USIKWEPE CHUO CHA UTAKATIFU.

by Admin | 17 November 2023 08:46 pm11

Zawadi kubwa Mungu aliyompa mwaminio ni UTAKATIFU. 

Utakatifu ni ile hali kuwa mkamilifu kama Mungu, kutokuwa na dosari au kasoro yoyote, msafi asilimia mia moja, bila kosa lolote ndani yako. 

Sasa heshima hii tumetunukiwa na Mungu, jambo ambalo hapo zamani halikwepo, ilihitaji matendo ya haki ya Mtu kuufikia, lakini hapakuwahi kutokea mwanadamu yoyote aliyeweza kufikia cheo hicho cha juu sana cha Mungu, yaani kutokuwa na dhambi kabisa.

Lakini pale tunapomwamini Bwana Yesu, siku hiyo hiyo, Mungu anatufanya Watakatifu kama yeye, haijalishi bado tutakuwa na asili ya dhambi nyingi kiasi gani. Hiyo ndio maana ya neema. Tunaitwa watakatifu bila ya kujisumbua kwa lolote.

Lakini sasa lengo la Mungu sio tuwe “watakatifu katika dhambi” Bali “tuwe watakatifu katika utakatifu”. Hivyo kuanzia huo wakati anaanza kumfundisha mtu kuusomea hadi kuuhitimu Utakatifu wake,aliopewa ili aendane na cheo alichotunukiwa tangu mwanzo.

Na hapo mtu akishindwa kupiga hatua, basi anaondolewa heshima hiyo kwake, na hivyo hawezi tena kuwa kama Mungu, na matokeo yake wokovu unampotea.

Mwaka Fulani hapa nchini kwetu kulikuwa na askari mmoja aliyeonyesha kitendo cha kishujaa kukataa rushwa ya milioni 10, ambapo alishawishiwa aipokee ili aifute kesi ya watuhumiwa wawili waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka,. Lakini yeye hakukubali, na ilipokuja kubainika, mkuu wa jeshi la polisi (IGP) akafurahishwa naye, Akampandisha cheo (kwani alikuwa ni askari wa chini). Lakini cha kushangaza baada ya kama miaka mwilini tukaja kusikia Yule askari aliyepandishwa cheo ameshushwa cheo kile. Kufuatilia ni kwanini imekuwa hivyo? Jeshi la polisi likatoa taarifa kuwa alionyesha utovu wa nidhani, wa kukataa kwenda kwenye mafunzo ya cheo chake kipya.  Akidhani kwasababu IGP amempandisha basi inatosha hakuna haja ya mafunzo tena. Akasahau kuwa ufahamu wake wa kielimu ni lazima uendane na cheo chake, kwamba akiwa bado na cheo kikubwa, wakati huo huo anapaswa aendelee kusoma,na kujifunza kimatendo, ili aweze kutumika ipasavyo. Lakini akashushwa cheo na kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa kukataa kutii amri ya jeshi.

Ndivyo ilivyo katika UTAKATIFU tunaopewa na Mungu bure, ni lazima tuutendee kazi kwa kila siku kupiga hatua mpya ya mabadiliko. Huwezi kusema umeokoka (wewe ni mtakatifu), halafu maisha yako ya mwaka jana na mwaka huu ni yaleyale wewe sio mtakatifu.  Kila siku lazima uwe na mabadiliko, ulikuwa unabeti, unaacha kubeti, ulikuwa unavaa mavazi ya uchi uchi, unayachoma moto, ulikuwa unajichubua, unaacha, ulikuwa unasengenya unakaa mbali na wasengenyaji, ulikuwa unakesha kwenye muvi usiku kucha unaacha hayo, unatumia muda wako mwingi kwenye kujisomea biblia, ulikuwa ni mtu wa rushwa unaanza kuondoa vitendo hivyo kwenye biashara yako. Ulikuwa huwezi kufunga na kuomba unaanza kujizoeza kuwa mtu wa rohoni, unafunga, unaomba, na kukesha, Huko ndiko Mungu anakokutaka. Anaona umekiheshimu cheo alichokupa.

Ukiwa ni mtu wa kupiga hatua kila siku, basi Mungu atazidi kukuona wewe ni MTAKATIFU na hivyo utakuwa karibu na yeye. Lakini ukiishi hoe hae, hutambuliki kama umeokoka, au vipi, tabia zilezile za zamani unaendelea nazo, wala hujihangaishi kuziondoa. Usijindanganye wewe umeokoka.

Bwana atusaidie..

Je! Upo ndani ya Kristo? Je unataarifa kuwa hizi ni siku za mwisho? Yesu amekaribia kurudi? Ni nini utamweleza Mungu siku ile endapo leo utaukataa wokovu unaoletwa kwako bure..  Tubu dhambi zako, mgeukie Bwana, akupe Roho Mtakatifu, akupe heshimu hiyo ya utakatifu. Hivyo Ikiwa upo tayari kufanya hivyo basi fungua hapa kwa ajili ya mwongozo wa sala ya toba >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group

Mada Nyinginezo:

FUNDISHO KUU LA NEEMA YA MUNGU KWETU.

MATUNDA 9 YA ROHO MTAKATIFU

UTAKASO NI SEHEMU YA MAISHA YA MKRISTO YA KILA SIKU.

USITAZAME NYUMA!

Kwanini hatuirithi neema kama tunavyoirithi dhambi?

HATARI YA KUHUBIRI INJILI TOFAUTI NA ILIYOANDIKWA KWENYE BIBLIA.

Wakili ni nani kibiblia? Uwakili ni nini?

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2023/11/17/usikwepe-chuo-cha-utakatifu/