Watu wa zamani walitumia nini kujua saa, dakika na sekunde?

by Nuru ya Upendo | 25 November 2025 08:46 am11

Swali: Kwasasa tunatumia kifaa kinachoitwa saa (iwe na ukutani, mkononi au kwenye simu) kujua sekunde, dakika na saa.. Je watu wa zamani walijuaje sekunde, dakika na saa?


Jibu: Nyakati za Biblia siku iligawanywa katika masaa 12 ya mchana na masaa 12 ya usiku, tunalithibitisha hilo katika Yohana 11:19-20.

Yohana 11:9 “Yesu akajibu, Je! Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu akienda mchana hajikwai; kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu.

10 Bali akienda usiku hujikwaa; kwa sababu nuru haimo ndani yake”.

Hii ikimaanisha kuwa ni kweli enzi za Bwana YESU akiwa duniani, siku ilikuwa ikigawanywa katika mgawanyo wa masaa.. Lakini kuhusiana na mgawanyo wa sekunde Biblia haituonyeshi mahali popote kwamba watu wa kale waligawanya saa katika sekunde, hivyo hakukuwa na mgawanyo wa sekunde katika kila saa.

Sasa swali walijuaje kuwa lisaa limoja limekwisha na limeingia lingine, na hatimaye kumaliza yote 12 ya mchana na usiku? Na ilihali hawakuwa na saa kama za kwetu zinazohesabu masaa?

Watu wa kale hawakutumia saa za mkononi kama za kwetu, katika kuigawanya siku katika masaa, bali walitumia njia za asili kuigawanya siku katika masaa 12, na njia hizo ni kutazama Jua, kutumia kivuli cha jua, kipimo cha maji, na saa ya mchanga, kipimo cha nyota tutazamame kimoja baada ya kingine kwa ufupi.

  1. Kipimo cha kutazama jua.

Asuhuni kulipopambazuka walijua ni saa moja, na Jua lilipofika la utosini waliweza kujua ndio nusu ya siku, yaani saa sita mchana, na lilipozama waliweza kujua ni saa 12 jioni, hivyo wakati jua likiwa katikati ya moja na saa sita mchana waliweza kukadiria masaa hayo ya katikati, vivyo hivyo na jioni, na njia hii ndio iliyotumika sana na wayahudi katika kujua masaa.

   2. Saa ya kivuli cha Jua (Sundial).

Hii ni njia iliyotumika kwa kutazama mwelekeo wa kivuli cha jua, na ndio ile iliyotajwa katika Isaya 38:8, wakati wa mfalme Ahazi.

   3. Saa ya Maji.

Hii ilitumika zaidi wakati wa usiku, ambapo kiwango cha maji kilidondoka kidogo kidogo katika kifaa husika, na njia hii ilitumiwa sana na watu wa Babeli.

   4. Saa ya Mchanga.

Mchanga uliwekwa katika kifaa maalum, na baadaye kuachiwa kudondoka kidogo kidogo.

  5. Kipimo cha Nyota.

Kipimo hiki kilitumika nyakati za usiku ambapo waliangalia nafasi za makundi ya nyota kama vile Orioni, na Kilimia.

Kwahiyo kwa ufupi ni kwamba enzi za Biblia walitumia zaidi kipimo cha jua na kivuli cha jua kujua mgawanyo wa masaa.

Sasa kwa urefu kwanini Bwana YESU asema saa za mchana si 12, fungua hapa >>>NI SAA KUMI NA MBILI (12) TU, ZA KRISTO KWAKO.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

JAWA NA UPENDO UNAOTAFUTA.

FAIDA NYINGINE YA MAOMBI YA KUSHUKURU.

FUNGUA KINYWA CHA ROHO MTAKATIFU KIHUDUMU.

USIKAWIE- KAWIE KUUFUNGUA MOYO WAKO

JE! UMEFIKIA VIGEZO VYA KUWA BABA ROHONI?

WhatsApp
DOWNLOAD PDF

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/11/25/watu-wa-zamani-walitumia-nini-kujua-saa-dakika-na-sekunde/