by Nuru ya Upendo | 14 October 2025 08:46 pm10
Siku moja Yesu alipokuwa anahubiri katika nyumba fulani, watu wengi walikusanyika mahali pale, na ghafla wakamletea mtu aliyepooza mwili mzima hawezi kufanya lolote, wakamweka Mbele yake ili amponye. Lakini tunaona mwitikio wa Yesu ulikuwa ni tofauti na matarajio yao. Bwana Yesu hakumwekea mikono na kumwambia simama uende, bali alimwambia..
Rafiki, umesamehewa dhambi zako.
Luka 5:17-20
[17]Ikawa siku zile mojawapo alikuwa akifundisha, na Mafarisayo na waalimu wa torati walikuwa wameketi hapo, waliotoka katika kila kijiji cha Galilaya, na Uyahudi, na Yerusalemu; na uweza wa Bwana ulikuwapo apate kuponya.
[18]Na tazama, wakaja watu wanamchukua kitandani mtu mwenye kupooza; wakataka kumpeleka ndani na kumweka mbele yake.
[19]Hata walipokosa nafasi ya kumpeleka ndani kwa ajili ya lile kundi la watu, walipanda juu ya dari wakampisha katika matofali ya juu, wakamshusha yeye na kitanda chake katikati mbele ya Yesu.
[20]Naye alipoiona imani yao, alimwambia, Ee rafiki, umesamehewa dhambi zako.
Jicho la mwanadamu linaona uponyaji ni kutendewa muujiza wa nje, lakini kwa Mungu Uponyaji hasaa ni kusamehewa dhambi. Mtu akishasamehewa dhambi, mengine yote hufuata..
Tunasamehewaje dhambi?
Kwa kumwamini Bwana Yesu na kumaanisha kumfuata kwa toba ya kweli. Hapo ndipo tunapopokea Msamaha Wa dhambi zetu, na hatimaye uponyaji Wa mambo yetu mengine yote.
Wakolosai 1:13-14
[13]Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake;
[14]ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi;
Matendo ya Mitume 26:18
[18]uwafumbue macho yao, na kuwageuza waiache giza na kuielekea nuru, waziache na nguvu za Shetani na kumwelekea Mungu; kisha wapate msamaha wa dhambi zao, na urithi miongoni mwao waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu mimi.
Ni ajabu Kuona, watu wanakwenda kwa Yesu na mapooza Yao, wengine katika afya zao kama huyu, wengine mapooza ya shughuli zao, wengine katika familia Zao n.k. wakitarajia Yesu awaponye kwa njia zao.
Lakini wanapokutana Na injili za wokovu na kuacha dhambi.. wanazikwepa wanakimbilia kwenye maombezi na mafuta Ya upako.
Ndugu fahamu kuwa asili ya kila tatizo ni dhambi..Mahali ambapo maisha yako yanawekwa wazi, yanamulikwa hapo ndipo uponyaji wako halisi upo. Usikimbie, usitange-tange.
Pokea kwanza msamaha wa dhambi mengine yafuate…kubali wokovu, kubali uzima, uponywe. Itakufaidia nini upate ulimwengu wote, afya yote, amani yote kisha akateketee tena jehanamu milele baadaye?
Ikiwa bado hujaokolewa (yaani hujapata msamaha wa dhambi zako) basi wakati ndio huu.. wasiliana nasi kwa namba hizi kwa mwongozo wa kumpokea Yesu.
Bwana akubariki.
Shalom
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
UNAWAZA NINI SASA, JUU YA UFALME WA MBINGUNI?
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/10/14/umesamehewa-dhambi-zako/
Copyright ©2025 Wingu la Mashahidi unless otherwise noted.