Kitanga/Vitanga ni nini?

Kitanga/Vitanga ni nini?

Kibiblia Kitanga ni sehemu ya mwisho wa mkono wa Mtu, au mnyama..kwa jina lingine ni kiganja.

Neno hilo utalisoma katika vifungu hivi.

Danieli 5:24-25
[24]Ndipo kile kitanga cha ule mkono kikaletwa kutoka mbele zake, na maandiko haya yameandikwa.
[25]Na maandiko yaliyoandikwa ni haya; MENE, MENE, TEKELI, NA PERESI.

Huu ni ule wakati mfalme Belshaza wa Babeli alipokuwa ameketi nankufanyia anasa vyombo vitakatifu vya Mungu pamoja na makahaba wake..ndipo hapo hapo kiganja cha mkono kikatokea na kuanza kuandika ukutani maneno hayo, mene mene tekeli na peresi.

Utalisoma Neno hilo pia katika vifungu hivi.

Mambo ya Walawi 14:26-27
[26]kisha kuhani atamimina sehemu ya hayo mafuta katika kitanga cha mkono wake mwenyewe wa kushoto;
[27]kisha kuhani atanyunyiza baadhi ya hayo mafuta yaliyo katika mkono wake wa kushoto, kwa kidole chake cha mkono wa kuume mara saba mbele za BWANA;

Mambo ya Walawi 11:27
[27]Tena kila mnyama aendaye kwa vitanga vyake, katika hao wanyama wote waendao kwa miguu minne, hao ni najisi kwenu; awaye yote atakayegusa mizoga yao, atakuwa ni najisi hata jioni.

Isaya 49:16
[16]Tazama, nimekuchora katika vitanga vya mikono yangu; kuta zako ziko mbele zangu daima.

Soma pia; ( 2Wafalme 9:35, Danieli 10:10,

Lakini Je nini tunaweza kujifunza kila tutazamapo kitanga/ vitanga vyetu.?

Ukiwa mwovu..kumbuka kuwa siku moja kitanga cha Mungu kitakuandikia hukumu kama kilivyomwandikia Belshaza mfalme wa Babeli..kama wewe ni mfanyaji wa anasa, ni mzinzi, ni mlevi, ni mchawi, unaabudu sanamu..Bwana atakuadhibu kwa hukumu mbaya sana. Ya mene, mene, tekeli na Peresi.

Ukifikia hii hatua basi habari yako inakuwa imeishia hapo hapo.

Lakini ikiwa wewe unampenda Mungu na kumcha yeye, na kuyafanya maagizo yake..Vilevile ameahidi atakuandika katika vitanga vyake…ikiwa na maana mtu akiandika jambo katika kiganja chake lengo lake ni ili asikusahau, si ndio?..Ndivyo ilivyo kwa Mungu, kwa watu wake wampendao..amewaandika katika viganja vyake kamwe hawezi kuwasahau.

Isaya 49:14-16
[14]Bali Sayuni alisema, YEHOVA ameniacha, Bwana amenisahau.
[15]Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe.
[16]Tazama, nimekuchora katika vitanga vya mikono yangu; kuta zako ziko mbele zangu daima.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

Makanwa ni nini katika biblia? (Danieli 6:22)

Kwa jina lake Ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa.

Nini maana ya.. “Utoapo sadaka mkono wako wa kuume usijue ufanyalo mkono wako wa kushoto”

Kutia mkono chini ya paja kama ishara ya kiapo, kulimaanisha nini?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments