JIBU: Hata katika hali ya kawaida mtu anapozungumza maneno mengine ya uongo ambayo wewe hujasema mtu huyo ni sawa na kakuongezea maneno… Kwamfano mtu anapokwenda kutoa ushahidi mahakamani ya kwamba amekusikia ukisema maneno Fulani na angali wewe hujasema hayo maneno,na anafanya vile kwa makusudi mtu huyo atakuwa ni kama amekuongezea maneno, Vivyo hivyo na kwa Mungu mtu anapotoa ushuhuda wa uongo kuhusu Mungu, au anapofundisha jambo la uongo kinyume na Neno la Mungu na anafanya vile makusudi kwa nia ya kupotosha, mtu huyo ni sawa na ameongeza neno katika maneno ya Mungu na Biblia inasema ataongezewa mapigo katika siku ile (Ufunuo 22:18).
Kwamfano maandiko yanasema “Mtu ameandikiwa kufa mara moja na baada ya kifo ni hukumu Waebrania (9:27)” Lakini inatokea mwalimu au mtumishi analijua hilo andiko na maana yake lakini badala ya kuwafundisha watu hilo, anawapotosha na kuwaambia hakuna hukumu baada ya kufa, au mtu baada ya kufa anakwenda toharani kutakaswa kisha mbinguni baadaye hata kama alikufa katika dhambi, Hivyo anaendelea kuwafariji watu wazidi kudumu katika dhambi zao..huyo ni sawa na ameongeza Neno katika maneno ya Mungu..
Kadhalika kupunguza maneno inatokea pale mtu anapoujua ukweli na hauhubiri wote kama inavyopaswa, pengine kwa hofu Fulani, au kwasababu anaogopa kutengwa, au kuchukiwa…mtu kama huyo ni sawa na amepunguza Neno kati ya maneno ya Mungu, na hivyo atapunguziwa sehemu yake (yaani thawabu yake) katika ule mti wa Uzima, na katika ule mji Mtakatifu Yerusalemu ya Mungu katika siku ile.(Ufunuo 22:19).
Kwamfano Maandiko yanasema Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; KWA MAANA KILA AFANYAYE MAMBO HAYO NI MACHUKIZO KWA BWANA, MUNGU WAKO. (Kumbu.22:5), sasa kwamfano Mwalimu, au muhubiri au mchungaji, akilijua hili na hawafundishi wanafunzi wake , au washirika wake,mambo kama hayo kwa hofu Fulani labda watamchukia, au watamkimbia sasa mtu kama huyu ni sawa na amepunguza Neno katika Maneno ya Mungu na hivyo sehemu yake pia itapunguzwa katika mji ule.
Kwahiyo tunapaswa tulichukue Neno la Mungu kama lilivyo bila kupunguza makali yake, au kuongeza shuhuda zipinganazo na Neno la Mungu kwa lengo la kuwapotosha watu.
Ubarikiwe.
Mada zinazoendana:
NENO LA MUNGU KATIKA UTIMILIFU WOTE.
TABIA YA KIPEKEE USIYOIJUA KUHUSU NENO LA MUNGU.
USIACHE KUJIFUNZA NENO LA MUNGU
MANENO YA MUNGU YANAPINDULIWAJE?
UMEFUNULIWA AKILI?
VIFUNGO VYA GIZA VYA MILELE.
Rudi Nyumbani:
Print this post