Ufunuo 19:11-13 [11]Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita. [12]Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe. [13]Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.
Ufunuo 19:11-13
[11]Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.
[12]Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.
[13]Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.
Ulishawahi kujiuliza ni kwanini mahali hapo Yesu hajitambulishi kwa jina lake la asili tulilolizoea, bali anajiita Neno la Mungu,?.
Ipo maana kubwa sana nyuma yake ambayo wakristo wengi hatuijui.
Ni muhimu tufahamu kuwa pale Tunapomtaja YESU, tunamlenga Yesu wa pande mbili.
Wakristo wengi tunaishia kumtambua Yesu kama mtu, jinsi alivyokuwa na mamlaka, na uweza, na maajabu, jinsi alivyosulubiwa na kuzikwa na kufufuka na kupaa juu, na sasa hivi anatawala na kumiliki viumbe vyote vya mbinguni na vya duniani ..jambo ambalo ni zuri sana, kwasababu kwa kumtambua hivyo ndivyo tunavyomwamini na kupokea wokovu na kuponywa shida zetu.
Lakini kosa ni pale tunapoishia kumtambia Yesu-mtu tu, hatutaki kumtambua Yesu kama Yesu-Neno.
Utajiuliza huyu YESU-NENO ni yupi?
Ni Yesu katika maneno yake aliyokuwa anayafundisha. Leo hii ukiweza kuyaishi maneno hayo kikamilifu 100%, basi na wewe unabadilika na kuwa Yesu, mwenyewe.
Kiasi kwamba, wakati mwingine hutahitaji Yesu aje kukusaidia, bali wewe mwenyewe utaweza kufanya, kila kitu.
Wakristo wengi tunampenda Yesu tunapomsoma au kumsikia, lakini hatutaki kuwa kama yeye. Kwasababu tunaona ugumu kuyaishi maneno yake.
Tunafanana na mwanafunzi anayetegemea tu kikokoteo (calculator) kupigia mahesabu yake, lakini kichwani asiwe na maarifa yoyote ya kinachofanyika nyuma ya kikokoteo kile
lakini mtu ambaye anajua kanuni ya kikokoteo, huyo huwa anakuwa ni bora zaidi..kwasababu hata pasipo kuwa nacho anaweza tu kupiga mahesabu yake na kupata majibu. Atakihitaji kwa kurahisisha tu kazi zake, lakini pasipo hicho bado anaweza kufanya.
Lakini hiyo itamgharimu aende shule, ajifunze misingi yote ya hisabati..tofauti na yule mwingine ambaye kazi yake ni kubofya tu. “Jibu hilo hapo!”
Ndivyo ilivyo kwa wakristo wanaomtegemea Yesu-mtu tu, na sio Yesu-Neno. Wanamgeuza Bwana Yesu kama calculator wanamwita awasaidie, lakini hawataki kuyaishi maneno yake..
Sio kila wakati tutamwitaji Yesu atusaidie, wakati mwingine anataka sisi wenyewe tufanye, ndivyo alivyowazoeza pia mitume wake ambao hapo mwanzo walizoelea kumtegemea tu yeye ilihali hawazingatii maneno yake
Mathayo 17:17
[17]Yesu akajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, kilichopotoka, nitakaa pamoja nanyi hata lini? Nitachukuliana nanyi hata lini? Mleteni huku kwangu.
Wakati mwingine tunamwita Yesu, atusaidie, na anakaa kimya hafanyi chochote..tunaita usiku kucha hajibu lolote. Ni kwasababu gani? Ni kwasababu hatutaki kuliishi Neno lake.
Kwamfano: mmoja anaweza akawa anafunga na kukesha kumlilia Yesu ampe mali (kwasababu anamjua Yesu-mtu anaweza yote)..lakini huku anaendelea na mambo yake ya kidunia.. Na mwingine akalizingatia lile Neno la Yesu linalosema;
Mathayo 6:32-33
[32]Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. [33]Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
[32]Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.
[33]Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
Huyu wa pili, anaweza asimtaje Yesu wala mali mahali popote, lakini akapokea hitaji lake, kwasababu tu kajua kanuni ya roho.. Lakini yule wa kwanza kupewa/kutokupewa ni juu ya Yesu mwenyewe..sio juu yake.
Hivyo tujifunze kuyaishi maneno ya Yesu, kwamfano tunapoambiwa tusamehe huyo ndio Yesu-Neno., tunapoambiwa tusizini ndiye Yesu Neno.
Na Yesu mwenyewe alitusisitizia kwamba maneno yake yakiwa ndani yetu, basi tukiomba lolote yeye atatupa.
Yohana 15:7
[7]Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
“Yodi” ni nini kama tunavyoisoma katika Mathayo 5:18?
BASI MUNGU ALIMWADHIMISHA MNO.
UNAMCHUKULIA YESU KWAKO KAMA NANI?
Unyenyekevu ni nini?
MAOMBOLEZO YA HADADRIMONI.
HUTATAMBUA LOLOTE, SIKU YA UNYAKUO IKIFIKA.
Mshipi wa dhahabu matitini ni nini?.
Rudi nyumbani
Print this post
Mungu awabariki kwa mafundisho mazuri ya kutujenga zaidi kiimani# amina
Amina mwalimu wa NENO,naendelea kukata kiu ya kuijua KWELI.Mungu na azidi kukuinua.
Amen Bwana azidi kutubariki sote…
Mungu awainue sana watumishi wa Bwana
Amen ubarikiwe na Bwana nawe pia..
Bwana YESU asifiwe watumishi wa Mungu!! Namshukuru Bwana Yesu ambaye kila siku ananifundisha kweli yake ili niufikie ukamilifu(Mathayo:5:48). Bwana YESU awabariki, karama na huduma alizowapa azidi kuziinua, mumtumikie sawasawa na mapenzi yake.
Bwana YESu asifiwe watumishi wabwana, mubarikiwe Sana kwajinsi munavyotujenga kwamasomo,