Shukrani ni nini kibiblia?

by Admin | 30 March 2024 08:46 am03

Shukrani au kushukuru ni ile hali ya kurudisha hisia chanya kwa mema au mabaya yaliyokufikia.

Kwa tafsiri ya kidunia, shukrani inatolewa pale mtu anapopokea mambo mema.. Kwamfano mtu atarudisha shukrani aidha ya maneno au matendo pale anapozawadiwa kitu, au anapofanyiwa jambo Fulani jema.

Lakini kibiblia, Shukrani inatolewa si tu baada ya kupokea mambo mazuri/mema bali pia kwa mambo yote (hata kwa yale mabaya).. Ndivyo biblia inavyotufundisha..

1Wathesalonike 5:18 “SHUKURUNI KWA KILA JAMBO; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu”.

Soma pia Ayubu 2:10,

Maana yake ni lazima kumshukuru Mungu hata katika yale mambo ambayo tunaona hayajaenda kama tulivyotarajia, (Ikiwemo misiba, na hata wakati mwingine hasara)… kwasababu tunajua yote ni mapenzi ya Mungu kwetu maadamu tupo ndani ya KRISTO.

Lakini Zaidi sana ni vizuri kumshukuru MUNGU kwa mema anayokufanyia.

Moyo wa shukrani ni moyo unaompendeza MUNGU, na moyo usio na shukrani huondoa/hukausha mema yote na Baraka zote kwetu kutoka kwa Mungu.

Wengi wanajifungia milango yao ya Baraka baada ya kukaa kimya pale wanapotendewa jambo fulani na MUNGU, lakini wengine wanaendeleza milango ya Barakabaada ya kumshukuru Mungu kwa mambo waliyotendewa.

Shukrani ni jambo linalompendeza Mungu na linaloendeleza Baraka juu yetu.

Luka 17:12  “Na alipoingia katika kijiji kimoja, alikutana na watu kumi wenye ukoma; wakasimama mbali,

13  wakapaza sauti wakisema, Ee Yesu, Bwana mkubwa, uturehemu!

14  Alipowaona aliwaambia, Enendeni, mkajionyeshe kwa makuhani. Ikawa walipokuwa wakienda walitakasika.

15  Na mmoja wao alipoona kwamba amepona, alirudi, huku akimtukuza Mungu kwa sauti kuu;

16  akaanguka kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria.

17  Yesu akajibu, akanena, Hawakutakaswa wote kumi? Wale kenda wa wapi?

18  Je! Hawakuonekana waliorudi kumpa Mungu utukufu ila mgeni huyu?

19  Akamwambia, Inuka, enenda zako, imani yako imekuokoa”.

JE SHUKRANI IPI NI BORA?..

Shukrani iliyo bora ni ile inayoambatana na Sadaka.. Hii ni shukrani bora na yenye nguvu sana zaidi ya ile ya midomo mitupu tu!.

Ifuatayo ni baadhi ya mistari ya shukrani katika biblia.

1Nyakati 16:8 “Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake; Wajulisheni watu matendo yake”.

Ezra 13:11 “Wakaimbiana, wakimhimidi Bwana, na kumshukuru, wakasema, Kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake kwa Israeli ni za milele. Kisha watu wote wakapaza sauti zao, na kupiga kelele, walipomhimidi Bwana, kwa sababu msingi wa nyumba ya Bwana umekwisha kuwekwa”.

Zaburi 7:17 “Nitamshukuru Bwana kwa kadiri ya haki yake; Nitaliimbia jina la Bwana aliye juu”

Mistari mingine ni pamoja na Zaburi 9:1, Zaburi 28:7, Zaburi 33:2, Zaburi 92:1, Zaburi 136:1-3 na Isaya 12:4.

NI MAJIRA GANI SAHIHI YA KUMSHUKURU MUNGU.

Majira sahihi ya kumshukuru Mungu ni pale siku inapoanza, na inapoisha.. Inapoamka asubuhi na kuianza siku ni lazima kumshukuru Mungu kwa ulinzi wa usiku kucha na kwa kukupa siku mpya, vile vile unapoimaliza siku ni lazima umshukuru kwa kuimaliza salama na kwa ulinzi.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Mistari ya biblia kuhusu shukrani.

JINSI SHETANI ANAVYOZUIA MAJIBU YA MAOMBI YETU.

TOA HUDUMA ILIYO BORA.

SI KWA MATENDO BALI NEEMA.

AMEFANYIKA BORA KUPITA MALAIKA!

Rudi Nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/03/30/shukrani-ni-nini-kibiblia/