SAA YA KIAMA.

SAA YA KIAMA.

Wingu la Mashahidi
Wingu la Mashahidi
SAA YA KIAMA.
Loading
/

Cha kushangaza ni kwamba wakristo tu peke yetu ndio hatujui saa tunayoishi na muda gani mchache tuliobakiwa nao, na hata kama tunajua basi wengi bado hatujachukulia kwa uzito jambo hili ukilinganisha na jinsi wanasayansi na shetani wanavyolichukulia kwa upande wao..Wanasayansi leo hii wameunda saa yao maalumu ijulikanyo kama “Doomsday clock” (saa ya kiama), ambayo hiyo inawakaumbusha ni wakati gani wanaoishi sasa, wameifananisha na saa  yetu hii ya kawaida, kwamba mshale ukifika tu saa 6 kamili usiku basi usiku wa manane umeanza, vilevile na siku mpya imeanza, Hivyo hiyo saa yao sasa ipo katika muundo huo huo kwamba zimebaki dakika chache sana kabla ya kuingia usiku wa manane wao(yaani kiama), wanakadiria kuwa  miaka yote ya nyuma saa hiyo ilikuwa haijafikia usiku wa manane lakini  kuanzia  mwaka 1947 ilifikia dakika 7 kabla ya kuingia usiku wa manane, na hiyo ni kwa jinsi walivyokuwa wanaona hali ya dunia inavyokwenda kwa matetesi ya vita vya mabomu ya Atomiki, kwamba muda wowote vita vinaweza kuanza na vikianza tu basi itachukua muda mfupi sana dunia kuwa sio sehemu tana ya kuishi mwanadamu.

Na kila siku mshale wao unapanda, mwaka 2015 walikadiria ni dakika 3 tu zimebaki , mwaka 2017 walikadiria dakika 2.5, mwaka jana walikadiria dakika 2 kabla ya kufikia saa 6 ya usiku wao…Yaani tafsiri yake ni kuwa hatari ya kukifikia kiama cha dunia ni kikubwa kuliko inavyodhaniwa katika miaka iliyopita…

Kama ulikuwa hujui sikuzote Mungu kabla hajaleta uharibifu wa hii dunia ni sharti kwanza wanadamu wajiharibu wenyewe, Ndivyo ilivyokuwa hata katika kipindi cha Nuhu, watu walijiharibu wenyewe kupindukia kukawa hakuna tena sababu ya maisha na ndipo Mungu akamaliza kila kitu (Mwanzo 6:12), ndugu  usione ukadhani kuwa duniani kuna amani, usidanganyike na siasa za dunia, ni jambo la kawaida kuficha ukweli ili watu wasiwe na wasiwasi lakini  nyuma yake ipo hofu kubwa ambayo wao wenyewe wanaitambua, pamoja na wanasayansi wao, kwa huu ugunduzi wa mabomu ya Atomiki ambayo hata leo kwenye vyombo vya habari unaona mataifa mengi yanagombana kila siku kuhusu hayo, kwasababu wanajua vita vikishaanza basi ndio mwisho wa kila kitu,..

muda mfupi chini nitakuonyesha video fupi, ya jaribio la kwanza la bomu la Atomiki lilidondoshwa huko Urusi tarehe 30 Octoba 1961, ukubwa wake ukiachilia mbali yale ya Nagasaki na Heroshima yaliyomaliza vita ya pili ya dunia kwa kuuwa  zaidi ya watu laki 2 kule Japan. Hili ni mara 1000 zaidi ya yale kwa uharibifu wake, tazama video fupi chini uone lilivyodondoshwa.

Lakini kabla hayo hayajatokea Unyakuo utakuwa umeshapita, katika ule mfufulizo wa maono 7 aliyoonyeshwa mtumishi wa Mungu maarufu William Branham  na kuambiwa hayo yatatokea kabla ya kuja kwa pili kwa Kristo, kama wengi tunafahamu na tunavyosoma katika historia, matano kati ya yale yalitimia kama yalivyo mawili bado, William Branham alionyeshwa kabla ya kutokea vita ya pili ya dunia jinsi hitler atakavyonyanyuka na kuiongoza dunia yote katika vita na jinsi  kifo chake kitakavyoishia na kuwa cha kiajabu ajabu, habari hiyo aliihubiri na ikajulikana na watu wote kabla hata ya kutokea kwa vita ya pili ya dunia, hilo lilikuwa ni ono la pili kati ya yale saba, sasa ono la saba ambalo lilikuwa ndio la  mwisho alionyeshwa kuangamizwa kwa taifa la Marekani, anasema alisikia mlipuko mkubwa usio wa kawaida nyuma yake na alipogeuka hakuona kitu chochote zaidi ya vipande vya mabaki na moshi tu,…Na hicho si kingine zaidi ya bomu la nyuklia.

Sasa hiyo alioneshwa kwa taifa lake, jambo hilo litakuja kuwa ulimwenguni kote, lakini mpaka hayo yote yatokee unyakuo utakuwa umeshapita, Mpaka sasa unaweza kuona ni saa gani hii tunaishi, Kama wanasayansi watu wa kidunia hawaishi kama vile wanayo wiki moja mbeleni, iweje mimi na wewe leo tuishi kama vile tuna maelfu ya miaka mbeleni,..Bwana anakuja, dalili zote zinaonesha, sijui tanataka tuoneshwe dalili zipi tena ndio tuamini na sisi kuwa tunaishi ukingoni mwa wakati..laiti kama na sisi tungekuwa na saa yetu basi saa yetu ingesoma tupo  visekunde vichache kabla ya kwenda katika unyakuo kwa Baba na kuanza kwa utawala mpya wa miaka 1000 wa Bwana wetu YESU KRISTO..

Tazama video fupi chini ya bomu lijulikanalo kama TSAR BOMBA, jinsi lilivyoachiwa ili ufahamu yatakayowakuta wale wote watakaokosa unyakuo.

Bwana Yesu akubariki sana Mtu wa Mungu, Tafadhali share na wengine


Mada Nyinginezo:

KATI YA UNYAKUO WA KANISA, DHIKI KUU, VITA VYA HAR-MAGEDONI, UTAWALA WA MIAKA 1000, VITA YA GOGU NA MAGOGU, HUKUMU YA KITI CHA ENZI CHEUPE. JE, NI KIPI KINAANZA NA KINGINE KUFUATA?

SIKU YA BWANA INAYOTISHA YAJA!

KITABU CHA UZIMA NI KIPI?

KUZIMU NI MAHALI PA NAMNA GANI ,JE! HUKO WANAISHI WATU WAKIFA NA KWENDA KUPATA MATESO AU NI VINGINEVYO?


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments