by Devis | 16 July 2025 08:46 pm07
SWALI: Nini maana ya ‘laana ya torati’, ambayo Kristo alikuja kutukomboa kutoka katika hiyo?
Wagalatia 3:13
[13]Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;
JIBU:
Mungu alimpa Musa Torati ambayo ndani yake haikuwa na baraka tu pale Mtu alipoitii, bali pia ilikuwa na laana nyuma yake pale mtu alipoiasi..
Sasa hizo laana ndio ziliitwa “laana ya torati”, yaani adhabu, hukumu na kutengwa na uso wa Mungu.
Ukisoma Kumbukumbu la torati sura ya 27 – 28 inaeleza kwa undani juu ya baraka na laana mtu azipatapo pale anapoitii Au kunapoikataa torati..
Kwamfano
Kumbukumbu la Torati 27:26 inasema;
[26]Na alaaniwe asiyeyaweka imara maneno ya torati hii kwa kuyafanya. Na watu wote waseme, Amina.
Hivyo wanadamu, wote hawakufanikiwa kuzishika amri zile, na sheria Mungu alizowapa, na matokeo yake ikiwa ni laana juu ya kila mtu.
Warumi 3:10-12,23
[10]kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Hakuna mwenye haki hata mmoja. [11]Hakuna afahamuye; Hakuna amtafutaye Mungu.
[12]Wote wamepotoka, wameoza wote pia; Hakuna mtenda mema, la! Hata mmoja…
[23]kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;
Sasa Kristo alipokuja, alifanywa laana kwa ajili yetu..sawasawa na hiyo Wagalatia 3:13, maana yake aliichukua hukumu yetu ya makosa kwa kupigwa na kufa kwake pale msalabani ili sisi tuponywe..
Warumi 8:1
[1]Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.
Ndio maana mtu yeyote ambaye hajamwamini Kristo bado yupo Chini ya hukumu na adhabu, kwasababu atataka kumpendeza Mungu kwa kutegemea tu nguvu zake mwenye, na hatimaye mwisho wa siku atashindwa..kwasababu hakuna mwanadamu aliyewahi kuishika torati yote…
Atasema haibi, hasemi uongolakini wakati huo huo ana mawazo mabaya, yote hayo ni makosa na dhambi…na mshahara wa dhambi sikuzote ni mauti..(Warumi 6:23)
Umeona umuhimu wa Yesu maishani mwetu?
Unasubiri nini usimwamini, akutoe katika laana hiyo, ili uhesabiwe bure kwa neema yake?
Mpokee sasa akuokoe…bofya hapa kwa mwongozo wa sala hiyo…
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/07/16/nini-maana-ya-laana-ya-torati-ambayo-kristo-alikuja-kutukomboa-kutoka-katika-hiyo/
Copyright ©2025 Wingu la Mashahidi unless otherwise noted.