ORODHA YA MITUME.

ORODHA YA MITUME.

Hii ni Orodha ya Mitume 12 wa Bwana YESU.

  1. SIMONI-aliyeitwa PETRO.
  2. ANDREA- Ndugu yake Simoni Petro.
  3. YAKOBO- Mwana wa Zebedayo.
  4. YOHANA- Mwana wa Zebedayo.
  5. FILIPO.
  6. BARTHOLOMAYO-  Au jina lingine Nathanaeli (Yohana 1:45)
  7. THOMASO.
  8. MATHAYO- Mtoza Ushuru.
  9. YAKOBO- Mwana wa Alfayo
  10. THADAYO- Aliyeitwa jina lingine “Yuda mwana wa Yakobo” (Luka 6:16)
  11. SIMONI – Mwenyeji wa Kana (Mkananayo) ambaye aliitwa jina lingine “Simoni Zelote (Matendo 1:13 na Luka 6:15)
  12. YUDA- Mwenyeji wa Keriothi (Iskariote)-Ndiye aliyemsaliti Yesu.

Orodha hii inapatika katika Kitabu cha Mathayo 10:2-4, na kitabu cha Marko 3:18, na Luka 6:13-16.

Katika Vitabu hivyo panaonekana Mitume kutajwa kwa jina Zaidi ya Moja katika injili nyingine, kwamfano Mtume aliyeitwa Thadayo (Mathayo 10:3),  kitabu cha Luka 6:16 anaonekana akitajwa kama “Yuda wa Yakobo”, Hiyo ni kuonyesha kuwa Mtume huyo alikuwa  anajulikana kwa jina Zaidi ya moja. Vile vile Mtume anayeonekana kuitwa Nathanaeli katika Yohana 1:45 ndio huyo huyo anayekuja kuoenakana akiitwa kwa jina la Bartholomeo katika Mathayo 10:3.

Lakini pia baada ya Yuda kumsaliti Bwana na kwenda kujinyonga, maandiko yanaonyesha kuwa Mtu aliyeitwa Mathiya alichukua nafasi yake na kuhesabiwa miongoni mwa mitume 11 wa Bwana Yesu.

Matendo 1:26 “Wakawapigia kura; kura ikamwangukia Mathiya; naye akahesabiwa kuwa pamoja na mitume kumi na mmoja”.

Hiyo ndiyo Orodha ya Mitume 12 wa Bwana Yesu Kristo, ambao Bwana aliwaweka kuwa kama Mashahidi wa kufufuka kwake (Matendo 10:39-42 na Matendo 1:22), na baada ya hawa Bwana alinyanyua mitume wengine mfano wa hawa, ambao miongoni mwao alikuwa Mtume Paulo.

Na Mitume wanatajwa katika Agano jipya tu na wao ndio walioweka msingi wa Imani kwa kanisa, katika Agano la kale walioweka msingi wa kumjua Mungu kama Yehova ni Manabii, hivyo kwa muunganiko wa Mafunuo waliopewa Mitume wa agano jipya na Manabii wa agano la kale, kanisa la Kristo linajegwa juu ya Msingi wao.

Waefeso 2:20 “Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni”.

Je unajua jinsi Bwana alivyowachagua Mitume wake? na ni kigezo gani aliitumia?.. kufahamu zaidi fungua hapa >>JINSI BWANA ALIVYOWACHAGUA MITUME WAKE.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Je ni kweli Tumejengwa juu ya Mitume na Manabii? (Waefeso 2:20)

Orodha ya mistari ya biblia kuhusu watoto

ORODHA YA IMANI POTOFU- Sehemu ya 1

YEZEBELI ALIKUWA NANI

JINSI YA KUPIGANA MAOMBI YA VITA.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments