KUOTA UNACHEZA MPIRA.

KUOTA UNACHEZA MPIRA.

Kuota unacheza mpira kuna maanisha nini kiroho?


Ndoto za namna hii kuwa zinakuja kutoka katika makundi mawili,

Kundi la kwanza ni kutokana na shughuli za kila siku.

Mhubiri 5:3 “Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi;..”.

Kwamfano kuota unacheza mpira, asilimia kubwa ya ndoto hii huotwa na wanaume. Na hiyo ni kutokana na kwamba aidha mtu huyo kwa sasa anajishughulisha na mchezo wa mipira, au huko yumba alishawahi kucheza mpira, aisha shuleni au mitaani n.k..

Sasa ukiota ndoto ya namna hii mara kwa mara, basi huna haja ya kuwa na wasiwasi kwani ni ndoto tu, ambayo imekuja kutoka na shughuli za kila siku, Na hiyo inakuwa haina maana yoyote rohoni.

Kundi la Pili, ni kutokana na Mungu.

Lakini pia, ndoto kama hiyo inaweza kuja kwa namna ya kipekee sana, yaani kwa uzito usiokuwa wa kawaida, pengine ulikuwa unashindana sana kucheza, timu yako imezidiwa sana, au mmewazidi wale wengine sana, au wewe unacheza vizuri au vibaya kuliko wengine.. Kiasi kwamba ulipoamka  imekukaa sana akilini tofauti na ndoto ambazo ndoto ambazo unaotaga kila siku.

Basi ukiona hivyo lipo jambo Mungu anakukumbusha.

Kumbuka hapa dunia tupo katika mashindano, Na kila mmoja ni kama mchezaji, Na Lengo la mchezaji sikuzote ni kushinda tu, na sio kushindwa, ili mwisho wa siku akapokee medali ya dhahabu au kombe.

Biblia inasema..

1Wakoritho 9.24 “Je! Hamjui, ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, ili mpate.

25 Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee taji isiyoharibika.

26 Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; napigana ngumi vivyo hivyo, si kama apigaye hewa;

27 bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa”.

Unaona, wewe kwa upande wako ulijiona unashiriki katika mchezo aina ya mpira, wengine wanaota wakikimbia riadha, wengine wakiogelea n.k.

Hivyo kuota unacheza mpira ni Mungu anakukumbusha kuwa upo kwenye mashindano ndugu. Sijui kwa upande wako maisha yako yapoje, kwasababu watu wengine Mungu anazungumza nao hata mara mbili au mara tatu, ili tu waelewe sauti ya Mungu..Lakini hawasikii. Soma hapa..

Ayubu 33:14 “Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.

15 Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;

16 Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao”,

Hivyo kama wewe ni mmojawapo na bado upo nje ya Kristo, ni heri ukajitathamini vizuri tena. Kwasababu Yesu anao mpango mkubwa na wewe katika maisha yako haijalishi wewe ni muislamu na nani. Unachopaswa kufanya ni kumgeukia tu yeye uanze kushindana mashindano ambayo alikukusudia wewe ushindane ya kwenda mbinguni.. Kwasababu lipo taji bora alilokuandalia.

Si bahati mbaya ukutane na ujumbe huu. Hivyo usipuuzie, Mungu anakupenda, na anataka kukuokoa.

Ubarikiwe.

Fuatilia vichwa vingine vya masomo vilivyoainishwa chini ikiwa utahitaji kumjua Kristo zaidi.

Group la whatsapp Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi

Mada Nyinginezo:

Je ushabiki wa mpira ni dhambi?

USIYADHARAU MARUDIA YA BWANA.

KUOTA UPO UCHI.

KUOTA NYOKA.

FAHAMU TAFSIRI ZA NDOTO MBALIMBALI.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Rocki
Rocki
1 year ago

nimeota natoroka shule in maana gan?