KUOTA UNANG’OKA MENO.

KUOTA UNANG’OKA MENO.

Hii ni moja ya ndoto inayootwa na watu wengi, ikiwa na wewe ni mmojawapo na inajirudia rudia  mara kwa mara basi fahamu kuwa lipo jambo ambalo Mungu anataka kukukumbusha, Sikuzote meno yanafanya kazi mbili kuu, ya kwanza ni kumeng’enya na ya pili ni kung’ata,..asilimia kubwa ya viumbe vyote vinatumia meno kwa kazi mojawapo ya hizo, isipokuwa tu mwanadamu inaongezeka nyingine hapo, ambayo ni kuzungumza, mtu usipokuwa na meno huwezi kuzungumza, atatoa sauti tu zisizoeleweka…

Vilevile Mtu Ukipoteza meno huwezi kula vitu vigumu, wala huwezi kung’ata kitu chochote Na ndio maana mtu unapoota meno yake aidha  ya juu au ya chini au magego yanang’oka halafu ghafla ukashtuka saa hiyo hiyo  na kujiona yupo salama huwa anashukuru kweli, anasema afadhali imekuwa ndoto, ni kwasababu unajua thamani iliyo katika meno yake.

Sasa ukiota meno yanatoka Hapo ni Mungu anakukumbusha, kuwa unakaribia kupoteza Meno yako ya rohoni, yenye thamani kubwa zaidi ya haya ya mwilini, ikiwa hujaokoka basi nakushauri  utubu haraka sana, umegukie Mungu wako, kwasababu mara kikipotea hicho basi fahamu kuwa kitapotea milele…Ukishaondolewa  uwezo wako wa kupambanua na kuyaelewa  mambo ya rohoni basi hutakaa uwe nao tena, ukishaondolewa uwezo wako wa kung’ata maadui zako wa rohoni kwa meno makali Mungu aliyokupa basi fahamu utabakia hivyo milele, Vilevile Ukishaondolewa uwezo wa kuzungumza na Mungu wako rohoni basi ndio utabikia hivyo milele na milele hatakaa  akuelewe wewe, hiyo inamaanisha hata ukiomba dua yao hawezi kukusikia…Na hiyo yote ni kwasababu ya dhambi zako unazozitenda sasa hivi.

Zaburi 58:3 “Wasio haki wamejitenga tangu kuzaliwa kwao; Tangu tumboni wamepotea, wakisema uongo.

4 Sumu yao, mfano wake ni sumu ya nyoka; Mfano wao ni fira kiziwi azibaye sikio lake.

5 Asiyeisikiliza sauti ya waganga, Ijapo wanafanya uganga kwa ustadi.

6 Ee Mungu, UYAVUNJE MENO YAO VINYWANI MWAO; Ee Bwana, uyavunje magego ya wana-simba.

7 Na watoweke kama maji yapitayo kwa kasi; Akiielekeza mishale yake, iwe imetiwa ubutu”.

Ndugu Usiipuuzie Injili ya msalaba hata kidogo, inapohubiriwa mbele zako, Mungu ameona jambo hilo kwako na hivyo anakuonya kwasababu anakupenda, mgeukie muumba wako, anza kuzingatia Neno lake kile anachokuambia tii na yeye mwenyewe atakuokoa na kukulinda na kukuongoza hadi unyakuo.

Aidha kama wewe tayari upo ndani ya Kristo, na unaota ndoto za namna hiyo hapo Mungu anakuonyesha pia ni jinsi gani unaelekea kupoteza ule uwezo wako wa thamani uliokuwa nao wa kupambanua  mambo ya rohoni na ukali wako, hivyo simama imara kama ulikuwa umeshaanza kuyumba yumba,  au kupoa simama imara ili usije ukabakia kuwa mbwa bubu tu asiyeweza hata kubweka rohoni (kukemea dhambi )kwa kukosa meno.

Isaya 56:10 “Walinzi wake ni vipofu, wote pia hawana maarifa; wote ni mbwa walio bubu, hawawezi kulia; huota ndoto, hulala, hupenda usingizi.

11 Naam, mbwa hao wana choyo sana, hawashibi kamwe; na hao ni wachungaji wasioweza kufahamu neno; wote pia wamegeuka upande, wazifuate njia zao wenyewe, kila mmoja kwa faida yake, toka pande zote.

12 Husema, Njoni, nitaleta divai, Na tunywe sana kileo; Na kesho itakuwa kama leo, Sikukuu kupita kiasi”.

Zingatia hayo na Bwana hakika atakuwa na wewe katika kila hatua moja unayopiga kwake…Hizi ni siku za mwisho na Unyakuo wa kanisa upo karibuni, tengeneza mambo yako.

Ubarikiwe.

Group la whatsapp Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi


Mada Nyinginezo:

KUOTA UNAENDESHA GARI.

KUOTA UPO UCHI.

KUOTA UNAFANYA MTIHANI.

JE! KUBET NI DHAMBI?

JE! NI KWELI KUNA VIUMBE VINAVYOISHI SAYARI NYINGINE (ALIENS)?

UBATILI.


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Leave a Reply