Nini maana yake, mpumbavu kuwa na fedha mikononi mwake ya kununulia hekima, Ikiwa hana moyo wa ufahamu?

Nini maana yake, mpumbavu kuwa na fedha mikononi mwake ya kununulia hekima, Ikiwa hana moyo wa ufahamu?


Mithali 17:16 “Nini maana yake, mpumbavu kuwa na fedha mkononi mwake ya kununulia hekima, Ikiwa hana moyo wa ufahamu?”..

Hili andiko lina maana gani?

Jibu: Awali ni vizuri kufahamu hekima inayozungumziwa hapo ni hekima gani?

Hekima inayozungumziwa hapo si hekima ya kiMungu, kwasababu hekima ya Mungu haipatikani kwa fedha…bali hekima inayozungumziwa hapo ni ile ya kiulimwengu, ambayo hiyo inaweza kupatikana kutoka kwa watu,na kwa njia ya kununuliwa (kwa njia ya kwenda katika shule za wenye hekima)…ambapo mtu atalipa kiasi fulani cha Ada na kisha kufundishwa hiyo hekima.

Mfano wa shule za hekima, ni hizi tulizonazo sasa, ambapo mtu atajiunga na shule fulani na kwenda kupewa Maarifa katika eneo fulani la maisha, ambayo yatamfanya aishi vizuri na kupata mafanikio katika maisha.

Kwahiyo hapo biblia iliposema… “Nini maana yake, mpumbavu kuwa na fedha mkononi mwake ya kununulia hekima, Ikiwa hana moyo wa ufahamu?”

Tafsiri yake kwa lugha nyepesi ni hii………. “ina maana gani mpumbavu kuwa na fedha ya kulipia elimu yake na ikiwa hana Moyo wala Nia ya kuipata hiyo hekima?”

Ni jambo ambalo kweli halina Maana,…kwasababu hata akienda kutafuta kuinunua hiyo hekima hataipata kwasababu moyo wake haupo huko, hivyo ataenda kupoteza fedha tu…

Andiko hili linatufundisha umuhimu wa kufanya kitu kwa moyo (iwe cha kimwili Au cha kiroho)… Kama hujanuia kufanya kitu kwa moyo basi ni heri usikifanye kabisa kwasababu ni sawa na kupoteza muda au fedha.

Maran atha.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Kwanini maombi kwa Marehemu si sahihi kibiblia?

Amdhaminiye mgeni hakosi ataumia;Achukiaye mambo ya dhamana yu salama

TAFUTA HEKIMA, MAARIFA, UFAHAMU NA BUSARA.

Shetani anaishi wapi, Je! Amefungwa au yupo kuzimu?

WALA HAKUSIMAMA MTU PAMOJA NAYE, YUSUFU ALIPOJITAMBULISHA KWA NDUGUZE

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments