KUOTA MAFURIKO,KUOTA MAJI MENGI,KUOTA MAWIMBI.

KUOTA MAFURIKO,KUOTA MAJI MENGI,KUOTA MAWIMBI.

Wingu la Mashahidi
Wingu la Mashahidi
KUOTA MAFURIKO,KUOTA MAJI MENGI,KUOTA MAWIMBI.
/

Naomba kufahamu Je! Kuota mafuriko ni kiashiria cha nini?

Mafuriko kazi yake si nyingine Zaidi ya kugharikisha, tofauti na mvua ambayo kazi yake ni kustawisha na kuleta mazao.. Hivyo ikiwa unaota ndoto ya namna hii mara kwa mara, au imekujia mara moja lakini kwa uzito sana, ambao sio wa kawaida basi ujue bila shaka kuwa kuna mafuriko makubwa (rohoni) yapo mbele yako, wengine utakuta wanaota mto umefurika na unataka kuwachukua, na kwa chini maji yake yanakwenda kwa kasi sana, au wengine wanaota wapo baharini na mawimbi makubwa yanakipiga chombo chao kidogo, kisha kinaanza kuyumba yumba na kuanza kuzama, wangine wanaogelewa lakini maji yanawazidia wanashindwa kuendelea mbele..n.k. Hivyo Ukikutana na ndoto yoyote inayohusiana na maji mengi(mafuriko) ujumbe wake ni mmoja, kwamba HATARI IPO MBELE YAKO..Na mafuriko hayo hayaletwi na mwingine zaidi ya shetani.

Sasa ndoto hii inalenga makundi yote mawili.

Kundi la Kwanza:Ni la watu ambao hawajamjua bado Kristo. 

Watu ambao wapo mbali na wokovu, ambao Yesu Kristo hajawabadilisha Maisha yao. Ikiwa wewe ni mmojawapo na umeota ndoto ya namna hiyo, basi ujue kuwa ni Mungu anakuonyesha, ni jinsi gani, mwisho wako utakavyokuwa,..Nataka nikuambie Sikuzote ukiwa nje ya Yesu Kristo hakuna wimbi ambalo halitakuchukua, liwe kubwa au dogo..kwasababu nyumba yako hujaijengwa juu ya mwamba ulio imara..

Sikia Yesu anachokisema…

Mathayo 7:24  “Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;

25  mvua ikanyesha, MAFURIKO YAKAJA, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba.

26  Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga;

27  mvua ikanyesha, MAFURIKO YAKAJA, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa”.

Hivyo inategemea na maisha yako yalivyo, kama wewe ni mlevi basi ujue lipo furiko la mauti ibilisi amekuandalia kukuletea katika huo huo ulevi wako.., kama wewe ni mzinzi basi jiandae na furiko lihusianalo na uzinzi wako ambalo litakuchukua na kukupeleka moja kwa moja mpaka kuzimu..Kama wewe ni mlaji rushwa, ni mwizi, ni tapeli, ni muuaji, ni mshirikina, ni mwabudu sanamu, basi jiandae na furiko la mauti mbele yako..ambalo halitakuachia kichwa wala mkia..Utakwenda moja kwa moja, na ghafla utajikuta kuzimu..kwasababu hiyo ndio nia ya shetani sikuzote..Soma Ufunuo 12:14-17

Kundi la Pili: Watu ambao wameokoka.

Ikiwa wewe upo ndani ya Kristo(Umeokoka).. na unaota ndoto zihusianazo  na mafuriko, basi ujue ni aidha Mungu anakuonyesha hatari iliyopo mbele yako, hila ulizopangiwa na ibilisi hivyo Bwana anataka akuepushe nazo..

Hivyo hapo unapaswa uongeze viwango vyako vya maombi, usiwe mvivu omba kwa bidii, na kudumu katika utakatifu..Kiasi kwamba hata wimbi lolote(mafuriko) la ibilisi likikuta katika mazingira yoyote yale basi huwezi kupepesuka kwasababu umejengwa juu ya mwamba imara Yesu Kristo..

Au namna nyingine ni Mungu anakutahadharisha, utazame vizuri hali yako ya kiroho sasa…Pengine umerudi nyuma na hiyo itakuwa kwako rahisi kuchukuliwa na mawimbi ya mafuriko hivyo unapaswa uimarishe wokovu wako usimame imara..

ZABURI 124

“1 Kama si Bwana aliyekuwa pamoja nasi, Israeli na aseme sasa, 

2 Kama si Bwana aliyekuwa pamoja nasi, Wanadamu walipotushambulia. 

3 Papo hapo wangalitumeza hai, Hasira yao ilipowaka juu yetu 

4 Papo hapo maji yangalitugharikisha, Mto ungalipita juu ya roho zetu; 

5 Papo hapo yangalipita juu ya nafsi zetu Maji yafurikayo. 

6 Na ahimidiwe Bwana; Asiyetutoa kuwa mawindo kwa meno yao. 

7 Nafsi yetu imeokoka kama ndege Katika mtego wa wawindaji, Mtego umevunjika, nasi tumeokoka. 

8 Msaada wetu u katika jina la Bwana, Aliyezifanya mbingu na nchi”.

Amen.

Je! Ungependa kuokoka leo?

Ni vizuri ukafanya maamuzi hayo haraka..Usijiangalie labda wewe ni muislamu, au ni mkristo..ikiwa Kristo yupo mbali na wewe, haijalishi ulizaliwa katika dini au la, maisha yako sikuzote yatakuwa hatarini..Leo hii sikuambii umpe YESU Maisha yako, ili kusudi kwamba hatari hizo zisikukute mbeleni..Hapana pamoja na hayo ndani ya Kristo zipo faida nyingi utazipata..Kwanza kabisa atakupa uzima wa milele, Na Pili anakupenda na anakuhitaji wewe mwana wake uliyepotea.. aliyekuumba ukae katika uwepo wake..Umfurahie yeye na yeye akufurahie wewe.

Hivyo Ikiwa upo tayari leo hii Yesu aingie ndani yako..Na umemaanisha kweli kutaka kubadilika na akuokoe Maisha yako na dhambi zako zote basi..

Basi uamuzi unaoufanya ni wa busara sana ambao hautakaa uujutie maisha yako yote kama ilivyokuwa hata kwetu sisi. Unachopaswa kufanya, hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako. Kisha piga magoti, kisha fuatisha sala hii kwa Imani, ukijua kuwa Mungu yupo hapo karibu na wewe pembeni yako kukusikia..Kisha ukiwa sasa katika utulivu Sema sala hii kwa sauti.

EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU  MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, . NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.

ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.

AMEN.

Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithitisha toba yako kwa Vitendo ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo, Sasa Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako. Vile vile unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwambudu Mungu, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.

Ubarikiwe sana

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312

   Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Mada Nyinginezo:

KUOTA UPO UCHI.

BONDE LA KUKATA MANENO.

NINI KINAFUATA SIKU ILE ILE YA KUOKOKA!

UVUMILIVU WA MUNGU ULIPOKUWA UKINGOJA.

TUUTAZAME PIA MWISHO WA UJENZI WETU.

UNYAKUO.

CHUKIZO LA UHARIBIFU

KWANINI WENGINE WANYAKULIWE,NA WENGINE WAACHWE?

TOA SADAKA ISIYO NA KASORO KWA BWANA.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
6 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Jerico mwanisawa
Jerico mwanisawa
2 years ago

Mimi afya yangu unasumbuliwa na magonjwa Mara KWA Mara nahitaji MSAADA wa Mambo.

Kudra
Kudra
3 years ago

Nimeota ndoto ya mafuriko kwa kiasi kikubwa,pia nahitaji maombi mwili wangu dhaifu

Florence Murugi kamau
Florence Murugi kamau
3 years ago

Mamangu ni mgonjwa Sanaa nahitaji maombi yeni

Zephania
Zephania
3 years ago

Shalom ningependa kuuliza je ukiota unaona nyota zipokimakundii nyingi halafu unaona kama unyayo wamguu ukiwa kama umezikanyaga…halafu tena baada yahapo unaota zipo zenyewe tuu ….nikaota tena Siku nyingine hizohizo nyota ninaziona angani tena mbili zikiwa zinakimbia kwaspeedi kubwa zikiwa na uwino sawia