JIKANE NAFSI MTEULE WA MUNGU.

JIKANE NAFSI MTEULE WA MUNGU.

Kitabu cha Jeografia, hawajaandikiwa watu ambao sio wanafunzi, kadhalika kitabu cha Fizikia na Baolojia…Vitabu vyote hivi wameandikiwa watu husika…yaani wanafunzi wa masomo hayo..Mtu mwingine yeyote akisoma hataelewa au hakitamsaidia sana…Na maudhui ya vitabu hivyo havijaandikwa kwa lengo la kusomwa tu, bali kujifunza…lengo la mwanafunzi kujifunza mambo yaliyoandikwa ndani ya kitabu kile ni ili kumpa maarifa ambayo yatamsaidia katika maisha yake na pia yatakayomsaidia kufaulu mitihani…asipokielewa kitabu hicho na kukisoma tu kama gazeti, anaweza kweli kukisoma chote ndani ya siku moja lakini utakapokuja mtihani atafeli…Kwasababu waandishi wa vitabu hivyo, lengo lao sio mwanafunzi asome ndani ya siku moja, bali ajifunze kidogo kidogo mambo yaliyopo kule na ayafanyie mazoezi na alinganishe mambo kutoka vitabu vingine, na ndio maana mpaka atakapohitimu inaweza kumchukua hata miaka 4 na zaidi.

Kadhalika na Biblia, NI KITABU CHA MAISHA. Kitabu hichi, hakimuhusu kila mtu, bali kinawahusu wanafunzi tu! Wengine watakisoma kama gazeti na hakitawasaidia chochote, lakini wanafunzi wanakisoma kama ni sehemu ya Maisha yao, future yao ipo hapo, Ndio ufunguo wa Maisha yao…Ndio maana biblia iliposema “Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako.(Mithali 4:13)”…Mstari huo haukulenga Elimu ya darasani…hapana! Bali ulilenga Elimu ya Mungu (Elimu ya ufalme wa mbinguni) Mathayo 13:52..maana huo ndio uzima wetu…wengi wanaupeleka mstari huu moja kwa moja kwenye Elimu ya duniani, lakini hiyo si kweli.. “hiyo ni maana ya pili ya mstari huo lakini maana ya kwanza Kabisa Sulemani aliyomaanisha hapo ni ELIMU YA UFALME WA MBINGUNI”.

Na unapozungumzia Elimu huachi kuzungumzia, Shule, huwezi kuacha kuzungumzia,Waalimu, huwezi kuacha kuzungumzia wanafunzi, wala huwezi kuacha kuzungumzia Mtaala (ambao upo ndani ya vitabu husika).

Na kadhalika Maisha mapya katika Kristo yetu ndio shule yetu, Roho Mtakatifu ndio Mwalimu Mkuu wetu, Biblia ndio Mtaala wetu(Kitabu husika)..na wote waliomwamini Yesu Kristo kwa kuzaliwa mara ya pili, kwa kudhamiria kabisa kumfuata kwa kujikana nafsi zao ndio wanafunzi wake…Utasema hilo linapatikana wapi kwenye maandiko…soma

Luka 14:25 “Makutano mengi walipokuwa wakifuatana naye, aligeuka, akawaambia,

26 Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.

27 Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu”.

Sasa mwanafunzi kabla hajajiunga na shule yoyote ya kidunia, anakubali kuachana na wazazi wake, na ndugu zake, na hata marafiki zake, anakwenda kujiunga na shule ya Bweni…Huko shuleni hataishia tu kukaa mbali na wazazi wake kwa kipindi kirefu, bali atalazimika kuvikataa pia vile vitu vizuri alivyokuwa anavipenda akiwa nyumbani kama Tv, simu, uhuru, nk..anakwenda mahali ambapo hapana uhuru aliokuwa anautaka, mahali ambapo pengine atakutana na changamoto za chakula kibovu, na malazi mabaya.…Na katika Ukristo ndio hivyo hivyo unapoamua kumfuata Kristo ni sawa na umejiunga na shule mpya, Maisha yako ya kale unayakataa, pamoja na mapenzi ya wazazi wako…kwasababu unakwenda kutafuta Uzima wako wa baadaye (future). Na Ukristo sio mteremko kama wengi wanavyofikiri, ukiamua kumfuata Kristo kupungukiwa wakati mwingine kunakuwepo na pia kuna kupitia dhiki nyingi..tofauti na wale watu wanaowahidia watu uongo kuwa watakafanikiwa siku zote.

Vivyo hivyo unapoingia shuleni, unakutana na sheria za shule na moja ya sheria hizo ni mavazi, na mwiko kutoka nje ya uzio wa shule.…shuleni huwezi kujivalia utakavyo, kunakuwa na UNIFORM maalumu…na wote mnafanana…na huwezi kuingia na kujitokea kama unavyotaka, ukitoka bila sababu maalumu ndio umejifukuzisha hivyo…..kadhalika Unapozaliwa mara ya pili, mavazi yako na mwonekano wako ni lazima ubadilike, ulikuwa unavaa vimini ni sharti uache, ulikuwa unavaa suruali wewe mwanamke ni sharti uache, ulikuwa unanyoa kiduku na kuvaa nguzo zinazobana na milegezo wewe mwanamume sharti uache, ulikuwa unapenda kusikiliza miziki ya kidunia, na movie zisizo na maana na fashion za ulimwengu, na kuzurura huku na huko vyote hivyo unaacha!…Na pia Ukristo sio kuingia na kutoka…Ukiingia umeingia! Na ukitoka umetoka…Mwalimu Mkuu huwa hawi mkali kwa Watoto wa mitaani, huwa anakuwa mkali kwa Watoto walioko shuleni kwake, vivyo hivyo Roho Mtakatifu anavyowafundisha watu waliozaliwa mara ya pili ni tofauti na ambao wapo nje.

Baada ya kukubaliana navyo hivyo vigezo, ndipo unapewa MTAALA MAALUMU pamoja na Waalimu wa kukufundisha, na wewe mwenyewe unaongeza bidii zako binafsi kujisomea…Ukisubiri tu kila siku kufundishwa darasani na wewe mwenyewe hutaki kutafuta, utafeli mtihani wa Mwisho, na Katika Ukristo ni hivyo hivyo, umezaliwa mara ya pili, wewe kila siku unapenda tu kufundishwa Biblia, muda wa kujisomea mwenyewe huna, utafeli majaribu na hutaendelea mbele kila siku utakuwa unarudi darasa lile lile, miaka yote wakati wenzako wanaenda mbele..

Na jambo lingine baada ya kujiunga na shule za kidunia ni kwamba utakaa shuleni katika hayo mazingira ya kuteseka kwa muda mrefu kidogo inaweza kuchukua hata miaka kadhaa, lakini siku utakapokuja kufanya mtihani wa mwisho na kufaulu utapokea cheti, ambacho hicho kitaonyesha tofauti yako wewe uliyekwenda shule na yule ambaye hajakwenda…kulivumilia viboko vya shule na kula chakula kibovu na wakati mwingine kulala vitanda vyenye kunguni sio bure!…siku utakapohitimu na kupata cheti heshima yako ndio itakapoonekana kuwa hukuwa mjinga kujikana nafsi yako.

Kadhalika Roho Mtakatifu akishakupitisha katika madarasa yake na kuyahitimu vizuri faida zake utakuja kuziona hapa hapa duniani pamoja na katika ulimwengu ujao…lakini sana utakuja kuziona katika ulimwengu ujao kwasababu vitu vya hapa duniani havidumu, vinapita lakini vya huko mbinguni ni vya milele…Siku zile wateule walioshinda watang’aa kama jua mbele za malaika wa mbinguni…

Mathayo 19:27 “Ndipo Petro akajibu, akamwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata; tutapata nini basi?.

28 Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli.

29 Na kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu wa kiume au wa kike, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia, na kuurithi uzima wa milele”.

Umeona Umuhimu wa kuitafuta Elimu ya ufalme wa mbinguni sasa?..Elimu ya dunia hii inafunua elimu ya ufalme wa mbinguni, Kristo anapokuambia leo utubu na kuacha dhambi, na ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina lake na uache ulimwengu na mambo yake yote, na kisha umfuate sio kwamba anataka atutese, hapana ni kwasababu anataka atusajili kwenye shule yake ambayo baadaye itatupa cheti kilicho bora! Zaidi kuliko vyeti vyote.. Na heshima! Zaidi kuliko heshima zote….na kumbuka hakuna shule yoyote isiyokuwa na sheria ndio maana anakuambia ewe mwanamke jikane nafsi!! acha mavazi yako ya kikahaba, acha mawigi, acha kupaka wanja, acha mavipodozi baki katika hali yako ya asili…kama unapenda kujipamba subiri tukifika mbingu za mbingu utajipamba utakavyo kama kutakuwepo na kujipamba….lakini kwasasa upo shule!..fanya kile Mwalimu Mkuu anachokuagiza ukifanye kwa faida yako…

Ulipokuwa katika shule za kidunia ulipoambiwa uvae sketi za marinda ulitii na usisuke nywele ulitii bila shuruti lakini unapoitafuta elimu ya Roho Mtakatifu hutaki kutiii…nataka nikuambie ukweli bado hujaanza madarasa ya Roho Mtakatifu, bado upo nyumbani wala mtu asikudanganye kuwa upo sawa na Mungu bado haupo sawa, usidanganywe pia Mungu haangalii mavazi anaangalia Roho, ni kweli kabisa anaangalia roho lakini roho inamahusiano makubwa na mwili ndio maana ipo ndani ya mwili, kama vile elimu ya kidunia ilivyo na uvaaji wa wanafunzi wake..Elimu ni ufunguo wa Maisha, yaangalie Maisha yako ya baadaye yatakavyokuwa usijiangalie leo…dhambi za kitambo zisije kukuponza ukaja kujuta milele huko baadaye..Fanyika mwanafunzi wa Kristo leo.

Bwana akubariki sana.

Pia kwa Maombezi, Ushauri, au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba

+225693036618/+225789001312

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

NJIA YA MSALABA

BWANA ALIMAANISHA NINI KUSEMA JIKANE MWENYEWE?

JE! NI KWELI UMEMFUATA YESU?

MJUE SANA YESU KRISTO.


Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Mohamed kassim
Mohamed kassim
3 years ago

🙌🙌🙌 Amin
Ongeza sauti mtu wa MUNGU
Ubarikiwe sana