Nini maana ya Neno Haleluya.

Nini maana ya Neno Haleluya.

Hili ni Neno lenye asili ya kiebrania, lenye muunganiko wa maneno mawili “Halelu”, na “Yah”..Halelu ikiwa na maana “msifu” na “Yah” ikiwa na maana “Bwana” ..”Yah” ni ufupisho wa Neno Yehova,..Hivyo Haleluya Ni neno lililomaanisha kumsifu Bwana kwa nyimbo za furaha..

Kama wewe ni msomaji wa biblia utaona likijitokeza sehemu nyingi katika maagano yote mawili, Kwenye agano la kale utaliona kwenye kitabu cha Zaburi, na katika agano jipya utaliona  kwenye kitabu cha Ufunuo.

Zaburi 106:1 “Haleluya. Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele.

2 Nani awezaye kuyanena matendo makuu ya Bwana, Kuzihubiri sifa zake zote?”

 

Zaburi 113:1 “Haleluya. Enyi watumishi wa Bwana, sifuni, Lisifuni jina la Bwana”.

 

Ufunuo 19:1 “Baada ya hayo nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, sauti kubwa mbinguni, ikisema, Haleluya; wokovu na utukufu na nguvu zina BWANA MUNGU wetu”.

Hata sasa Neno hili tunalitumia wakristo pale tunapomsifu Mungu kwa furaha.. Au tunapoufurahia ukuu wake. Wewe nawe usione aibu kulitamka Neno hili kwa nguvu pale uufurahiapo utukufu wa Mungu.

Bwana akubariki.


 

Mada Nyinginezo:

BWANA ALIMAANISHA NINI KUSEMA JIKANE MWENYEWE?

BWANA ALIMAANISHA NINI KUSEMA “WAACHE WAFU WAZIKE WAFU WAO.(MATHAYO 8:21)?

JE! KITABU CHA YASHARI NI KITABU GANI? (2SAMWELI 1:17-18),

JE! KUBET NI DHAMBI?

JE! KUFANYA MASTURBATION (PUNYETO) NI DHAMBI?

UWEZA WA MUNGU UNAONEKANA WAPI?

UNYAKUO.


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Rowland
Rowland
2 years ago

AMEN…! ni nani anayepaswa kumsifu BWANA? JE ni wale walio okoka TU au hata wamataifa(wasio mkiri KRISTO)! NA je wamataifa mfano wanaoimba nyimbo za kidunia wakimsifu kwa kutaka jina lake MUNGU anapokea sifa zao???