UMEITIMIZA HAKI YOTE?

UMEITIMIZA HAKI YOTE?

Ipo haki na ipo Haki yote.

Mathayo 3:13 “Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe.

14 Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu?

15 Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akamkubali”

Kuna maneno mawili hapo ambayo ningependa tuyatazame. 1) ITUPASAVYO 2) HAKI YOTE.

1) ITUPASAVYO.

Hapo Bwana hajasema, Ndivyo inipasavyo kuitimiza haki yote” bali amesema “Ndivyo Itupasavyo”.. Maana yake hiyo haki haipaswi kutimizwa yeye peke yake tu, bali watu wote, na hao watu ni wale wote walio upande wake, ndio maana Bwana Yesu akasema Imet ujeupasa, maana yake yeye pamoja na wote watakaomfuata..ni lazima waitimize haki yote.

Sasa hiyo haki yote ni ipi?

2) HAKI YOTE.

Kama tulivyosema ipo haki na ipo haki Yote.
Unapomwamini Bwana Yesu, hapo umeitimiza haki, unaposhiriki meza ya Bwana hapo umeitimiza haki, unapohubiri hapo umetimiza haki, unapoishi maisha ya utakatifu hapo umetimiza haki, lakini bado si haki yote. Haki yote inakamilika na wewe kukamilisha UBATIZO WA MAJI.

Bwana Yesu alikuwa mkamilifu, alikuwa tayari mtakatifu kiasi kwamba asingekuwa na haja ya kubatizwa. Lakini aliona asipobatizwa atakuwa hajaitimiza haki yote.

Sasa kama Bwana Yesu alibatizwa ili kuitimiza haki yote, mimi na wewe leo ni nani tusibatizwe! Au tuone ubatizo hauna maana?.

Kumbuka tena Bwana anasema Imetupasa!!..maana yake sio yeye peke yake tu! Bali yeye na sisi, wote imetupasa kuitimiza Haki ya Mungu.

Katika siku hizi za mwisho shetani anawazuia watu kwa nguvu wasiitimize haki yote, anataka waitimize Nusu haki tu!..kwasababu anajua mtu akiitimiza haki yote atakuwa amempoteza, na yeye bado anataka watu wengi zaidi, wapotee naye kwenye ziwa la moto.

Na kumbuka sio kila ubatizo ni ubatizo sahihi, shetani kashafika mpaka hatua ya kuupindisha ubatizo.

Ubatizo sahihi ni ule wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo (Matendo 2:38), na si kwa kunyunyiziwa, Bwana Yesu hakwenda kwa Yohana mbatizaji na kunyunyiziwa, maandiko yanasema “alipanda kutoka majini” na si “kutoka kwenye kikombe chenye maji”.

Marko 1:9 “Ikawa siku zile, Yesu alikuja kutoka Nazareti ya Galilaya, akabatizwa na Yohana katika Yordani.

10 Mara alipopanda kutoka majini, akaona mbingu zinapasuka, na Roho, kama hua, akishuka juu yake”

Yohana alibatiza katika maji mengi sehemu zote (Yohana 3:23).

Sasa swali ni hili: Kama nisipobatizwa kabisa au nikibatizwa kwa ubatizo usio sahihi, baada ya kuujua ukweli sitaokolewa!

Jibu rahisi ni NDIO! Hutakolewa siku ya mwisho, kwasababu umeijua Njia ya Haki na hujaifuata, watakaopata neema ni wale ambao hawakuwahi kusikia kabisa, ambao pengine wangesikia ukweli unaoupata au tunaoupata, wangebadilika haraka sana.

Swali ni je! UMEITIMIZA HAKI YOTE?.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?

WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.

YANAYOENDELEA SASA KATIKA MADHABAHU YA MUNGU ROHONI.

KWANINI UBATIZO NI WA MUHIMU.

JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
1 year ago

NDUGU KATIKA KRISTO YESU
haki ambayo inatajwa kwenye kitabu cha mathay 3:13 sio haki ambayo mkristo wa sasa anayopaswa kuilipa kwasababu iyo haki imekwisha kulipwa pale msalabani na YESU KRISTO kwakua iyo haki tulinyanganywa na shetani pale edeni soma Warumi 5:12-21
KWANINI TUNABATIZWA
(1) kwamaana iyo kama mkristo anabatizwa kwakuwa iloniagizo lililotolewa na kristo kweny waefeso 4:5
(2)yapo mengi yanayo sababisha mkristo abatizwe lakini lengo kubwa ni mkristo kuapokea au kuipata NEEMA
naweza nikaonyesha mambo mengi lakin yote nitarudi apo apo kwenye NEEMA (KUFANYIKA MWANA ,KUSAMEHEWA ZAMBI,KUFUFUKA PAMOJA NA KRISTO/KUZALIWA UPYA,KUHESABIWA HAKI .NK)
kama utakuwa na swali au maoni
0693475464 barnaba