Je! Sulemani alienda mbinguni?

Je! Sulemani alienda mbinguni?

JIBU: Jibu ni ndio.

Kosa alilolifanya Sulemani la kushawishiwa na wake zake kuwajengea madhabahu miungu, (1Wafalme 11:3:13) maandiko hayatuthibitishii kuwa lilikuwa ni endelevu, kana kwamba alimwacha Mungu moja kwa moja, hapana, au alitenda dhambi isiyosameheka kabisa hapana. Ni wazi kuwa Sulemani alitubu, kwa kosa lile, tunaposoma kitabu cha Mhubiri ambacho alikiandika katika uzee wake, kinatupa picha ya mambo mengi ambayo aliyatenda au aliyadhania kuwa ni sawa lakini mwisho wake akagundua ni ubatili ni sawa na kuufuata upepo. Na ndio maana mwisho kabisa akahitimisha, kuwa jumla ya yote yampasayo mtu ni kumcha Bwana na kuepukana na uovu. Kuonyesha kuwa Sulemani aligundua usahihi upo wapi, kabla hajafa.

Lakini pia asingetajwa katika vizazi vya ukoo wa  Bwana Yesu kama angekuwa ni mmojawapo wa waliopotea. Hivyo hatuwezi kusema kuwa Sulemani alikwenda kuzimu, hata kama hakuna maandiko ya moja kwa moja yanayoonyesha mahali alipotubu.

Kikubwa tujifunze katika kosa alilolifanya. Maandiko yanasema kutii ni bora kuliko dhabihu. Kama Sulemani angetii agizo la Bwana la kutokuoa wanawake wa-kimataifa, hayo yote yasingemkuta. Lakini alidhani kwa hekima zake kuwa nyingi asingeweza kudanganyika. Ndio alikuwa mjanja mwanzoni katika ujana wake, lakini sekunde za mwisho za uzee wake shetani alimpiga mweleka. Zipo dhambi ambazo shetani anakuandalia uzitende baadaye, lakini maandalizi yake anayatengeneza sasa.  Tii kila agizo la Mungu, hata kama ni dogo kiasi gani, hata kama litaonekana ni jepesi kulishinda kiasi gani sasa, wewe tii, kwasababu Mungu anaona mbele wewe unaona hapa. Simama katika Neno, sio katika mitazamo yako, ndipo utakapoweza kumshinda shetani, ikiwa wenye hekima kama hawa walinaswa katika tundu bovu wewe ni nani usinasike pindi unapolipuuzia Neno la Mungu linalokusemesha moyoni mwako uache hiyo tabia au hiyo dhambi?.

Bwana atusaidie.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

SHAMBA HUWA HALIMTAMBUI WALA KUMSUBIRIA MKULIMA.

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 11 (Mithali, Wimbo ulio bora, Mhubiri)

Kile kinara cha Taa ndani ya Hekalu la Sulemani kilikuwa kinawakilisha nini?

Mwandishi wa kitabu cha Zaburi ni nani?

Nchi ya Nodi ambayo Kaini alikimbilia ndio nchi gani kwasasa?(Mwanzo 4:16).

Ni kosa gani lililowafanya wana wa israeli wawe watumwa miaka 400 Misri?.

Mithali 24:17 inamaana gani kusema Tengeneza kazi yako huko nje?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments