Nipo Tayari Kubatizwa.

by Devis | 2 June 2025 08:46 am06

Ubatizo ni agizo la Bwana katika hatua za awali za wokovu. Wapo watu wanaosema Ubatizo hauna maana, ndugu usijaribu kufanya hivyo, unaweza usiwe na maana kwako, lakini unaomaana kwa yule aliyekupa hayo maagizo.

Kwanini tunabatizwa?

Mathayo 28:19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;

Ikiwa yeye hakuwa na dhambi wala kasoro yoyote alibatizwa, kwanini sisi tusibatizwe?

Mathayo 3:13 Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe.

Ubatizo ni ishara ya nje ya kile ulichokiamini, kuwa umekufa kwa habari ya dhambi, kisha ukafufuka katika upya na  Kristo.

Warumi 6:3-4

[3]Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?

[4]Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.

Ni nani anayepaswa kubatizwa.

Ni yule aliyeamini, yaani kuupokea ujumbe wa injili kwa geuko(toba).

Matendo 2:41

Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa;…

Ni wakati gani anapaswa abatizwe?

Haraka sana, tangu siku ile alipoamini. Ubatizo sio mpaka  umekomaa kiroho au kimafundisho, hapana, bali ulipopokea tu wokovu, wakati huo huo unastahili ubatizo.

Matendo ya Mitume 2:38

[38]Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

Ubatizo sahihi ni upi?

Ni ule wa kuzamishwa katika maji tele (Yohana 3:23, Matendo 8:36-38 ),

Na kwa jina la Yesu Kristo.(Ambalo ndio Jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu) [Mathayo 28:19, matendo 8:16, 10:48, 19:5]

Ikiwa Sikubatizwa kwa kuzamishwa katika maji mengi, au nilibatizwa nikiwa mtoto mchanga yanipasa nibatizwe tena?

Ndio, ili kufuata mkondo sahihi wa kimaandiko, huna budi kubatizwa tena.

Msaada wa ubatizo:

Kwakuwa umeokoka, na bado hujapata huduma hiyo basi waweza tafuta Kanisa la kiroho, ambalo linaamini katika ubatizo wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo ili utimize agizo hilo.

Lakini ikiwa utapenda kusaidiwa na sisi. Basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi kwa msaada huo:

+255693036618 / +255789001312

Bwana akubariki.

Mistari ya kusimamia kila ukumbukapo tendo la ubatizo.

Wakolosai 2:12 Mkazikwa pamoja naye katika ubatizo; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu.

Wagalatia 3:27 Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.

Bwana akubariki.

Kwa mafundisho zaidi kuhusu ubatizo

KWANINI UBATIZO NI WA MUHIMU.

MFANO WA MAMBO HAYO NI UBATIZO.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/06/02/nipo-tayari-kubatizwa/