ORODHA YA IMANI POTOFU- Sehemu ya 1.

ORODHA YA IMANI POTOFU- Sehemu ya 1.

Hii ni orodha ya Imani potofu, ambazo ndani yake zina uongo, unaotaka kukaribiana na ukweli.

1.IMANI YA MUNGU BABA.

Hii ni imani ya kwanza ambayo ni ya kujihadhari nayo kwasababu ni kutoka kwa Yule Adui asilimia mia moja. Imani hii inaelekeza kuwa Mamlaka ya Bwana Yesu duniani sasa hivi haipo!, imekwisha na sasa iliyopo ni mamlaka ya Mungu Baba!.

Imani hii inazidi kuelekeza kuwa unyakuo wa kanisa ulishapita, na hakuna chochote sasa tunachokisubiri, na hakuna haja ya utakatifu wa nje!

Imani hii haimtaji shetani kama shetani, bali inamtaja shetani kama “Kerubi”, jambo ambalo sio sahihi, kwasababu shetani alikuwa kerubi alipokuwa mbinguni lakini sifa hiyo aliipoteza baada ya kutaka kuabudiwa, na kutupwa chini akalaaniwa na kuwa shetani,  kwahiyo sasahivi haitwi tena Kerubi, bali shetani na ibilisi, Yule joka!.. Makerubi wamebaki mbinguni, wakimtukuza Mungu na kumwabudu, ambao ni watakatifu na wasafi.

Ufunuo 12:9  “Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, AITWAYE IBILISI NA SHETANI, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye”

Imani hii imeanzia Afrika mashariki, katika nchi ya Tanzania, Mwaka 2003 na muasisi wa Imani hiyo, alijiita Eliya na Adamu wa pili, shetani anaipalilia kwa kasi imani hii na inalenga lile kundi ambalo halipendi kusoma Neno, bali linasubiria tu kupokea na kutazama uzuri wa nje!..

Tahadhari: Mathayo 7:15  “Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.

16  Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?

17  Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya”.

2. IMANI YA IBADA ZA WAFU.

Hii ni imani inayoamini kuwa wafu wanaweza kutuombea, au tunaweza kuwaombea!..Imani hii inapatikana katika dini nyingi na madhehebu mengi, ikiwemo dini ya kikatoliki. Imani hii ni imani kutoka kwa shetani asilimia mia moja! Na haina ukweli wowote kimaandiko. Lengo la shetani kuizindua imani hii duniani ni ili kuwatumainisha watu kuwa kunayo nafasi nyingine ya kutengeneza mambo baada ya kifo!..

Hivyo kwa wanaoifuata inawafanya wastarehe katika dhambi zao!.. wakiamini kuwa hata wakifa watakatifu waliopo duniani watawaombea na Mungu atawapunguzia adhabu..

Neno la Mungu linasema kuwa mpatanishi wa sisi na Mungu ni YESU TU PEKE YAKE!...

1Timotheo 2:5-6  “Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu; ambaye alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wote, utakaoshuhudiwa kwa majira yake”

Na anatupatanisha si kwa kusubiri tufe! Hapana! Bali angali tukiwa hai baada ya kumwamini!.. Tukifa katika dhambi zetu kazi yake yakutupatanisha na Mungu inakuwa haipo, tutakachokuwa tunangoja baada ya hapo ni hukumu!… yeye mwenyewe alisema hivyo katika Yohana 8:24

Yohana 8:24  “Kwa hiyo naliwaambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu”.

Na ndio maana kuna umuhimu wa kumpokea Yesu na kuoshwa dhambi hapa duniani!, lakini tukifa na dhambi zetu bila kutakaswa tumekwisha!

Vile vile hakuna mwanadamu yeyote mbinguni, au duniani au kuzimu anayeshughulika na habari zetu sisi tulio hai kutuombea au kutusikiliza.. anayetuombea sasahivi na kushughulika na mambo yetu sisi tulio hai ni mmoja tu ambaye ni YESU KRISTO, na hatuombei tukiwa tumeshakufa!.. anatuombea sasahivi angali tukiwa hai kwamba tusamehewe na baba pale tunapoungama dhambi zetu kwa kumaanisha kuacha dhambi!.. Baada ya kifo hakuna maombi yoyote ya upatanisho kwaajili yetu. (1Yohana 2:1).

Na wala hakuna mahali popote katika biblia panapoonyesha mtakatifu yeyote aliyekufa akiwaombea walio hai, wala hakuna sehemu hata moja katika biblia nzima inayoonyesha au kurekodi mtakatifu mmoja aliye hai kamwombea marehemu..

Kwahiyo imani ya watakatifu waliokufa kutuombea haina msingi wa kimaandiko, bali ni uongo wa shetani, ambao una sumu kali, na si wa kuupokea wala kuuamini, bali kujiepusha nao.

Tahadhari: 1Timotheo 4:1  “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;

2  kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe”

Usikose sehemu ya pili….

Group la whatsapp Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

JIWE LILILO HAI.

NINI TOFAUTI KATI YA MATENDO YA SHERIA NA MATENDO YA IMANI?

Je Lutu alikwenda kuwahukumu watu wa Sodoma na Gomora? Kulingana na Mwanzo 19:9?

Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?

MISTARI YA BIBLIA KUHUSU WATOTO.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
EMANUEL KIBONA
EMANUEL KIBONA
1 year ago

Watumishi wa Bwana nabarikiwa sana na mafundisho katika site hii. Lakini pia nina ombi nahitaji vitabu vya rejea katika Lugha ya kiingereza au Kiswahili vyenye mafundisho ya Kiroho

Sekela Edward
Sekela Edward
1 year ago

Amen 🙏,nimejifunza

Emmanuel Kitengule
Emmanuel Kitengule
1 year ago

Amina mwalimu, ujumbe huu umekuja wakati muafaka naamini tutapata kujifunza mengi.