KUOTA AJALI, KUNAMAANISHA NINI?

KUOTA AJALI, KUNAMAANISHA NINI?

Ndoto za ajali zinaweza kuja katika maumbile mengi tofauti tofauti, wengine wanaota ajali za pikipiki, wengine za magari, wengi ndege, wengine meli, wengine treni, katika namna tofauti tofauti. Wengine wanaota mtu kagongwa na gari, au magari yanagonga gongana n.k… kwa vyovyote vile, ndoto hizo zinabeba maudhui moja nayo ni “AJALI”

Sasa ili kupata tafsiri sahihi ya ndoto hiyo ni vizuri ukajitambua wewe upo katika kundi gani.

1.) Kundi la kwanza ni waliookoka.

2) Kundi la pili ni wenye dhambi.

Tukianzana na kundi la kwanza: Ikiwa wewe, umeokoka (yaani unao uhakika umesimama ndani ya Kristo).  Basi fahamu kuwa ni Mungu anakutahadharisha tukio lililopo mbele yako, aidha kuna ajali utakutana nayo, au itatokea kwa mtu mwingine, au mahali fulani. Hivyo  unachopaswa kufanya, ni kuingia katika maomba ya kuvunja hiyo mipango ya adui. Ambayo pengine imepangwa kwako au kwa mtu mwingine..kemea kwa bidii kwa mamlaka uliyopewa katika jina la Yesu. Na Mungu ataisambaratisha hiyo mipango yote.

Ikiwa ndoto hiyo imekuja kwa uzito usiipuuzie, kwasababu Mungu kukuonyesha hivyo, ni ili usimame kama askari wa Mungu kushindana na hizo nyakati mbaya kabla hazijafika.( Soma Ayubu 33:14-15)

Kundi la Pili: Mwenye dhambi.

Ikiwa wewe ni mwenye dhambi(yaani hujaokoka, Kristo hayupo ndani yako). Ujue ndoto hiyo ni ishara ya tahadhari kubwa sana kwako. Kwamba kipindi si kirefu Mungu atakuadhibu, na kuadhibu kwake, kunaweza kukawa ni kifo cha ghafla, au kunaswa katika dhambi zako unazozifanya, na ukashindwa kutoka huko milele.

Soma hii Habari kwa makini;

Ezekieli 7: 6 “Mwisho umekuja, mwisho huu umekuja; unaamka ukupate; angalia, unakuja.

7 AJALI YAKO IMEKUJIA, wewe ukaaye katika nchi hii; majira yamewadia, siku ile inakaribia; siku ya fujo, wala si ya shangwe milimani.

8 BASI HIVI KARIBU NITAMWAGA GHADHABU YANGU JUU YAKO, nitazitimiza hasira zangu juu yako, nami nitakuhukumu sawasawa na njia zako; nami nitakupatiliza machukizo yako yote.

9 Jicho langu halitaachilia, wala sitaona huruma; nitakupatiliza njia zako na machukizo yako yote yatakuwa katikati yako; nanyi mtajua ya kuwa mimi, Bwana, napiga.

10 ANGALIA, SIKU HIYO; ANGALIA, INAKUJA; AJALI YAKO IMETOKEA; fimbo imechanua, kiburi kimechipuka”.

Umeona? Hayo maandiko yenyewe yanajieleza, ikiwa wewe ni mzinzi, fahamu kubwa ajali ya Ukimwi ipo mbele yako, wewe ni fisadi ajali ya vifungo ipo mbele yako, wewe ni mwizi ajali ya kifo ipo mbele yako, wewe ni mshirikina ajali ya jehanum ipo mbele yako.

Kwa ujumla kama wewe ni mwenye dhambi ujue mwisho wako upo karibuni sana. Na ukifa ni motoni. Ndio tafsiri ya ndoto hiyo.

Unasubiri nini mpaka hayo yote yakukute, ikiwa upo tayari leo kutubu dhambi, basi, Bwana Yesu atakusamehe, na kukuepusha na madhara hayo yote aliyokuonyesha mbele yako. Angeweza kukaa kimya tu, hayo mambo yakukute kwa ghafla, lakini kwasababu hataki uangamie ndio maana amekutahadharisha mapema.. Hivyo leo hii fungua moyo wako, kubali kugeuka, na uache dhambi zako zote, ili Kristo ayatengeneze tena Maisha yako.

Ikiwa upo tayari kutubu leo, basi fungua hapa, kwa ajili ya mwongozo wa SALA YA TOBA. >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Angalia pia Kuota Unajenga nyumba

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Group la whatsapp Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Angel
Angel
9 months ago

Bwana Yesu asifiwe MTUMISHI wa Mungu nabarikiwa Sana na mafundisho yako Mungu akubariki Sana Mim nimeokoka nampenda Yesu na nimesimima Leo nimeota nipo na wenzangu tunapanda mlima tulipofika juu ya mlima kuna gari lilikuwa mbele yetu likawaka moto tukaanza kushuka ule mlima tukakutana tena na Nagari mengine tukajikuta tuko kwenye maji watu waajabu wakawa wanatokea kwenye maji wanapambana na wenzangu lakini Mim hawakuweza kunigusa nikavuka salama naomba unisaidie tafsiri yako MTUMISHI wa Mungu asante