ya ndoto uliyoota unaokota hela za noti elfu tano tano mbili Mara tatu

Virginia Nicholas.
Virginia Nicholas.
4 years ago

Je nini maana kuota unachimba viazi vitamu kwa shamba yako?

Virginia Nicholas.
Virginia Nicholas.
4 years ago

Amen, brother ,.nimebarikiwa, tena nimeelewa kabisa . Thanks.

John Sanga
John Sanga
4 years ago

Asante nimekuelewa Sana ndugu yangu mungu akubariki