SWALI: Nini maana ya Mhubiri 10:9 Mwenye kuchonga mawe ataumizwa kwayo; Naye apasuaye miti huona hatari katika hiyo.
JIBU: Mstari huu unatuonyesha hatari ya kazi yoyote inayotendwa na mtu. Hapo ametumia mfano wa wanaochonga mawe. Wajenzi wa zamani walikwenda kuchonga mawe miambani kwa ajili ya ujenzi wa majengo yao, lakini wakiwa kule walikutana na hatari nyingi, aidha kuangukiwa na mawe hayo, na kuwaponda viungo vyao, vifaa vyao vya uchongaji kuwajeruhi.
Vilevile anatumia tena mfano wa wanaopasua miti, kwa ajili ya mbao za ujenzi, bado na wao pia wanakutana na hatari, aidha kuangukiwa na miti yenyewe, au shoka kuteleza na kumjeruhi mtu au yeye.
Kumbukumbu 19:5 kama aingiapo mtu na mwenziwe mwituni kwenda kukata kuni, akapeleka mkono wake na shoka ili kukata mti, likatoka shoka katika mpini, likampiga yule mwenziwe hata akafa; basi na akimbilie katika miji hii mmojawapo awe hai.
Ni sawa na mjenzi ambaye amezoea kupiga sana nyundo au kuwepo maeneo ya ujenzi muda wake mwingi, utaona upo wakati nyundo itateleza na kumponda kidole chake, au atakanyaga msumari n.k. Tofauti na kama angekuwa hajishughulishi na kazi hiyo yupo nyumbani tu.
Hii ni kufunua nini rohoni?
Kama wana wa Mungu tufahamu kuwa kazi yake ya kwenda kung’oa mapando ya mwovu, katika shamba la Bwana tutarajie kukutana na madhara yake, si wakati wote utakuwa ni mwepesi tu (yaani kuvuna), zipo nyakati tutakutana na kupigwa, au kudhalilishwa, au kufungwa na wakati mwingine hata kuuawa. (Mathayo 10:17-19)
Mtume Paulo alipokuwa katika ziara zake za kupanda ukristo Asia na Ulaya, alikutana na hatari nyingi, ikiwemo kupigwa mawe na watu wabaya, kufungwa, na kurushiwa vitisho mbalimbali. Wamishionari kama dr David Livingstone walioleta injili Afrika zamani walikutana na hatari za magonjwa kama malaria, na wanyama wakali.
Lakini katika yote, Bwana ameahidi, mafanikio makubwa, kuliko hatari zake. Hivyo hatupaswi kuogopa na kudhani kuwa kazi ya Mungu ni kazi ya kwenda kujichinja wakati wote. Hapana, zipo nyakati nyingi za raha, na mafanikio makubwa ya rohoni yasiyokuwa na ghasia yoyote, lakini Bwana hajatuficha pia hatari zake wakati mwingine. Ili tutakapokutana nazo tusihuzunike moyo na kukata tamaa, bali tuendelee na kazi.
Bwana akubariki.
Je! Umeokoka? Je! Umesamehewa dhambi zako? Kama ni la, ni nini kinachokusubirisha? Ukifa leo utakwenda wapi, kumbuka lipo ziwa la moto, kumbuka ipo hukumu kwa waovu. Tubu leo mgeukie Kristo akusafishe dhambi zako, Ukabatizwe katika jina la Yersu Kristo upokee ondoleo la dhambi. Hizi ni siku za mwisho, Kristo anakaribia kurudi.
Ikiwa upo tayari leo kufanya hivyo basi fungua hapa kwa mwongozo huo>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618. Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
Mafundisho mengine:
Yeye abomoaye boma, nyoka atamwuma.
Je! fedha ni jawabu la mambo yote? (Mhubiri 10:19).
TUUTAFUTE UMOJA WA ROHO.
Fahamu maana ya Mithali 28:20 Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele;
NI KWA NAMNA GANI SHETANI ANAIZUIA INJILI?
FANYA MAAMUZI KABLA HAZIJAKARIBIA SIKU ZA HATARI.
Rudi nyumbani
Print this post