Title January 2019

NJAA IPO?, USIACHE KULA ASALI.

NJAA inaficha uchungu wa kitu, mtu mwenye njaa hata akipewa mboga iliyochungu kiasi gani, bado ataiona ni tamu tu, kwasababu NJAA ipo ndani yake, lakini kwake yeye aliyeshiba, hata chakula kiungwe kwa viungo vingi kiasi gani bado ataona tu kuna kasoro nyingi ndani yake..Ni kwasababu njaa haipo ndani yake.

Unaweza ukajiuliza ni kwanini Neno la Mungu linafananishwa na ASALI? Sababu ni hizi kwanza Asali ni kitu kitamu kuliko vyakula vyote na matunda yote, pili asali ni chakula kisichoharibika kinadumu milele, ni kitu kisichoisha ubora wake kwa mamilioni na mamilioni ya miaka ipo vile vile tofauti na kitu chochote kile kinachoweza kulika, Bwana anasema:

“Mwanangu, ule asali, kwa maana ni njema, Na sega la asali lililo tamu ulionjapo. 14 Basi utaijua hekima kuwa tamu kwa nafsi yako; Ikiwa umekwisha kuiona; Ndipo itakapofuata thawabu; Wala tumaini lako halitabatilika.” (Mithali 24: 13)”.

Lakini japo asali ni tamu kuliko vitu vyote kamwe hatuwezi kuuona utamu wake pale nafsi zetu zikiwa zimejikinai, tukijiona kuwa tunajua, tumefika, hakuna mtu anayeweza kutuongezea kitu cha ziada katika ukristo wetu ni dini zetu tu, tukijiona kuwa sisi ni bora kuliko wengine,

tunawadharau wengine wote, hatutaki kuwasikiliza wala kuwahudumia?, tunasema wale sio wa dhehebu letu, hivyo hatuwasikilizi hawana chochote cha kutuongezea, n.k. ..

Hapo hata kama tutalifahamu Neno la Mungu kwa wingi kiasi gani, hata kama tutakuwa na mafunuo mengi kiasi gani, hata kama tutahubiri mikutano mingi kiasi gani, hata kama tutawaombea wagonjwa wakapona kiasi gani..ULE UTAMU WA NENO LA MUNGU HATUTAUHISI KAMWE NDANI YETU.

Na ndio hapo mtu wa namna hiyo anaishia kuwa wa kidini tu, kama wale mafarisayo na masadukayo, walivyokuwa kipindi kile cha Yesu. Walimwona Bwana kama mtu asiyekuwa na dini, wala elimu, walimwona Bwana kama mtu mwenye pepo, walimwona Bwana kama mwana wa Seremala maskini tu asiyejua kitu, , hivyo pale alipokuja na Neno la Uzima kutoka kwa Mungu, walimdharau japo waliufahamu kuwa anachosema ni ukweli lakini kwa kuwa waliridhika tu na dini zao na mapokeo yao, walikuwa wameshiba nafsini mwao, wakaupinga wokovu…..kwani hekima inasema:

“Nafsi iliyoshiba hukinai sega la asali; Bali nafsi yenye njaa huona kila kitu kichungu kuwa kitamu.” (Mithali27:7).

Embu leo hii, turuhusu nafsi zetu ziwe na NJAA kwa ajili HAKI na KWELI ya Neno la Mungu Ili endapo maagizo yanayoonekana kuwa ni magumu yatokayo katika Neno la Mungu yatakapokuja mbele yetu tuyaone kuwa ni matamu hata kama yataonekana kuwa ni machungu kwa watu wengine, walioshiba. Pale biblia inapotuagiza mara baada ya kuamini kwetu tukabatizwe kwa kuzamishwa katika maji tele,na katika jina la YESU basi sisi tuwe wepesi wa kutii,maadamu nafsi zetu zina njaa ya haki, hata kama tutaona kisima, au mto au bahari vipo mbali nasi basi tufanye hivyo tu kwasababu Roho zetu zina njaa..Tufanye kama yule Mkushi aliyehitaji kubatizwa akiwa njiani, katika safari yake.

Matendo 8: 35 “Filipo akafunua kinywa chake, naye, akianza kwa andiko lilo hilo, akamhubiri habari njema za Yesu.

36 Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji; yule towashi akasema, Tazama, maji haya; ni nini kinachonizuia nisibatizwe?

37 Filipo akasema, Ukiamini kwa moyo wako wote, inawezekana. Akajibu, akanena, Naamini ya kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu.]

38 Akaamuru lile gari lisimame; wakatelemka wote wawili majini, Filipo na yule towashi; naye akambatiza”.

Tusifanane na hao walioshiba, wameshakinai sega la asali ambao pamoja na elimu zao kubwa za dini wakilijua hilo wamelipuuzia kama jambo lisilo na umuhimu sana.

(Luka 6:21 Heri ninyi mlio na njaa sasa, kwa sababu mtashiba.)

Pale biblia inapotuonya tuvae mavazi ya kujisitiri, na tusivae mavazi yaipasayo jinsia tofauti (kumb 22:5). Basi tuone kuwa hicho ni chakula kitamu kwa kutii haraka sana, kwa kwenda kutupa vimini, na suruali, na kaptura ambazo ni za jinsia tofauti na za kwetu [wanawake]. Sisi tusifanane na hao walioshiba wanaosema Mungu haangalii mavazi bali roho, tukiwaacha wale waliojikinai wanaosema tunaishi chini ya neema na wala sio sheria..Sisi tuziache tu nafsi zetu ziwe na njaa..ndipo tutakapoliona Neno la Mungu ni tamu kwetu.

Tuwe kama Daudi, anasema “MAUSIA YAKO NI MATAMU SANA KWANGU, KUPITA ASALI KINYWANI MWANGU Zaburi 119:103.”

Pale biblia inapotuonya tusiabudu sanamu wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni wala chini duniani, basi moja kwa moja tusijione kuwa dini zetu ni bora kuliko Neno la Mungu, tusione kuwa viongozi wetu wa dini ni bora kuliko Neno la Mungu, tusione kuwa dhehebu letu ni zaidi ya Neno la Mungu na kupuuzia, na kuzidi kuabudu sanamu za wafu na kuzifanyia ibada na kusali rozari za kipagani vitu ambavyo Neno limekataza. Sisi tutii tu hata kama dini zetu zinatukemea. Kwasababu tunataka kwenda mbinguni.

Mathayo 5:6 “Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa.”

Tule asali sana maadamu tuna njaa, lakini ole wetu endapo tumeshiba, kwani ni jambo gani litakalotuburudisha lenye utamu zaidi ya asali?.

Dumu katika Neno la Mungu.

Ubarikiwe DAIMA wewe umtafutaye BWANA.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

UBATILI.

WANA WA MAJOKA.

NGUVU YA HEKIMA NA AKILI

MADHARA YA KUTAFUTA ISHARA


Rudi Nyumbani

Print this post

UNAMFAHAMU MUNGU WA KWELI?

Mwanzo Bwana alipowatoa wana wa Israeli katika nchi ya Misri, hakuwakuta ni wakamilifu kwa asilimia zote kama anavyotaka yeye, kwasababu kule Misri walipokuwepo hakukuwa na utaratibu wowote wa kumwabudu Mungu wa kweli, na wala wana wa Israeli walikuwa hawamjui kwa kina Mungu wa Ibrahimu, walikuwa wanayo kama historia vichwani mwao kuwa kipindi Fulani nyuma Mungu alimtokea Baba yao Ibrahimu na kumpa maneno mengi ya Ahadi, walisikia tu kipindi Fulani Mungu, aliipiga dunia kwa njaa lakini alimfunulia Yusufu aliyekuwa mwisraeli kama wao juu ya majanga hayo  yatakayokuja..hawakumjua sana kwa undani, Mungu wao ni Mungu wa namna gani…Walimjua tu ni Mungu hodari na atakayekuja kuwaokoa katika matatizo yao basi.

Na kwa jinsi walivyokuwa wanaendelea kukaa katika nchi ya Misri, pasipo kumsikia kwa vizazi vingi,  kidogo kidogo walianza kumdhania Mungu wa Yakobo ni  kama miungu ya kimisri,  walidhani kwamba Mungu wa Yakobo baba yao anaweza akatengenezewa mfano wa kinyago Fulani kama wa-Misri wanavyoifanyia miungu yao. Waliona kwasababu wa-Misri wanatolea dhabihu sanamu zao huku wanaendelea na roho zao mbaya, na bado wanapata mvua nakufanikiwa wakajua na Mungu wa Yakobo yuko hivyo hivyo, wanaweza wakamtolea dhabihu, na sadaka lakini maisha yao yakaendelea kuwa vile vile, wakaendelea kuwa na kiburi chao, matusi yao, malalamiko yao, uuaji wao, n.k.

Hivyo kwasababu waliishi na Wa-Misri kwa muda mrefu, kwa zaidi ya miaka 400, ule utamaduni au ule mfumo wa kuabudu walioutumia wa-Misri, uliwaingia na wao pia kudhani kuwa Mungu wa Israeli naye anaabudiwa kama inavyoabudiwa miungu ya kimisri..

Hata katika maisha ni kawaida kuona mazingira Fulani yakiwaathiri watu Fulani na kudhani watu wote wako kama wao. Utakuta  kwamfano familia Fulani ina utaratifu wa kukaa pamoja, na kula pamoja mezani..lakini mmoja wa familia hiyo anatoka na kwenda kutembelea familia nyingine na kutazamia kuikuta familia ile ipo kama ya kwao, badala yake anakuta kila mtu yupo kivyake, baba na mama hawaongei, kila mtu na ratiba zake..lazima itamshangaza kidogo kwasababu amekuta kitu asichokitegemea..

Ndivyo ilivyokuwa kwa Wana wa Israeli, Bwana Mungu wakati anakuja kuwatoa ilikuwa ni shida sana wao kumwelewa na ndio maana tunaona Bwana Mungu aliwapitisha kwanza jangwani kabla ya kuwaingiza nchi ya Ahadi ili awafundishe yeye ni nani, na anataka nini kutoka kwao.

Utaona baada tu ya kutolewa nchi ya Misri, pamoja na kufanyiwa miujiza yote ile, wakaanza kunung’unika na kulalamika, ni kwasababu gani walikuwa wanafanya vile? Ni kwasababu walikuwa hawamjui bado Mungu wa Israeli kuwa hapendi watu wanaonungu’unika, wao walidhani Mungu wa Israeli ni kama miungu ya kimisri ambayo ukiinung’unikia tu haiwezi kufanya lolote, walidhani ni kama ile miungu ya kimisri ambayo ukiilalamikia na kuitukana haikufanyi chochote.

Na ukiendelea mbele zaidi utaona wana wa Israeli wanaanza kufikiria kutengeneza ndama ya kusubu ili iwarudishe Misri, ni kwanini walifanya vile? ni kwasababu walidhani Mungu wa Israeli ni kama miungu ya kimisri, kwamba inafika mahali inashindwa kufanya jambo Fulani, na hivyo kuitafutia njia mbadala.

Na mambo mengine mengi, waliyoyafanya wana wa Israeli yaliyomkasirisha Mungu yalitokana na kutomjua Mungu wa YAKOBO ni nani? Yalitokana na kumdhania Mungu wa Baba yao Ibrahimu ni mfano wa mmojawapo wa miungu ya Misri, isipokuwa yeye ana nguvu kidogo kipita yao.

Kwasababu hiyo basi iliwachukua muda mrefu sana kumjua Mungu wa Israeli ni nani..Mpaka Bwana alipoanza kuwapa sheria ndio kidogo kidogo ndipo Alipoanza kuwaambia yeye ni MUNGU  MMOJA, na hakuna mwingine zaidi yake wala wa kufananishwa na yeye, hivyo wasiwe na miungu mingine ya kando ila yeye peke yake. ALIPOANZA KUWAAMBIA YEYE NI MUNGU MTAKATIFU NA HIVYO ANAWATAKA NA WAO WAWE WATAKATIFU KAMA YEYE ALIVYO..

Walawi 11: 45 “Kwa kuwa mimi ni Bwana niliyewaleta kutoka nchi ya Misri, ili kwamba niwe Mungu wenu; BASI MTAKUWA WATAKATIFU, KWA KUWA MIMI NI MTAKATIFU”. 

Ndipo walipoanza kumwelewa Mungu kuwa sio kama miungu ya Misri waliyoizoea kwamba unaweza ukaitumikia na bado ukaendelea kuwa mwizi, unaweza ukaitolea dhabihu na bado ukaendelea kuwa mnung’unikaji, unaweza ukaitumikia na bado ukaendelea kuwa muuaji au mwizi unaweza ukaiabudu na  kuiimbia na bado ukaendelea kuilalamikia, unaweza ukaifuata na bado ukaendelea kuwa mzinzi, au mlaji rushwa, au mtu mwenye chuki, kwamba unaweza ukawa na miungu mingine midogo midogo mingi ya pembeni ya kukusaidia pale Mungu mkubwa anapokwama,   n.k ndipo walipojua kuwa Mungu wa Israeli sio kama walivyokuwa wanamdhania kama miungu ya Misri waliyoizoea Ndipo walipomwelewa vizuri Mungu wa Israeli ni Mungu mtakatifu sana  na hana msaidizi na yupo mmoja,Iliwachukua miaka zaidi ya 40 kumwelewa vizuri Mungu wa Israeli..

Na baada akili zao kubadilishwa kumjua Mungu wa kweli ni Mungu wa namna gani, ndipo wakaweza kutembea na Mungu.

Kaka/Dada unayesoma haya..swali ni lile lile   “Je! Unamjua Mungu wa kweli??” Kumbuka unaposema umetoka kwenye dhambi ni sawa na Bwana kakutoa nchi ya Misri ambayo ulikuwa ni mtumwa wa dhambi? Lakini je! Baada ya kutoka huko umemfahamu Mungu unayemtumikia?? Au unamchukulia Mungu, kama ile miungu uliyokuwa unaiabudu kabla ya kumpokea yeye??…

Biblia inasema katika agano jipya pia..

1 PERTO 1: 13 “kwa hiyo vifungeni viuno vya nia zenu, na kuwa na kiasi; mkiitumainia kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake yesu kristo.

14 kama watoto wa kutii msijifananishe NA TAMAA ZENU ZA KWANZA ZA UJINGA WENU;

15 bali kama yeye ALIYEWAITA ALIVYO MTAKATIFU, NINYI NANYI IWENI WATAKATIFU KATIKA MWENENDO WENU WOTE;

16 kwa maana imeandikwa, MTAKUWA WATAKATIFU KWA KUWA MIMI NI MTAKATIFU.

17 na ikiwa mnamwita baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni”.

Huwezi ukasema umetolewa katika utumwa wa dhambi na bado unasujudia sanamu, huwezi ukasema umetolewa katika utumwa wa dhambi na bado ukawa mwasherati, au mlevi, au mtukanaji…Huwezi ukasema umeokolewa kutoka katika utumwa wa dhambi na bado unavaa nguo zinazoonyesha maungo yako, unavaa nguzo zinazo kubana, unavalia vimini, suruali na kupaka wanja..Hizo zote ni tamaduni za miungu ya ki-Misri na huwezi kumtumikia Mungu wa kweli kwa tamaduni za ki-Misri.

Ndugu yangu kama unataka kwenda na Bwana, mtii anayokuambia leo, Geuka upate ufahamu, usidanganyike kwamba Mungu anaangalia roho haangalii mwili, usidanganyike kwamba wanaopaka lipstick,na wanja na wanaovaa hereni, na wigi wataingia mbinguni..Usidanganyike kuwa wanaofanya masturbation, na wanaotazama pornography, na wanaoishi na wanawake/wanaume ambao hawajaoana kuwa wataingia mbinguni, usidanganyike kuwa ukiwa vuguvugu, nusu Mungu nusu ulimwengu, utaingia mbinguni.. Bwana anasema mwenyewe kuwa ATAKUTAPIKA!!  Kwasababu yeye ni mtakatifu na hivyo tutakuwa watakatifu kama yeye alivyo..

Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, NA HUO UTAKATIFU, AMBAO HAPANA MTU ATAKAYEMWONA BWANA ASIPOKUWA NAO;”

Ni maombi yangu kuwa utamjua Mungu wa kweli ni nani, kama hujamjua na utachukua uamuzi thabiti wa kumfuata yeye kwa viwango anavyotaka yeye vya UTAKATIFU. Na kama hujabatizwa nakushauri ufanye hivyo mapema, kwasababu ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi, na kwa Jina la Yesu  ni wa muhimu sana, katika kuikamilisha safari yako ya wokovu.

Bwana akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Tafadhali “Share” ujumbe huu kwa wengine na Bwana atakubariki.


Mada Nyinginezo:

TAWI LIZAALO HULISAFISHA ILI LIZIDI KUZAA.

NGUVU YA MUNGU YA UUMBAJI

IKO NJIA IONEKANAYO KUWA SAWA MACHONI PA MTU.

MNGOJEE BWANA


Rudi Nyumbani

Print this post

MAMBO YATAKAYOTOKEA ISRAELI SIKU ZA HIVI KARIBUNI.

Ishara kubwa Bwana Yesu aliyowapa wanafunzi wake ambayo kwa hiyo waliambiwa watakapoiona basi wajue kuwa “muda wa mavuno umekaribia” ni ishara ya MTINI. tukisoma

Mathayo 24:32 inasema “Basi KWA MTINI JIFUNZENI mfano; tawi lake likiisha kuchipuka na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno u karibu;

33 nanyi kadhalika, myaonapo hayo yote, tambueni ya kuwa yu karibu, milangoni.

Na tunajua kuwa “mtini” alioumaanisha hapo si mwingine zaidi zaidi ya TAIFA LA ISRAELI (Yeremia 24), Ikiwa na maana kuwa tutakapoona taifa la Israeli linaanza kuchipua na kuchanua tena, basi majira ya mwisho wa dunia yamekaribia sana. Kumbuka Mungu katika mpango wake wa wokovu alianza na Israeli na katika kutimiliza atatimiliza na taifa hilo hilo, kwasababu makao ya MFALME YESU atakapokuja kwa mara ya pili kuutawala huu ulimwengu mzima katika nchi ya wenye haki, hayatakuwa katika mojawapo ya nchi hizi za mataifa tulizopo sisi na zitakazokuwepo huko hapana, bali makao yake yake makuu yatakuwa pale Israeli nchi takatifu. Alishuka hapo mara ya kwanza, atashuka hapo hapo mara ya pili. Hivyo ni lazima kwanza pale patakaswe kisha mataifa mengine yafuate kabla ya yeye kuteremka ulimwenguni.

Hivyo Mungu akishamaliza kupatakasa Israeli, ndipo atakapoitumia Israeli kuitakasa dunia nzima kwa fimbo yake. Na ndio maana Mungu alisema hivi juu ya Israeli. 

Yeremia 51:20 “ WEWE U RUNGU LANGU NA SILAHA ZANGU ZA VITA; kwa wewe nitawavunja-vunja mataifa; na kwa wewe nitaharibu falme;

21 na kwa wewe nitamvunja-vunja farasi, na yeye ampandaye; na kwa wewe nitalivunja-vunja gari la vita, na yeye achukuliwaye ndani yake;

22 na kwa wewe nitawavunja-vunja mwanamume na mwanamke; na kwa wewe nitawavunja-vunja mzee na mtoto; na kwa wewe nitawavunja-vunja kijana mwanamume na kijana mwanamke;

23 na kwa wewe nitamvunja-vunja mchungaji na kundi lake; na kwa wewe nitamvunja-vunja mkulima na jozi yake ya ng’ombe; na kwa wewe nitawavunja-vunja maliwali na maakida.”

Unaona?. Sasa kulingana na unabii wa kibiblia katika hatua tuliyopo sasa tunatazamia kushuhudia VITA KUU MBILI KUBWA zitakazopiganwa pale Israeli kabla ya mambo yote kuisha. Vita ya kwanza ni ile inayozungumziwa katika Ezekieli 38-39, ambayo ndio itakayofuata muda mfupi ujao Na vita ya pili ni ile ya HAR-MAGEDONI (Ufunuo 16:16), hiyo itakayokuja kuhitimisha utawala mbovu wa huu ulimwengu, inajulikana kama vita ya Mungu mwenyezi.

VITA YA ULIYOZUNGUMZIWA KATIKA EZEKIELI 38-39.

Siku zote Mungu kabla hajafanya jambo kubwa litakaloleta madhara huwa anatanguliza kwanza madogo madogo ili kuwakumbusha watu wachukue tahadhara kwani makubwa zaidi ya hayo yanakuja mbeleni. Na ndio maana Bwana Yesu alisema, kutakuwa na vita, na tetesi za vita, kutakuwa na njaa na matetemeko ya ardhi, hayo yote ni MWANZO WA UTUNGU, Unaona Hapo utungu wenyewe bado haujafika. Ukifika inamaanisha maafa yatakuwa makubwa zaidi kuliko haya tuyaonayo. Na ukitazama kwa ukaribu haya matetemeko ya ardhi tunayoyaona ulimwenguni na kusema ni makubwa, yanayoangamiza maelfu haya yote si kitu, Yapo matetemeko hasa yatakayokuja siku ile ya mwisho hii dunia itakapoikiswa pale visiwa na milima vitakapohama kwa nguvu ya tetemeko la ardhi ambalo Mungu atalileta mwenyewe duniani kote, na mvua ya mawe makubwa sana ambayo haijawahi kunyesha tangu ulimwengu kuumbwa, hapo ndipo wanadamu wote waliosalia wakati huo watalia na kuomba milima iwaangukie wajisitiri mbali na hasira ya Mungu. Ni mambo ya kutisha sana.

Ufunuo 6.12 “Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu,

13 na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi.

14 Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake.

15 Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima,

16 wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo.

17 Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?”

Vivyo hivyo na kwenye suala la magonjwa na vita. Magonjwa yaliyopo leo yanatabika na homa zake ni za wastani, kadhalika na yanapatikana maeneo Fulani Fulani tu sio kila mahali haya yote ni mwanzo wa utungu,lakini yale yatakayoletwa na Mungu katika siku ile ya ghadhabu ya hasira yake, biblia inasema kutakuwa na jipu baya na bovu juu ya watu wote ulimwenguni walioipokea ile chapa ya mnyama. Jaribu kufikiri ukimwi na kansa,au ebola ni magonjwa yanayoogopeka, Lakini biblia hayajayaona hayo, mpaka kulizungumzia hili jipu bovu tu lenyewe…ni baya kiasi gani mpaka wanadamu watamtukana Mungu kwa maumivu ya ugonjwa huo. Sio kutamani kuwepo huko ndugu.

Sasa tukirudi kwenye suala la vita. Leo Tunaweza kushuhudia vita ya kwanza na vya pili vya dunia vilivyoua watu zaidi ya watu milioni 80, huo ni mwanzo tu wa utungu, na lakini ipo vita itakayopiganwa siku za mwisho ambayo ndio ile ya mwisho inayojulikana kama HAR-MAGEDONI. Watu watakaouawa ni idadi kubwa mito ya damu itabubujika Israeli kwa wingi wa watu watakaouawa.

Sasa tuitazame Israeli kama jinsi ilivyofananishwa na mtini kuchipuka kwake, ambako kulikuwa ni mwaka 1948.

Tunaona kuwa tangu huo wakati Israeli ilipokuwa Taifa huru tena, mvutano mkubwa ulianza kujitokeza mashariki ya kati na duniani kote kwa ujumla. Nchi za kiharabu zikiigombani Israeli na mataifa mengine yakizisapoti.Mpaka kupeleka Israeli kuwa na maadui wengi pande zake zote. Watu wasifahamu kuwa jambo hilo linatoka kwa Bwana mwenyewe ili kuonyesha kuwa moja ya hizi siku mataifa yote yatahukumiwa na rungu la Bwana Israeli.

Hiyo Iliendelea hivyo hivyo mpaka kupelekea mwaka 1967 mataifa yote ya urabuni yakiongozwa na Syria kujikusanya kwa ajili ya kuipoteza Israeli katika ramani ya dunia. Lakini jambo hilo kama tunavyosoma katika historia, Israeli ilizipiga silaha zao za vita na vita kuisha ndani ya siku 6 tu. Kupeleka mpaka Israeli kuteka sehemu ya kubwa ya taifa lake ambalo hapo kabla lilikuwa haliyamiliki pamoja na nchi za kando kando.

Sasa hayo nayo ni mwanzo wa utungu ili kutupa sisi picha ya mambo yatakayokuja kutoka siku za hivi karibuni. Hii ilikuwa ni mataifa ya uarabuni lakini siku zinakuja mataifa yote ulimwenguni yataungana kwenda kupigana na Israeli hiyo ndiyo vita ya Har-magedoni.

Hivyo tukisoma kitabu cha Ezekieli 28-39, tunaona vita nyingine hapa ukiwa na muda wako mwenyewe unaweza kusoma sura zote mbili upate kuiona habari nzima ni vita ambayo itapiganwa tena kipindi hichi karibu na unyakuo kutokea. Embu Tusome mistari michache tu ya mwanzo.

Ezekieli 38

EZEKIELI: MLANGO 38

1 Neno la Bwana likanijia, kusema,

2 Mwanadamu, kaza uso wako, umwelekee Gogu, wa nchi ya Magogu, mkuu wa Roshi, Mesheki, na Tubali, ukatabiri juu yake,

3 useme, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni juu yako, Ewe Gogu, mkuu wa Roshi, na Mesheki, na Tubali;

4 nami nitakugeuza na kutia kulabu katika mataya yako, nami nitakutoa, pamoja na jeshi lako lote, farasi na hao wapandao farasi, wote wamevaa silaha za namna zote, jeshi kubwa sana, wenye ngao na kigao, wote wakishika upanga;

5 Uajemi, na Kushi, na Putu, pamoja nao; wote wana ngao na chapeo;

6 Gomeri, na vikosi vyake vyote; nyumba ya Togarma, pande za mwisho za kaskazini, na vikosi vyake vyote; naam, watu wengi pamoja nawe.

7 Ujiweke tayari, naam, jiweke tayari, wewe na majeshi yako yote waliokukusanyikia, nawe uwe jemadari wao.

8 NA BAADA YA SIKU NYINGI UTAJILIWA; KATIKA MIAKA YA MWISHO, UTAINGIA NCHI ILIYORUDISHIWA HALI YAKE YA KWANZA, BAADA YA KUPIGWA KWA UPANGA, ILIYOKUSANYWA TOKA KABILA NYINGI ZA WATU, juu ya milima ya Israeli, iliyokuwa ukiwa wa daima; lakini imetolewa katika kabila za watu, nao watakaa salama salimini wote pia.

9 Nawe utapaa juu, utakuja kama tufani, utakuwa kama wingu kuifunika nchi, wewe, na vikosi vyako vyote, na kabila nyingi za watu pamoja nawe.

10 BWANA MUNGU ASEMA HIVI; ITAKUWA KATIKA SIKU HIYO, MAWAZO YATAINGIA MOYONI MWAKO, NAWE UTAKUSUDIA KUSUDI BAYA;

11 nawe utasema, Nitapanda juu niiendee nchi yenye vijiji visivyo na maboma; nitawaendea watu wanaostarehe, wanaokaa salama, wote wakikaa pasipo kuta, ambao hawana makomeo wala malango;

12 ili kuteka mateka, na kuwinda mawindo; uugeuze mkono wako juu ya mahali palipoharibika, ambapo sasa panakaliwa na watu, na juu ya watu waliokusanyika toka mataifa, waliopata ng’ombe na mali, wakaao katikati ya dunia.

13 Sheba, na Dedani, na wafanya biashara wa Tarshishi, pamoja na wana-simba wake wote, watakuambia, Je! Umekuja kuteka mateka? Umekusanya jeshi lako, ili kuwinda mawindo? Kuchukua fedha na dhahabu, kuchukua ng’ombe na mali, kuteka mateka mengi sana?

14 Basi, mwanadamu, tabiri, umwambie Gogu, Bwana MUNGU asema hivi; Katika siku ile watu wangu, Israeli, watakapokaa salama, hutapata habari?

15 Nawe utakuja kutoka mahali pako, kutoka pande za mwisho za kaskazini, wewe, na watu wa kabila nyingi pamoja nawe, wote wamepanda farasi, kusanyiko kubwa, na jeshi kuu;

16 NAWE UTAPANDA JUU UWAJILIE WATU WANGU, ISRAELI, KAMA WINGU KUIFUNIKA NCHI; ITAKUWA KATIKA SIKU ZA MWISHO, NITAKULETA UPIGANE NA NCHI YANGU, ILI MATAIFA WANIJUE, nitakapotakaswa kwako, Ewe Gogu, mbele ya macho yao.

17 Bwana MUNGU asema hivi; Je! Wewe ndiwe niliyemnena zamani za kale, kwa vinywa vya watumishi wangu, manabii wa Israeli, waliotabiri siku zile kwa muda wa miaka mingi, ya kwamba nitakuleta upigane nao?

18 Itakuwa katika siku hiyo, Gogu atakapokuja kupigana na nchi ya Israeli, asema Bwana MUNGU, ghadhabu yangu itapanda katika mianzi ya pua yangu.

19 Kwa maana katika wivu wangu, na katika moto wa ghadhabu yangu, nimenena, Hakika katika siku ile kutakuwako tetemeko kubwa katika nchi ya Israeli;

20 hata samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama wa kondeni, na vitu vyote vitambaavyo juu ya nchi, na wanadamu wote walio juu ya uso wa nchi, watatetemeka mbele ya uso wangu; nayo milima itatupwa chini, na magenge yataanguka, na kila ukuta utaanguka chini.

21 Nami nitaita upanga, uje juu yake katika milima yangu yote, asema Bwana MUNGU; nao upanga wa kila mtu utakuwa juu ya ndugu yake.

22 Nami nitamhukumu kwa tauni, na kwa damu; nami nitanyesha mvua ifurikayo, na mvua ya mawe makubwa sana, na moto na kiberiti juu yake, na vikosi vyake, na watu wa kabila nyingi walio pamoja naye.

23 Nami nitajitukuza, na kujitakasa, na kujidhihirisha, mbele ya macho ya mataifa mengi; nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana”.

Sasa Nchi ya Magogu, biblia inayoitaja hapo ni eneo linalojulikana kama URUSI kwasasa. Hivyo nchi hii leo tunaoina ni nchi yenye nguvu sana kiasi kwamba inalitishia hata taifa la Marekani kwa nguvu zake na ukuu wake. Lakini biblia inasema siku moja mawazo yataliingia hili taifa ili kwenda kuishambulia Israeli. Na kibaya zaidi halitashuka peke yake, hapana bali litashuka na majeshi ya mataifa mengine mengi kama tunavyoyasoma hapo juu. Na mengi ya hayo yatakuwa na haya mataifa ya kiharabu, ambayo hayo kimsingi ni maadui wa Israeli tangu zamani, pamoja na nchi nyingi zilizokando kando ya Urusi.

Wote watapanga vita kuiendea ile nchi ndogo sana Israeli. Kama tunavyoona hata sasa Taifa linaloongoza kuwa na maadui wengi duniani ni taifa la Israeli, hivyo Urusi kwa kujipendekeza na kujionyesha kuwa yeye anayo nguvu na kwamba anaweza kuwasaidia watu waliwashindwa ISRAELI. Yeye naye siku hiyo atapanga vita na mabomu yake ya Atomiki ili kwenda kulisambaratisha taifa lile. Hawajui kuwa hapo ndipo Mungu alipokusudia uwe mwisho wa mataifa hayo yote chini ya jua. Siku hiyo Urusi itapotezwa kwenye ramani ya dunia, kwasababu Bwana atakuwa upande wa Israeli. Na wa-Rusi siku hiyo watasoma maandiko haya ya Ezekieli na kutambua kuwa unabii huo ulikuwa unawahusu wao.

Kumbuka vita hiyo japo itauwa watu wengi sana kiasi kwamba biblia inasema mizoga yao itakuwa inazikwa kwa muda wa miezi 7 ikikusanywa tu, na silaha zao zitakuwa zikitumika kama kuni kwa muda wa miaka 7, lakini huo utakuwa ni mwanzo tu wa utungu. Vita yenyewe kuu bado. Vita ya Har-magedoni ambayo itahusisha mataifa yote ulimwenguni.

Tutakuja kuizungumzia vizuri vita hii [Har-Magedoni] katika makala nyingine. Lakini tufahamu kuwa vita inayozungumziwa katika Ezekieli 38-39 ipo mbioni kutokea, kama tunavyoona sasahivi mvutano ulivyo mkubwa mashariki ya kati na ishara kuwa vita vinajiandaa kupiganwa muda wowote. Hivyo ndivyo Mungu anavyozidi kuitasa Israeli kidogo kidogo, Na ndivyo pia wanavyojiandaa kumpokea Masiya wao.

Swali tujiulize wakati sasahivi neema inarudi Israeli, mimi na wewe mpaka mambo hayo yatakapotokea tutakuwa wapi? Kumbuka ndugu tuliambiwa tukiyaona hayo yanaanza kutokea basi tunyanyue vichwa vyetu, kwa kuwa ukombozi wetu umekaribia. Ikiwa na maana UNYAKUO wetu upo karibu.

Kristo yupo mlangoni ndugu. Unasubiri nini usiufanye leo wito wako na uteule wako imara?. Walioishi kipindi chote cha nyuma kuanzia miaka ya 1900 kurudi nyuma mpaka kipindi cha kanisa la kwanza hawakukishuhudia kitu hichi sisi tunachokishuhudia leo yaani taifa huru la Israeli. Na biblia ilishasema kizazi hiki hakitapita, sasa unasubiri nini usiushindanie wokovu katika muda huu mfupi uliobaki?.

Ungependa mambo hayo yakukute kwa ghafla, Bwana amesema dunia hii itaangamizwa kwasababu ya maovu yake. Na wenye haki watapata kwa Mungu waepushwe nayo.. je! Na wewe ungependa uwe miongoni mwa watakaoharibiwa katika ile siku ya Bwana? Kama sivyo mgeukie Kristo, ambaye yeye ndio safina pekee iliyothibitishwa na Mbingu kwa wokovu wa mwanadamu.

Bwana akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Print this post