Bwana alimaanisha nini kusema JIKANE mwenyewe?(Mathayo 6:24)

Bwana alimaanisha nini kusema JIKANE mwenyewe?(Mathayo 6:24)

JIBU: Neno kujikana linamaana kuwa, ‘kukataa matamanio yako binafsi au malengo yako kwa sababu fulani’. Hivyo kujikana kunakozungumziwa katika biblia ni kujikana kwa Kristo. Hii ikiwa na maana kuwa unapoamua kumfuata Kristo unakuwa tayari kuyakataa matamainio yako hata kama ni mazuri kiasi gani, hata kama yanatia maanani kiasi gani, unayaweka chini na kukubali kuyafuata yale ya Bwana Yesu tu. Na ndio maana mtume Paulo aliweka wazi na kusema hivi: 

“7..Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo.

8 Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo; (Wafilipi 3:7-8)”. 

Unaona hii ni nguzo kuu na ya muhimu sana, inayomtambulisha mtu kama amemfuata Kristo. Wanaotubu dhambi zao ni wengi lakini wanaodhamiria kumfuata Kristo ni wachache sana. Unapoamua kuwa binti wa kikristo, uwe tayari kuukana uzui wako, na kuacha kuvaa vimini na suruali, nguo za kikahaba, na mapambo ya kiulimwengu…ili ufanyike mwanafunzi wa Yesu vinginevyo bado hujawa mkristo hata kama utasema umeokoka. Vile vile kijana unapokuja kwa Kristo uwe tayari kukataa tamaa zote za ujanani, disco, miziki ya kidunina, pombe na sigara, uasherati, unavipiga vita unaamua kumwangalia Kristo kuanzia huo wakati na kuendelea. Ni mambo ambayo ungeweza kuyafanya kama vijana wengine katika ujana wako lakini unajikana kwa ajili ya kuujua uzuri ulio katika Kristo. Na Bwana Yesu akishaona huo moyo wako hapo ndipo na yeye anapochukua nafasi ya kukufanya kuwa mtu mwingine wa tofauti kabisa katika viwango vya rohoni. Unafanyika kuwa mwanafunzi wake kweli kweli kama mitume wake.

 Na hili ni tendo endelevu ambalo linapaswa liwe kila siku, hata katika kuifanya kazi ya Mungu unapaswa ujikane mwenyewe, muda ambao ungetakiwa kufanyabiashara kama watu wengine wewe unaifanya kazi ya Mungu, Vilevile tumeagizwa tudumu katika sala, wakati ambao ungepaswa ulale usiku kama watu wengine wewe unaamka kuomba, huko ni kujikana nafsi. Bwana anakokuzungumzia. Lakini pamoja na hayo katika kujikana huko, na kupoteza matamanio yako au vitu vyako kwa ajili ya Kristo yeye mwenyewe anatuambia, kwa kufanya hivyo ndivyo tunavyozipata. Kwa Mungu hakuna matujo kwani sikuzote mawazo anayotuwazia sisi na ya amani wala sio mabaya ili kutupa sisi tumaini zuri katika siku zetu za mwisho (Yeremia 29:11).

Na ndio maana hatuoni shida hata anapotuambia tuache kila kitu kwa ajili yake. Faida yake tutaiona kama sio katika ulimwengu huu basi katika ulimwengu unaokuja. Kwasababu anatuwazia kusudi jema siku zote.  Hivyo, Ni heri uonekane unapoteza kila kitu sasa kwasababu tu umeamua kumfuata Kristo, kuliko kupata kila kitu cha ulimwengu huu na mwisho wa siku unaishi katika ziwa la moto, itakufaidia nini?. 

Mathayo 16:24 “Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na AJIKANE MWENYEWE, ajitwike msalaba wake, anifuate.

25 Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona.

26 Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?”.

Ubarikiwe.

Mada Nyinginezo:

JE! NI KWELI UMEMFUATA YESU?

KISASI NI JUU YA BWANA.

MADARAKA YA WAKATI MKAMILIFU.

HUYU AZAZELI NI NANI TUNAYEMSOMA KATIKA(WALAWI 16:8)

JINSI EDENI ILIVYOKUWA.

UNYAKUO.


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
3 years ago

Ubarikiwe mtumishi kupitia ujumbe wako nimekuwa Mwanafunzi wa YESU, ubarikiwe Sana mwisho wa dahari tukutane Paradiso

Mlondani mtéé adolphe
Mlondani mtéé adolphe
3 years ago

Jambo katika jina la yesu kristo. Mimi ni mtumishi, nataka kujiunga na kundi ili.