Kwanini mkono wa Musa uingie ukoma?

by Nuru ya Upendo | 14 October 2025 08:46 am10

Swali: Kwanini MUNGU aliufanya mkono wa Musa kuwa na ukoma kama ishara kwa wana wa Israeli? (Kutoka 4:6).

Jibu: Turejee..

Kutoka 4:6 “Bwana akamwambia tena, Sasa tia mkono wako kifuani mwako. Akautia mkono wake kifuani mwake; naye alipoutoa, kumbe! Mkono wake ulikuwa una ukoma, umekuwa mweupe kama theluji.

7 Akasema, Tia mkono wako kifuani mwako tena. Akautia mkono wake kifuani mwake tena, na alipoutoa kifuani mwake, kumbe! Umerudia hali ya mwili wake.

8 Basi itakuwa, wasipokusadiki, wala kuisikiliza sauti ya ishara ya kwanza, wataisikiliza sauti ya ishara ya pili”.

Sababu kuu ya BWANA MUNGU, kuutia mkono wa Musa ukoma na kisha kuuponya ni kutoa ujumbe kwa wana wa Israeli kuwa yeye ni Mungu awaponyaye.. Kwa hivyo wana wa Israeli walipoiona ile ishara walitambua kuwa Mungu wao ni Mungu anayeponya na kuondoa maradhi, misiba, mateso na hata utumwa..

Jambo hilo tunalithibitisha mbele kidogo katika ile sura ya 15 alipowaambia jambo hilo pale alipoyaponya maji yaliyokuwa machungu..

Kutoka 15:22 “Musa akawaongoza Israeli waende mbele kutoka Bahari ya Shamu, nao wakatokea kwa jangwa la Shuri; wakaenda safari ya siku tatu jangwani wasione maji.

23 Walipofika mahali palipoitwa Mara hawakupata kuyanywa yale maji ya Mara, kwa kuwa yalikuwa machungu; kwa ajili ya hayo jina lake likaitwa Mara.

24 Ndipo watu wakamnung’unikia Musa, wakisema, Tunywe nini?

25 Naye akamlilia Bwana; Bwana akamwonyesha mti, naye akautia katika hayo maji, maji yakawa matamu. Basi akawawekea amri na hukumu huko, akawaonja huko;

26 akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya Bwana, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yo yote niliyowatia Wamisri; KWA KUWA MIMI NDIMI BWANA NIKUPONYAYE.

26 kawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya Bwana, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, MIMI SITATIA JUU YAKO MARADHI YO YOTE NILIYOWATIA WAMISRI; KWA KUWA MIMI NDIMI BWANA NIKUPONYAYE”.

Na hata sasa bado MUNGU wetu ana sifa hiyo hiyo, “YEYE NI MUNGU ATUPONYAYE”… Ikiwa tutasikiliza kwa bidii sauti yake na kufanya yale anayotuelekeza.. Magonjwa yote hayatakuwa sehemu yetu, mateso yote hayatakuwa sehemu yetu na kila aina ya mabaya ya ibilisi hayatatutawala.

Je umempokea YESU KRISTO kama Bwana na Mwokozi pekee wa maisha yako?

Kama bado unasubiri nini?.. mwamini leo uokolewe na kuponywa.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

FANYIKA SIPORA WA KRISTO, UNYAKUO UPO KARIBU.

FIMBO YA HARUNI!

MAMBO SITA, AMBAYO MUNGU HUTUMIA KUONDOA UOVU NDANI YA MTU.

Kwanini Mungu alimchagua Musa, na si mtu mwingine?

NABII MUSA.

WhatsApp
DOWNLOAD PDF

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/10/14/kwanini-mkono-wa-musa-uingie-ukoma/