Ni laana ipi hiyo Mungu alimaanisha ataipiga dunia nayo katika Malaki 4:5-6?

Ni laana ipi hiyo Mungu alimaanisha ataipiga dunia nayo katika Malaki 4:5-6?

SWALI: Malaki 4: 5”Angalieni,nitawatumia Eliya nabii,kabla siku ile ya BWANA,iliyo kuu na ya kuogofya haijafika.Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao,na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ILI NISIJE NIKAIPIGA DUNIA KWA ‘Laana’…Hapo anamaanisha [LAANA kwa namna gani] au LAANA Ipi?.


JIBU: Mahali popote Mungu anapozungumzia kuipiga dunia, anamaanisha kwa mapigo kama yale yaliyotokea wakati wa Nuhu, na ule wakati wa Sodoma na Gomora,..

Kumbuka wakati ule wa Nuhu, watu walikuwa sio wa kujizuia na hiyo ikasababisha watu kujisahau kupindukia na hiyo yote ni kwasababu hakukuwa na manabii wa kutosha wa kuwaonya..Vile vile hata wakati wa utawala wa Mfalme ahabu, kama Eliya asingetumwa na Mungu kuwageuza watu mioyo iwaelekee Mungu, katika kipindi kile cha kilele cha maovu Israeli ambapo ibada za sanamu na miungu ilikuwa ni jambo la kawaida vikiongozwa na Yezebeli, walikuwa wamebakiwa na muda mchache sana kabla ya kuangamizwa kwao..Lakini kwasababu Mungu alilihurumia Taifa lake teule na viapo alivyomuapia Ibrahimu, basi alikuwa akiwatumia manabii wake wengi wawe wanawaonya mara kwa mara. 

Vivyo hivyo katika agano jipya, kama Mungu asingeachia Roho wake mtakatifu, na asingepeleka watumishi wake mitume na manabii kuhubiri duniani kote kuwaonya watu wamgeukie Mungu, dunia hii isingekuwepo mpaka leo hii..Tunaona tokea kipindi cha kanisa la kwanza Mungu amekuwa akiwatuma watumishi wake kwa Roho ile ile ya Eliya kuwarejesha watu wamegukie Mungu.. 

Hadi kanisa hili la mwisho la Laodikia tulilopo sasa tunaona aliwatuma watumishi wake wengi, akiwemo William Branham kwa ujumbe wa kuwarejesha watu wamgeukie Mungu..Na hata sasa bado anaendelea kuwatuma wengine wengi kwa huduma hiyo….. ikiwa utapenda kufahamu kuwa urefu juu ya huduma ya Eliya jinsi inavyotenda kazi katika agano jipya, nitumie ujumbe inbox nikutumie somo lake kwa urefu kwasababu hapa hatuwezi kuliandika lote.. Lakini ipo siku Injili hii ya kuonywa na kukumbushwa itakoma..Wala Mungu hataipeleka Roho yake tena juu ya watumishi wake kuigeuza mioyo ya watu imwelekee Mungu..Wakati huo ukifika basi ndio KIAMA chenyewe..

Hasira ya Mungu au LAANA ya Mungu itaakwenda kuachiliwa juu ya dunia nzima.. Kama Mtume Petro alivyoandika.. 

2 Petro 3:9 “Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.

10 Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.

11 Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa,

12 mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka?”.

Bwana akubariki.

HOME

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Prophet: FP. Misigalo
Prophet: FP. Misigalo
2 years ago

ikiwa utapenda kufahamu kuwa urefu juu ya huduma ya Eliya jinsi inavyotenda kazi katika agano jipya, nitumie ujumbe inbox nikutumie somo lake kwa urefu kwasababu hapa hatuwezi kuliandika lote.

NINAOMBA SOMO HILI…