UZURI WA MAJIVU.

by Nuru ya Upendo | 17 October 2025 08:46 pm10

Isaya 61: 1-3

1 Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta …
kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, WAPEWE TAJI YA MAUA BADALA YA MAJIVU, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito; wapate kuitwa miti ya haki, iliyopandwa na Bwana, ili atukuzwe.

Kitu kikishachomwa na kuteketea kabisa, kinachosalia cha mwisho kabisa huwa ni majivu. Majivu hayana thamani yoyote, ni vumbi jembamba, ambalo likikanywagwa, hutoweka kabisa.

Hivyo zipo nyakati ambazo, watu wanakuwa kama majivu mbele ya macho yao wenyewe, au kwa wengine. Yaani Kila kitu kimekufa na kuteketea kabisa, yale maono aliyokuwa nayo yamefutika, wengine afya zao zimekuwa jivu,hawana matumaini ya kupona tena, wengine maisha yamevurugika, akiangalia muda aliochezea  moyo unapoa kabisa, wengine mahusiano yao yametafunwa, haoni kuendelea mbele.. Rohoni akijiangalia ni jivu tu, kila mahali ni jivu  hajasaliwa na chochote, isipokuwa kukata tamaa na kupotea kabisa..

Ndio maana katika enzi za biblia mtu aliyekuwa katika maombolezo Makali, alijimwagia majivu mwilini kama ishara kuwa umepukutika kabisa..Mfano wa hawa ni Ayubu na Mordekai (Ayubu 2:8, Esta 4:1 )

Lakini Mungu afufuaye matumaini, alitoa unabii huu juu ya mwanawe atakayekuja kuukomboa ulimwengu, akasema..

Amemtia mafuta, “ili awape watu wake taji ya maua badala ya majivu..”

Tafsiri yake, ni kuwa sio tu atamwondoa kwenye majivu  na kumwacha, Hapana, bali anambadilishia na kumpa taji la maua.

Maua huwakilisha heshima, cheo, hadhi, baraka, afya.

Hivyo haijalishi utakuwa katika hali isiyoeleweka kiasi gani, Yupo Yesu wa kukuondoa majivuni na kukuvika maua, ‘Majivu yako leo ndio maua yako baadaye, lakini ikiwa tu utakuwa ndani ya Kristo’.

Usihofu wala usiogope, wala usikate tamaa..Magonjwa hugeuzwa afya.

Yusufu alikuwa majivu gerezani, lakini Mungu alimfanya maua katika kiti cha Farao. Petro alikuwa jivu kwa kumkana Bwana wake, lakini ndiye alikuwa mjenzi wa  kanisa la Kristo. Ruthu alikuwa mjane kwa kufiwa na mumewe, lakini Bwana alimwekwa kama mama wa uzao wa kifalme, Haijalishi hutafaa kwa jinsi gani leo, Kristo yupo kukugeuza, na kukuondoa majivuni.

Lakini hii inahitaji kumpokea na kuendelea kuishi ndani yake. Je upo tayari kuyakabidhi leo maisha yako kwake?

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

MAISHA YA UVUGUVUGU, YANAMFANYA MUNGU AUMWE.

Kwanini mkono wa Musa uingie ukoma?

UMESAMEHEWA DHAMBI ZAKO.

WhatsApp
DOWNLOAD PDF

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/10/17/uzuri-wa-majivu/