Jibu: Turejee.
Warumi 1:11 “Kwa maana ninatamani sana kuwaona, nipate kuwapa KARAMA YA ROHONI, ili mfanywe imara”
Awali ya yote ni vizuri kuzingatia kuwa hasemi “karama za rohoni” kana kwamba ni nyingi…bali anasema “karama ya rohoni” ikiwa na maana ni “moja tu”.
Na hiyo si nyingine zaidi ya ile iliyokuwa ndani ya Paulo (Karama aliyokuwa nayo Paulo).
Sasa anaposema “apate kuwapa karama ya rohoni”…hamaanishi kumpa tu mwingine karama kama aliyokuwa nayo yeye, au awawekee mikono wapokee karama za rohoni kama unabii, au lugha, au imani La! Hakumaanisha hivyo, kwasababu vipawa na karama ni Mungu pekee ndiye atoaye na si mwanadamu.
Lakini maana ya “kuwapa karama ya rohoni”…ni kuwanufaisha wale watu kwa karama iliyokuwemo ndani yake Paulo.
Mtu mwenye karama ya unabii na anapompa mwingine unabii kwa uongozo wa Roho Mtakatifu maana yake “amempa mtu huyo karama ya rohoni”..mtu mwenye karama ya uponyaji anaombea wengine na wakapokea uponyaji, maana yake amewapa wale watu karama ya rohoni na ndicho Mtume Paulo alichokimaanisha pale.
Ili tuelewe vizuri tusome tena maandiko yafuatayo..
Warumi 12:6 “Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, TUTOE unabii kwa kadiri ya imani;
7 ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake”.
Umeona hapo?…anasema ikiwa unabii, ualimu, au karama nyingine yoyote basi TUTOE kwa wengine?.
Kwahiyo Mtume Paulo alikuwa amelenga kuwanufaisha watu kwa ile karama Mungu aliyoiweka ndani yake, na si kuwagawia karama za roho mtakatifu zile zinazotajwa katika 1Wakorintho 12.
Na zaidi sana Paulo alikuwa anashauku sana kufanya hivyo kwa makundi yote ya watu (Wayunani na Wayahudi).
Warumi 1:13 “Lakini, ndugu zangu, sipendi msiwe na habari, ya kuwa mara nyingi nalikusudia kuja kwenu, nikazuiliwa hata sasa, ili nipate kuwa na matunda kwenu ninyi pia kama nilivyo nayo katika Mataifa wengine.
14 Nawiwa na Wayunani na wasio Wayunani, nawiwa na wenye hekima na wasio na hekima”.
Je na wewe unaitoa karama yako kwa wengine??..fahamu kuwa kila mtu aliyempokea KRISTO anayo karama ya rohoni, na ni lazima utumike kuwajenga wengine na kuwavuta kwa KRISTO zaidi.
Bwana akubariki.