Nini maana ya waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo? (Matendo 11:23)

by Admin | 1 December 2024 08:46 pm12

SWALI:  Mitume walikuwa na maana gani kuwasihi wanafunzi kule Antiokia, waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo? Ni maana ya hiyo kauli?

Matendo 11:22 Habari hizo za watu hao zikafika masikioni mwa kanisa lililokuwako katika Yerusalemu; wakamtuma Barnaba, aende hata Antiokia.

23 Naye, alipokwisha kufika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo.

24 Maana alikuwa mtu mwema amejaa Roho Mtakatifu na imani; watu wengi wakaongezeka upande wa Bwana.

JIBU: Kauli hiyo inamaanisha kwa “kusudi sahihi la moyo” sawasawa na imani waliyoipokea, Kwasababu Mitume walijua madhumuni ya wao kumfuata Yesu yakiwa sio sahihi, kusimama kwao kunaweza kusidumu. Kwasababu walijua wapo wanaomfuata Kristo kwa sababu ya fitna, wengine fedha, wengine watu, wengine vyeo, wengine kuajiriwa n.k.. Na hiyo haipaswi. Kwasababu Mungu huuchunguza kwanza moyo wako kilichokupelekea  kumfuata ni nini?. Ikiwa sio kwa lile kusudi lake sahihi, hauwezi kusimama.

Sifa hizo za Mungu kuchunguza makusudi ya moyo tunazisoma kwenye vifungu hivi;

Waebrania 4:12 Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukataokuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.

Hivyo hata sasa, Mungu anataka tuipokee imani kwa kusudi la kweli la moyo, ili tuweze kudumu, na kuona utendaji kazi wake bora, katika maisha yetu ya rohoni, na pia tuweze kusimama hadi mwisho .

Kusudi sahihi la moyo ni kumfuata Yesu ili akuokoe dhambini, kumtazama Kristo kama dhabihu kamilifu ya Mungu iliyotolewa kwa ajili ya kuondoa dhambi zetu, na sio atupe utajiri, au atuponye magonjwa, au atupe mke/mume.

Kwanini  iwe hivyo?

Kwasababu hayo yasipokuja kwa wakati  utamwacha Kristo, au yakipatikana basi Kristo hawezi kuwa tena na thamani moyoni mwako, kwasababu kusudi lako moyoni lilikuwa utatuliwe tu changamoto yako, si zaidi. Na ndio maana ni rahisi leo kuona watu wengi makanisani, lakini wasiwe wote wameokoka.

Mitume waliliona hili kama ni jambo muhimu sana kufundishwa mwanzoni kabisa mwa imani kwa waongofu wapya. Vivyo hivyo na sisi tuige fundisho hilo pindi tunapowajenga waongofu wapya.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

JE! UKRISTO UNAMPA MTU DHAMANA YA KUWA TAJIRI?

NJIA/BARABARA YA WOKOVU NDANI YA KITABU CHA WARUMI.

Biblia inamaana gani kusema ‘maana Mungu wetu ni moto ulao’ (Waebrania 12:29)

Rudi Nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/12/01/nini-maana-ya-waambatane-na-bwana-kwa-kusudi-la-moyo-matendo-1123/