KWANINI MAHUSIANO YA JINSIA MOJA NI DHAMBI?

KWANINI MAHUSIANO YA JINSIA MOJA NI DHAMBI?

Mahusiano yoyote yale yanayohusisha watu wa jinsia moja ni machukizo mbele za Mungu..Biblia imeweka wazi katika kitabu cha Mambo ya Walawi
 
Walawi 18:22 “Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo”.
 
 
Walawi 20:13 “Tena mtu mume akilala pamoja na mtu mume, kama alalavyo na mtu mke, wote wawili wamefanya machukizo; hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao”
 
Ipo asili ya dhambi ambayo mtu anazaliwa nayo…Asili hiyo ya dhambi au kwa lugha nyingine inaitwa sheria ya dhambi, inafanya kazi ndani ya mtu, tangu akiwa tumboni mwa mama yake…hiyo inamfanya mtu anazaliwa na tabia fulani fulani ambazo asili yake ni dhambi…mfano wa tabia hizo ni kama hasira zisizokuwa na sababu, kiburi, uchungu usiokuwa na sababu, ukorofu, utundu, tamaa ya uasherati n.k vyote hivyo vinatokana na ile asili ya dhambi mtu anayozaliwa nayo.
 
Lakini pamoja na hayo, kuna dhambi ambazo Mungu aliziweka mbali sana na mwanadamu kuzifikia, na hizo hazimo miongoni mwa dhambi za asili..Ni dhambi lakini mtu anakuwa hazaliwi nazo… Mtu mwenyewe kwa mapenzi yake anapokuwa mtu mzima anaweza kuzipachika ndani yake na kuzifanya.
Na moja ya dhambi hizo ni dhambi za kumtamani mtu wa jinsia moja na ya kwako. Hiyo tamaa ya namna hiyo haipo ndani ya mtu tangu anazaliwa. Mwanamke kumtamani mwanamke mwenzake au mwanamume kumtamani mwanamume mwenzake…
 
Dhambi hii ni moja ya dhambi mbaya sana kuliko nyingi kwasababu ipo kinyume na UHAI na UZIMA.
Hebu tafakari endapo Adamu angekuwa na Adamu mwenzake sisi tungetokea wapi? Au wakina Hawa wangeumbwa wawili, sisi tungetokea wapi leo?.. Neno la Bwana linalosema zaeni mkaongezeke lingekuwa wapi?…Hebu fikiri Wanyama wangekuwa wote wa jinsia moja..hii mifugo tuliyonayo leo ingekuwa wapi?…Maziwa tunayokunywa yangetokea wapi? Nyama tunazokula nazo zingetokea wapi, asali tunayoifurahia ingetoka wapi? Endapo nyuki wote wangekuwa wakike au wakiume?
 
Hata chakula tusingekuwa nacho, kwasababu hata mimea ina sehemu ya kike na ya kiume…sasa kama mimea yote ingekuwa na sehemu ya kiume tu, au ya kike tu…hiyo ngano tunayokula kila siku ingetokea wapi? Mboga tunazokula zingetokea wapi?..Kwahiyo dunia isingekuwa dunia wala Maisha yasingekuwepo endapo kungekuwa na jinsia moja tu duniani.
Kwahiyo dhambi ya mahusiano ya jinsia moja ni dhambi ya KIFO, Kwasababu ipo kinyume na UHAI…Chochote ambacho kipo kinyume na Uhai ni Kifo. Na yeyote afanyaye dhambi ya kifo atakufa.
Kaa mbali na ushoga ni dhambi, kaa mbali na usagaji, wapo wengi wanafanya dhambi hizi kwa siri, pasipo kujua madhara ya dhambi hiyo, Ni dhambi zinazoivuta ghadhabu ya Mungu kwa haraka sana….Dhambi zilizoifanya sodoma na ghomora ziteketezwe ni dhambi hizo za mahusiano ya jinsia moja. Na dhambi hizi hazina cha kujitetea kwasababu ni dhambi za makusudi..Mtu anazipandikiza ndani yake akiwa na akili timamu kabisa, hazina ushawishi wowote..hakuna mazingira yoyote yanayomshawishi mtu kumtamani mtu wa jinsia moja na yeye, ni mtu mwenyewe anazitengeneza ndani yake kwa msaada wa roho za mapepo.
 
Warumi 1:26 “Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili;
 
27 wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao.
 
28 Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa”
 
Tubu, kama wewe ni mmojawapo, kisha uanze uanze kutafuta kuyafanya mapenzi wa Bwana. Naye atakuangazia neema zake.
 
Shalom.

Mada Nyinginezo:

INJILI YA MILELE.

NINI TOFAUTI KATI YA DHAMBI, UOVU NA KOSA KIBIBLIA?

LILE TUMAINI LILILO NDANI YETU LINAPOULIZIWA.

CHACHU YA MAFARISAYO NA CHACHU YA HERODE.

UNYAKUO.

NIFANYE NINI ILI NIIKWEPE HUKUMU.


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments