JE! KUBET NI DHAMBI?

by Admin | 27 July 2019 08:46 pm07

Ili kujua kama ku-BET ni dhambi au la! Ni vizuri kwanza kufahamu mapenzi ya Mungu ni yapi?…Huwezi kujua kipi kisichompendeza Mungu kama hujui kipi kinachompendeza…Sasa Mungu alivyotuumba watu wake na viumbe vyake vyote hata Wanyama, alituwekea kitu kinachoitwa dhamira ndani yetu…Hii dhamira kazi yake ni kutulinda sisi tusiende kinyume na mapenzi ya Mungu tunapoishi…Na ipo kwa viumbe vyote (wanadamu na wanyama)..Ndani ya hii dhamira kumefungiwa sheria za Mungu. Kwahiyo pasipo hata Mungu mwenyewe kuzungumza na mtu juu ya jambo Fulani tayari ile dhamira iliyopo ndani yake ina uwezo wa kukamata na kuhisi jambo ambalo sio sawa.

Kwamfano utaona, Simba anauwezo wa kula swala na kumrarua kikatili, lakini simba huyo huyo hamli mtoto wake…ni kwanini? Ni kwasababu dhamira iliyopo ndani yake inamshuhudia kuwa jambo hilo sio sawa…simba hajapewa sheria yoyote na Mungu, lakini ndani ya moyo wake kumefungiwa sheria, kwa kupitia dhamira aliyo nayo. Kadhalika huwezi kuona mbwa au mnyama yoyote analala na mnyama wa jinsia moja naye…

Ni kwanini? ni kwasababu ya dhamira iliyopo ndani yao..inayowashuhudia kuwa jambo Fulani sio sahihi, sio kwamba hawana hisia! Wanazo hisia lakini hawawezi wakavuka hiyo mipaka.

Na wanadamu ni hivyo hivyo, kuna kitu kinaitwa dhamira ambayo hiyo imebeba sheria za Mungu ndani yake, kiasi kwamba mtu anaweza asizijue kabisa amri za Mungu, lakini bado akazitimiza vile vile..

Haihitaji biblia kujua kuwa uuaji ni mbaya, au kuwatesa Watoto wako ni vibaya…Hiyo sheria tayari mtu anazaliwa nayo moyoni mwake…ndo maana hata wanyama pamoja na ukatili wao wote hawayafanyi hayo, hawasomi biblia lakini wanazitimiza sheria za Mungu….Haihitaji biblia kujua kuwa utoaji mimba ni vibaya, au kumdhulumu mtu ni vibaya, hiyo tayari mtu angejua hata kama hajawahi kusikia habari za Mungu. Haihitaji sheria kufahamu kumuoa dada yako/kaka yako wa damu ni makosa, hiyo tayari ipo ndani yako, hata hizo hisia zenyewe hazipo licha tu ya dhamira kukushuhudia.

Sheria ilipokuja, kazi yake ni kuitoa hiyo hiyo sheria kutoka katika roho na kuileta katika maandishi..Na hiyo ni kutokana na ugumu wa mioyo yetu, unajua hata watoto wanapotumwa dukani, na wanaonekana ni wazito kidogo kuelewa au wanasahausahu sahau, basi wazazi wanaamua kuwaandikia kikaratasi kidogo cha maelekezo ili wasisahau. Na sheria ilikuja kwa namna hiyo hiyo. Ililetwa kutufanya tuyakumbuke yale tuliyokuwa tumeyasahau katika roho zetu na dhamira zetu..

Sasa Watu waliokuwa wanaishi wakati wa Nuhu, walikuwa hawana sheria yoyote, Maana sheria ililetwa na Musa miaka mingi sana baada ya gharika?..Sasa unaweza kuuliza kama kulikuwa hakuna sheria, wale watu walihukumiwa kwanini?…Walihukumiwa kwa dhamira iliyokuwepo ndani yao…walikuwa wanafanya mambo ambayo ndani ya dhamira zao walikuwa wanajua kabisa sio sawa…lakini waliendelea kuyafanya! Hivyo ikawa dhambi kwao,(Warumi 1:17-30) Na Mungu akawaangamiza wote kwa gharika. Kwahiyo sheria hii ambayo tayari ipo ndani ya dhamira zetu ndio inayojulikana kama INJILI YA MILELE (Ufunuo 14:6). Kwa maelezo marefu juu ya injili hii ya milele  Bofya hapa >> INJILI YA MILELE

Sasa mpaka sasahivi hii INJILI YA MILELE ipo, Kuna vitu ambavyo havijazungumziwa hata kwenye Biblia takatifu lakini mtu akiona tu! Anajua hiyo sio sawa machoni pa Mungu..Mfano wa vitu hivyo ni Uvutaji wa sigara, utoaji mimba, mtu anayetoa mimba anajua kabisa ndani ya moyo wake anaua na anafanya jambo lisilo sahihi…ingawa ukitafuta mahali popote kwenye biblia palipoandikwa utoaji mimba ni dhambi huwezi kupata…Lakini mtu anayefanya hivyo anajua kabisa na anauhakika ndani ya moyo wake anamkosea Mungu, na ndivyo ilivyo…au mtu anayetumia madawa ya kulevya…anajua kabisa jambo afanyalo sio jema…

Jambo lingine ni mtu anayefanya masturbation, ukienda kumwuliza mtu anayefanya masturbation unajua ni kosa kufanya hivyo, wala hatakubishia Zaidi ataogopa na atakuuliza namna ya kuacha!…lakini ukienda kwenye maandiko ukitafuta mahali popote pamezungumzia suala la masturbation kuwa ni dhambi hutapaona!…lakini kwanini yule mtu ndani ya moyo wake anauhakika kuwa anachokifanya sio sahihi?..

Ni kwasababu ya dhamira iliyopo ndani yake! (Sheria ambayo Mungu alishaiweka ndani ya moyo wake) inayomshuhudia jambo sahihi na lisilo sahihi…Au leo hii ukimfuata mtu anayeangalia pornography, atakwambia kabisa mimi nafanya makosa, wala hatakubishia wala kukuuliza ni wapi pameandikwa hivyo kwenye biblia?…wala hatataka kujua, yeye anachojua kuwa anafanya dhambi, jambo lisilompendeza Mungu, hilo tu!…Au mtu anayecheza kamari, anajua kabisa jambo afanyalo sio sawa, na anajua kabisa huo mchezo ni wa kishetani, anajua kabisa ni mchezo wa dhuluma ambao wakati mwingine unaweza kuhatarisha, uchumi wake, na usalama wake, anajua kabisa Mungu hayupo katikati ya huo mchezo, Na dhambi nyingine nyingi zinazofanywa na wanadamu ndio hivyo hivyo, hazihitaji biblia kuzihakiki, tayari zimeshajihakiki zenyewe ndani yetu.

Sasa tukirudi kwenye suala la KU-BET na lenyewe ni hivyo hivyo, Kubet ni kamari, isipokuwa iliyohalalishwa na nchi.

Hakuna mahali popote katika biblia imezungumzia habari za kubet…Lakini ipo INJILI YA MILELE ndani ya kila mtu…Inayokushuhudia kuwa hichi kitu sio sahihi.

Kama ukichunguza kwa makini mtu anayebet kabla hajaanza kufanya hicho kitu kina kitu ndani yake kinamshtua kwanza, anaanza kukosa amani na anakuwa na mashaka mashaka na huo mchezo, ndio hapo ataanza kujiuliza, hivi kweli huu mchezo ni wa KiMungu? Hayo ndio maswali ya kwanza mtu anayoanza kujiuliza kabla ya kuingia…Na anapoikataa hiyo sauti na kuingia huko, baadaye haisikii tena ndio anaanza kuona ni mchezo wa kawaida tu usio na madhara yoyote, lakini siku za kwanza kwanza atakwenda mpaka kuuliza watu kama ni sawa kuucheza au la?..Ukishaona hali kama hiyo jua kabisa kuna kitu cha hatari unakiendea..

Na ni kwanini unaanza kusikia hivyo viashiria kabla hata hujajiingiza kwenye huo mchezo? Ni kwasababu mchezo huo ni wa kishetani, na unamwingiza mtu kwenye roho moja kwa moja..Mashirika yote ya betting ulimwenguni yanafanya kazi ya shetani kama ulikuwa hulijui hilo ndugu yangu.., yanafanya mambo mengi ya siri ambayo shetani hawezi kuruhusu watu wayajue, ndio mashirika yanayokusanya utajiri mkubwa kwa shetani..Na hayo ndiyo yatakuja kushirikiana na mpinga-Kristo katika kumpa nguvu.

Mashirika hayo mengi yanamilikiwa na vikundi vya kichawi vikubwa duniani kama freemason, brotherhood, yana kivuli cha kulipa kodi, lakini yana agenda nyingine za siri nyuma ya pazia, yanapokea maagizo kutoka kwa lusifa mwenyewe kufadhili mikutano ya hadhara ya ushoga ili kuipalilia roho ya ushoga duniani,..kufadhili haki za mashoga na wasagaji, kufadhili agenda za utoaji mimba n.k kwa nje yanaonekana ni mazuri, lakini wamiliki wa mashirika hayo ni mawakala wa shetani mwenyewe waliowekwa na shetani kwa kazi hiyo.

Na baadhi ya mashirika hayo pia yanafadhili ugaidi kwa siri, ili kuihimiza dunia ilete ustaarabu mpya wa ulimwengu, na pia yanatumia fedha nyingi kuyanyanyua mashirika mengine madogo madogo yanayofanya kazi kama hizo za kuiharibu dunia.…Shetani anafanya kazi kubwa kuachilia mapepo ambayo yatahakikisha watu wengi wanakwenda kubet na kuhakikisha wanakosa, ili aongeze fedha nyingi katika ufalme wake kwaajili ya kumwekea njia mpinga-Kristo. Biblia inasema shetani anampa aliyewake jinsi apendavyo, yeye ndiye anayechagua ni nani apate na ni nani akose, na kumbuka anawapa walio wake, hawezi kumpa ambaye anajua hamsujudii wala haongezi chochote katika ufalme wake..

Mtu anayekwenda kubet kuna pepo Fulani linamvaa, ambalo litamfanya Kesho arudi tena kufanya hivyo hata kama atakosa mara ngapi lakini hatachoka kubet…Mwisho wa siku unakuwa fukara, na bado taabu yako umempa shetani aitumie.

Kwahiyo Biblia inatuambia tutoke huko? (2 Wakoritho 6:15-18)..tutatokaje! Ni kwa kutubu na kudhamiria kuacha hivyo vitu…Biblia inasema shina moja la mabaya yote ni kupenda fedha, unapotamani kupata fedha za ghafla, tambua ni kama mtu aliyewasha WIFI kwenye simu yake, mtu aliyekaribu na yeye anaweza kuupata mtandao wake, na kadhalika mtu anayependa au kutaka kupata fedha za ghafla, anakuwa ni rahisi sana kuonekana kwenye mitandao ya mashetani na kuvaliwa na maroho…

1 Timotheo 6:9 “Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu.

10 Maana SHINA MOJA LA MABAYA YA KILA NAMNA NI KUPENDA FEDHA; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.

11 Bali wewe, mtu wa Mungu, uyakimbie mambo hayo; ukafuate haki, utauwa, imani, upendo, saburi, upole”.

Hivyo tunaonywa tusipende fedha za ghafla! huo ni mtego mkubwa sana shetani anaoutumia…Tembea huko barabarani kwenye nguzo za umeme uone vibao vya waganga,..wote kitu cha kwanza watakwambia…njoo upate utajiri!..Mpango wa Mungu ni kuchuma kidogo kidogo…Sio kwamba hapendi tupate kingi hapana! Ndio mpango wake tuwe na vingi Lakini tukusanye kidogo kidogo…….Tukusanye shilingi mia, mia, kuanzia asubuhi hadi jioni na kupata milioni kumi hiyo ni sawa!….lakini kupata milioni kumi ndani ya dakika moja ogopa sana hizo njia!..Vingi vya hivyo ni mitego ya shetani, Na ndio betting inachofanya.

Mithali 13: 11 “Mali iliyopatikana kwa haraka itapunguka; Bali yeye achumaye kidogo kidogo atazidishiwa”.

Bwana akubariki sana.

Pia kwa Maombezi, Ushauri, au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba

+225693036618/ +225789001312

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

INJILI YA MILELE.

JE! UKRISTO UNAMPA MTU DHAMANA YA KUWA TAJIRI?

KUCHEZA KARATA NI SAHIHI KWA MTU ALIYE MKRITO?

NJIA YA ‘UTAJIRI MKUU’ KWA KIJANA.


Rudi Nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/07/27/je-kubet-ni-dhambi/