Jibu: Turejee…
Mhubiri 4:4 “Tena nikafikiri amali zote, na kila kazi ya ustadi, ya kwamba inatoka katika mtu kupingana na mwenzake. Hayo nayo ni ubatili na kujilisha upepo”.
Amali ni “kazi ya tabu/kuchosha”.. Mtu anayefanya kazi yenye kuchosha mwili na akili, kazi yake hiyo inaitwa “Amali”.
Hivyo mstari huo wa Mhubiri 4:4 unaweza kueleka hivi….
Mhubiri 4:4 “Tena nikafikiri KAZI ZOTE ZA TABU, na kila kazi ya ustadi, ya kwamba inatoka katika mtu kupingana na mwenzake. Hayo nayo ni ubatili na kujilisha upepo”.
Maana yake kazi nyingi za kuchosha zinatokana zinahusisha mambo maovu ikiwemo Tamaa, Uchungu, Wivu, uchoyo, hasira na visasi.
(Ingawa pia si zote, yaani si wote wenye kufanya kazi za taabu/kuchosha wapo juu ya misingi hiyo, wapo wengine nia zao ni njema kabisa wana amani na Bwana anawatunza na kuwaonekania.. lakini wengi wao msingi wao ni uovu).
Mhubiri 4:8 “Kuna mtu aliye peke yake, wala hana wa pili wake; naam, hana mwana wala ndugu; hata hivyo amali yake haina mwisho, wala macho yake hayashibi utajiri. Basi asema, Ni kwa ajili ya nani nafanya kazi, na kujinyima nafsi yangu mema? Hayo nayo ni ubatili, naam, ni taabu kubwa”.
Lakini kama mtu atakuwa na Amali na akamcha Bwana ana heri, kwani tabu yake si bure kama maandiko yasemavyo, ila kwa mwenye kumweka Bwana pembeni, amali yake itakuwa bure.
Mistari mingine yenye kutaja Amali ni pamoja na Mhubiri 5:19, na Mhubiri 8:15.
Ikiwa kazi yako ya mikono, inakulemea akili na nguvu na huoni faida yake basi kimbilia kwa Bwana YESU naye atakutia mizigo sawasawa na ile Mathayo 11:28.