Nimekuwa kama mwari nyuni wa jangwani,

Nimekuwa kama mwari nyuni wa jangwani,

SWALI: Naomba kufahamu Zaburi 102:6 inamaana gani? Mwandishi anaposema..

Zaburi 102:6

[6]Nimekuwa kama mwari nyuni wa jangwani,

Na kufanana na bundi wa mahameni.


Mwari ni aina ya ndege ambao, wana midomo mirefu, na kifuko kikubwa shingoni ambacho wanatumia kuhifadhia chakula kabla hawajakimeza. Ni ndege ambao wanapendelea sehemu za maji maji ambapo inakuwa ni rahisi wao kupata samaki..(Tazama picha juu)

Lakini mwari anayezungumziwa hapa ni jamii nyingine ya jangwani tofauti na yule wa majini..Kwa kawaida ndege hawa(jamii zote) ni ndege wanaopenda sana kujitenga, huwezi wakuta wanatembea pamoja..na mara nyingine utawakuta wapo katika hali ya kupooza wakitumia masaa mengi hata siku wakiwa wameficha vichwa vyao chini ya mbawa zao. Kwa ufupi ni ndege wa upweke sana.

Ndivyo mwandishi wa zaburi alivyojifananisha na ndege hawa kwa upweke aliokuwa anaupitia

Lakini zaidi anajilinganisha pia na bundi wa mahameni.. Bundi ni ndege ambao wanajitenga pia..wanapendelea sehemu za majangwa au mapango au kwenye majumba yaliyoachwa zamani, au makaburini.

Katika hali hizo za unyonge huwa wanatoa milio ya ajabu ajabu hususani wakati wa usiku.

bundi wa mahameni

Wakati fulani niliwahi kwenda mlimani kusali, mlima huo ulikuwa mbali na makazi ya watu, na ulikuwa na mwamba mkubwa kwa nyuma..lakini kwa juu sikuona ndege yoyote isipokuwa bundi mmoja ambaye kila usiku unamsikia analia tu peke yake kwa kule juu…ni ndege wa upweke sana.

Ndivyo mtunzi wa Zaburi alivyokuwa anajifananisha na ndege hawa, kwa hali aliyokuwa nayo wakati huo.

Anasema tena nimekuwa kama shomoro  Aliye peke yake juu ya nyumba.

shomoro aliye peke yakeShomoro ni hawa ndege wadogo wanaotengeneza viota vyao kwenye pembe au mabati ya nyumba. Ni ndege ambao huwezi kuwakuta wanatembea mmoja mmoja.ikitokea hivyo ni aidha mmojawapo amekufa au mgonjwa.

Hivyo mtunzi wa Zaburi anaaeleza kimifano jinsi apitiavyo taabu kutoka kwa maadui wake, hali yake inavyofanana na hao ndege..jinsi aliavyo mbele za Mungu akimwomba amsikie.

Tusome tokea mistari ya juu kidogo;

Zaburi 102:1-8

1 Ee Bwana, usikie kuomba kwangu, Kilio changu kikufikie.

2 Usinifiche uso wako siku ya shida yangu, Unitegee sikio lako, siku niitapo unijibu upesi.

3 Maana siku zangu zinatoweka kama moshi, Na mifupa yangu inateketea kama kinga.

4 Moyo wangu umepigwa kama majani na kukauka, Naam, ninasahau kula chakula changu.

5 Kwa ajili ya sauti ya kuugua kwangu Mifupa yangu imegandamana na nyama yangu.

6 Nimekuwa kama mwari nyuni wa jangwani, Na kufanana na bundi wa mahameni.

7 Nakesha, tena nimekuwa kama shomoro Aliye peke yake juu ya nyumba.

8 Adui zangu wananilaumu mchana kutwa; Wanaonichukia kana kwamba wana wazimu Huapa kwa kunitaja mimi.

Umeona, lakini katika kuugua kwake kote, Bado, Mungu alikuwa tegemeo lake, na mwisho wa siku, ukiendelea kusoma utaona Mungu anasema..

Zaburi 102:16-21

16 Bwana atakapokuwa ameijenga Sayuni, Atakapoonekana katika utukufu wake,

17 Atakapoyaelekea maombi yake aliye mkiwa, Asiyadharau maombi yao.

18 Kizazi kitakachokuja kitaandikiwa hayo, Na watu watakaoumbwa watamsifu Bwana.

19 Maana ametazama toka patakatifu pake pa juu, Toka mbinguni Bwana ameiangalia nchi,

20 Ili akusikie kuugua kwake aliyefungwa, Na kuwafungua walioandikiwa kufa.

21 Watu walitangaze jina la Bwana katika Sayuni, Na sifa zake katika Yerusalemu,

Hii ni kuonesha kuwa maombi na dua za wacha Mungu si bure..Bwana anasikia na atawatoa katika taabu zao endapo hawataacha kumlilia.

Ikiwa unasumbuliwa na magonjwa au hali ambazo wewe mwenyewe umeshindwa kuziondoa..Fahamu kuwa ukimtumaini Bwana katika hali hiyo hiyo ya kuwa mwari na bundi atakuponya..kabisa kabisa, au kukupa haja yako.

Maombolezo 3:31-33

31 Kwa kuwa Bwana hatamtupa mtu Hata milele.

32 Maana ajapomhuzunisha atamrehemu, Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake.

33 Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu. Wala kuwahuzunisha.

Bwana akubariki.Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Lumbwi ni nini katika biblia?

Ayala, Paa na Kulungu ni wanyama gani?

Wibari ni nani?(Mithali 30:26)

Hawa ndege katika Walawi 11:13-19 ndio ndege gani kwasasa?

“Shinikizo” ni nini kibiblia, Na maana yake rohoni ni ipi?

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

Kisiwa cha Patmo kipo nchi gani?

Bahari mbalimbali zilizoorodheshwa kwenye biblia.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
2 years ago

Ubarikiwe mtumishi wa Mungu.