MAOMBI YA TOBA.

MAOMBI YA TOBA.

Kuna tofuati kati ya sala ya toba na Maombi ya toba.

Sala ya toba, ni pale mtu anapokuja kwa mara ya kwanza kwa Kristo, pale anapoamua kuacha Maisha yake ya dhambi. Na kwamba kuanzia huo wakati na kuendelea Kristo anakuwa kiongozi wa Maisha yake, sasa, ikiwa yupo tayari kufanya hivyo basi pale anapopiga magoti, na kuonyoosha mikono yake juu, na kuomba msamaha, aidha yeye mwenyewe au kuongozwa na mtu mwingine, hiyo ndio inayoitwa sala ya toba, Na hii pia inafanywa hata kwa yule mtu ambaye alishaokoka akarudi nyuma, na sasa yupo tayari kumtumikia Mungu tena, kwa moyo wake wote.

Maombi ya toba:

Lakini Maombi ya toba, Nitofati kidogo: Haya ni lazima kwanza uwe katika wokovu.

Maombi haya ni maombi ya upatanisho. Na huwa si ya muda mfupi, au kipindi kifupi. Na mara nyingi huwa yanaambatana na kufunga kulingana na toba yenyewe inayoombwa. Mfano wa maombi haya:

  1. Toba kwa ajili ya familia/ukoo
  2. Toba kwa ajili ya Taifa/Nchi
  3. Toba kwa ajili ya Kanisa

Na nyingine yeyote inategemea na hitaji la mtu.

Kwamfano katika biblia tunaweza kuona mtu kama Danieli aliingia katika maombi ya toba kwa ajili ya taifa lake Israeli na watu wake, akiwa kule Babilioni,..Hiyo hakuiomba juu juu tu bali ilimgharimu afunge,

Danieli 9:1 “Katika mwaka wa kwanza wa Dario, mwana wa Ahasuero, wa uzao wa Wamedi, aliyetawazwa kuwa mfalme juu ya milki ya Wakaldayo; 

2 katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Danielii, kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka, ambayo neno la Bwana lilimjia Yeremia nabii, ya kuutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani, miaka sabini. 

3 Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia na majivu. 

4 Nikamwomba Bwana, Mungu wangu, nikaungama, nikasema, Ee Bwana, Mungu mkuu, mwenye kutisha, ashikaye maagano na rehema kwao wampendao, na kuzishika amri zake;..”

Matokeo ya maombi ya toba na rehema ilimfanya Danieli sio tu kupewa hitaji lake, bali na ziada ya pale, alipomba, mambo ambayo mpaka sisi wa siku za mwisho yanayafaidi..Soma sura yote hiyo utaona jambo hilo.

Hivyo maombi ya Toba yana umuhimu sana kama ukijua inachomwomba Mungu.

Ikiwa kuna makosa fulani umeona yamefanyika katika familia yako, na Hivyo unahitaji Mungu awarehemu, unachopaswa kufanya usisali tu juu juu..Bali hakikisha unajitakasa kwanza, kisha unachukua muda wa kufunga kipindi kadhaa, Na katikati ya mfungo huo unamwomba Mungu rehema juu ya hiyo familia yako, au ukoo wako, na makosa yenu, ikijijumuisha na wewe humo humo.

Na akiwezekana kabisa mwisho wa dua zako ambatanisha na sadaka yako kwa Mungu,..Hiyo usiipeleke kwa yatima au watu wasiojiweza hapana, bali ipeleke madhabahuni pa Mungu, kanisani kwako. Kama alivyokuwa anafanya Ayubu, kwa Watoto wake(Ayubu 1:5).

Vivyo hivyo katika kuliombea taifa, au kanisa, maombi ya toba yanakwenda kwa namna hiyo hiyo.

Maombi haya yana nguvu nyingi sana. Na yanafungua vifungo vya aina mbalimbali. Hata na wale wenye dhambi Mungu anaweza kuwarehemu kwa ajili yako tu, kama alivyofanya kwa Danieli na Israeli taifa lake.

Hivyo katika maombi yako ya toba zingatia hivyo vipengele vitatu:

  • Utakaso
  • Mfungo
  • Sadaka ya upatanisho

Bwana akubariki.


Lakini pengine ninayezungumza naye bado hajaokoka, Na yupo tayari kufanya hivyo.

Kama ni wewe basi uamuzi unaoufanya ni wa busara sana ambao hautakaa uujutie maisha yako yote kama ilivyokuwa hata kwetu sisi. Unachopaswa kufanya, hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako. Kisha piga magoti, kisha fuatisha sala hii kwa Imani, ukijua kuwa Mungu yupo hapo karibu na wewe pembeni yako kukusikia..Kisha ukiwa sasa katika utulivu Sema sala hii kwa sauti.

EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU  MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, . NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.

ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.

AMEN

Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithitisha toba yako kwa Vitendo ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo, Sasa Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako. Vile vile unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwambudu Mungu, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.

Ubarikiwe sana

Mada Nyinginezo:

FAIDA ZA MAOMBI.

Nifanye nini ili niwe na uhakika nikifa naenda mbinguni?

NINI NI KILICHOMFANYA IBRAHIMU AKUBALI KUMTOA MWANAWE SADAKA?

 

UMUHIMU WA YESU KWETU.

HUYU MELKIZEDEKI NI NANI?

IMANI NI KUWA NA UHAKIKA WA MAMBO YATARAJIWAYO.

USIPUNGUZE MAOMBI.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments