by Nuru ya Upendo | 28 October 2025 08:46 pm10
Mwanzo 3:15
[15]nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa..
Kitu pekee Ambacho kilitabiriwa kuweza kuvunja vichwa vya majoka(shetani), ni uzao wa mwanamke tu. Aliyetabiriwa kwenye (Mwanzo 3:15)
Uzao huu wa mwanamke ni Yesu Kristo.. kwasababu ni yeye tu pekee ndiye aliyezaliwa Bila mwanamume, sisi wote ni uzao wa mwanamume…kwasababu mbegu yetu imetoka kwa Baba zetu, lakini Kristo ni mbegu iliyoshuka Kutoka mbinguni, ndio maana hapo anatajwa Kama uzao wa mwanamke.
Yeye kwa ushindi alioupata dhidi ya nguvu za giza kwa kufufuka kwake kutoka kwa wafu na kupaa mbinguni..ni pigo Kubwa sana kwa shetani, ambalo lilimlenga moja kwa moja katika kichwa chake.
Kwasababu kwa njia hiyo wanadamu tumevuka kutoka mautini kwenda uzimani…
Lakini habari njema ni kuwa yeyote amwaminiye, anakuwa sehemu ya uzao huo kwa imani. Na hivyo anapokea mamlaka ile ile ya kuvunja mafuvu ya majoka…mpaka ufalme wa giza kutokomea kabisa katika uso wa ulimwengu..
Wagalatia 3:29
[29]Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.
Luka 10:19
[19]Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.
Kumbuka uwezo huu, hakuna uzao mwingine wowote unaoweza kumuharibu shetani, waafrika hawawezi, wazungu hawawezi, wachina hawawezi, waarabu hawawezi, ukoo wa kiyahudi hauwezi, familia za kichifu, haiwezi, wanadamu wote hawawezi kuponda majoka, hata waungane kwa vifaru vyao na makombora ya nyuklia, bado hawawezi kinyume chake wao ndio watafanyika chakula cha hao majoka.Ni uzao mmoja tu wa Yesu Kristo ndio wenye nguvu hizo..
Swali ni je! Tunapondaje vichwa vya majoka.
Ni kwa kuendelea kuhubiri. Ukikaa tu bila kushuhudia habari za Kristo kwa wenye dhambi, kukaa bila kujishughulisha na shamba la Bwana..Fahamu kuwa ‘mabuti’ yako uliyopewa huko miguuni huyatendei Haki..yapo tu!
Unamridhia shetani, unafurahishwa na uwepo wake shambani mwa Bwana, ndugu njia pekee inayomdosha shetani kwa wepesi ni wewe kukutana na mwenye dhambi mmoja na kumshuhudia habari za wokovu.
Mitume walipoenda kuhubiri baada ya kutumwa na Yesu, waliporudi na ushindi, Yesu aliwaambia nalimwona shetani akianguka kutoka mbinguni kama umeme..
Luka 10:18
[18]Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme.
Simama tumia mabuti yako vizuri, endeleza kuponda, ponda kweli kweli, haribu kisawasawa, kwa njia ya injili.
Sio kwa kuimba “nakuponda shetani” au
Kusema “toka shetani” bali kwa injili
Kuponda kwingine ni maombi na kuishi maisha ya utakatifu, huku nako kunahubiri injili ya Kristo na hivyo shetani anaumizwa vibaya sana.
Amka tumia buti zako, kila kichaka katika shamba la Bwana ambacho majoka yamejificha Ni kwenda kuponda tu, mpaka habari njema za ufalme zifike ulimwenguni kote.
Bwana awe nawe.
Amen.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
IHUBIRI INJILI, KILA MAHALI KWASABABU AKUZAYE NI MUNGU.
INJILI NI UWEZA WA MUNGU, UULETAO WOKOVU.
MBONA MMESIMAMA HAPA MCHANA KUTWA BILA KAZI?
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/10/28/endeleza-upondaji/
Copyright ©2025 Wingu la Mashahidi unless otherwise noted.