Tafsiri ya Yeremia 29:12 Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza.

by Nuru ya Upendo | 8 August 2024 08:46 am08

Yeremia 29:12 Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza.

13 Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.

14 Nami nitaonekana kwenu, asema Bwana, nami nitawarudisha watu wenu waliofungwa, nami nitawakusanya ninyi, nikiwatoa katika mataifa yote, na katika mahali pote, nilikowafukuza, asema Bwana; nami nitawaleta tena, hata mahali ambapo kutoka hapo naliwafanya mchukuliwe mateka

Huu ni utabiri ambao Mungu aliwaambia Israeli, pindi tu walipochukuliwa utumwani Babeli, akiwaahidia atawarudisha tena kwenye nchi yao baada ya miaka sabini. Na zaidi ya hayo akawapa pia na Neno la ahadi kwamba wakati huo wakimtafuta kwa mioyo yao yote, watamwona, watamwomba atawasikia, na wote watarejeshwa nyumbani ijapokuwa walichukuliwa mbali sana.

Na kweli utabiri huo ulikuja kutumia, kwani mwishoni mwa hiyo miaka sabini, mbiu ilipigwa waisraeli wote warudishwe kwao. Na aliwaonekania sana pindi waliporejea.

Ni neno la ahadi hata kwetu,

Kwamba tukimtafuta yeye kwa mioyo yetu yote, tutamwona. Kumbuka anasema “MIOYO YETU YOTE”. Kosa linatokea pale tunapompenda Mungu kwa sehemu, leo kwake kesho kwa shetani. Ndio Inayopelekea tusimwone Mungu katika ukamilifu wake wote. Mungu anahitaji vyako vyote vielekee kwake, ndipo tumwombe na kumwita ili atuitikie..

Shalom

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine

Nijapokuwa sipo kwa mwili, lakini nipo pamoja nanyi kwa roho,

Nini Maana ya Adamu?

FAHAMU TAFSIRI ZA NDOTO MBALIMBALI.

Rudi Nyumbani

WhatsApp
DOWNLOAD PDF

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/08/08/tafsiri-ya-yeremia-2912-nanyi-mtaniita-mtakwenda-na-kuniomba-nami-nitawasikiliza/