Nini maana ya Mithali 9:13 Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu?

Nini maana ya Mithali 9:13 Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu?

SWALI: Naomba kufahamu maana ya hili andiko;

Mithali 9:13 “Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu”.


JIBU: Kupiga kilele kunakozungumziwa hapo ni zaidi ya ile ya ‘kupaza sauti ya juu’ bali hapo anamaanisha pia ‘Kulazimisha jambo lake lionekane, ambalo limeshindikana kwa namna ya kawaida, hivyo anatumia njia nyingine za usumbufu.(Ndio makelele)

Kwamfano, labda amejiona havutii mbele za watu, anachofanya, ni kusambaza picha za uchi-uchi mitandaoni, au kuvaa nguo za ajabu na kukatiza mitaani, ili wanaume wamwone wamtamani wamfuate. Hizo ni kilele za mwanamke mpumbavu.

Na ndio maana ukiendelea kusoma vifungu vinavyofuata vinamlenga mwanamke wa namna hii, tusome..

Mithali 9:13 Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu.  14 Hukaa mlangoni pa nyumba yake, Juu ya kiti mahali pa mjini palipoinuka,  15 Apate kuwaita wapitao njiani, Waendao moja kwa moja katika njia zao.  16 Kila aliye mjinga na aingie humu. Tena amwambia mtu aliyepungukiwa na akili,  17 Maji yaliyoibiwa ni matamu, Na mkate ulioliwa kwa siri hupendeza.  18 Lakini huyo hajui ya kuwa wafu wamo humo; Ya kuwa wageni wake wamo chini kuzimuni

Na ndio huyu huyu anayezungumziwa katika Mithali 7:10-11

Ni mwanamke ambaye akiona, hapendezi anakwenda kujichubua na kwenda kujipamba na kujiwekea makucha marefu na kuvaa viatu vilivyoinuka kama kwato, aonekane kama mdoli barabarani, Ili watu wamwangalie wamsifie, au wamfuate wamwoe au walale naye.

Tofauti na mwanamke mwenye busara, biblia inasema huwa ni MTULIVU, na Mpole, na anazingatia sana kuufunika mwili wake. Hana tabia ya kujikweza zaidi ya alivyoumbwa na Mungu, hana makelele, mwenendo wake umenyooka, huwezi mwona anajianika kwenye mitandao ya kijamii, kila tukio yumo na yeye aonekane mrembo, akipost picha zake za uchi-uchi, huwezi mpata hapo.

1Timotheo 2:9  “Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani; 10  bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu. 11  Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna”

Je! Wewe ni mwanamke mwenye makelele? Au mtulivu. Kumbuka heshima yako na thamani yako ipo katika sitara yako. Ukishindwa kujithamini utaitwa ‘mjinga’, na’ usiyejua kitu’ Kama maandiko yanavyosema hapo.

Jitambue.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA

Afadhali mtu akutwe na dubu aliyenyang’anywa watoto wake.

Nini maana yake, mpumbavu kuwa na fedha mikononi mwake ya kununulia hekima, Ikiwa hana moyo wa ufahamu?

Nini maana ya huu mstari; Mithali 10:22 “Baraka ya Bwana hutajirisha, Wala hachanganyi huzuni nayo”

Nini maana ya Mithali 27:6 “Jeraha utiwazo na rafiki ni amini;

Kwanini Mungu anajifanya kama hajui mambo?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Thank Mwakyami
Thank Mwakyami
11 months ago

JE kusuka nywele au kujipamba ni dhambi