by Nuru ya Upendo | 4 December 2025 08:46 am12
Jibu: Turejee..
1Wakorintho 9:27 “BALI NAUTESA MWILI WANGU na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa”.
Kuutesa mwili kunakozungumziwa hapa si kujiumiza kwa viboko na mapigo… bali ni kuuzuia mwili kupata vitu viupendavyo, ili makusudi kutimiza mapenzi ya MUNGU.
Mfano wa vitu ambavyo vikizidi sana kufanyika katika mwili vinaathiri mbio za kiroho ni pamoja na VYAKULA NA USINGIZI vipo na vingine vingi lakini hivi ndio vikuu..
1. VYAKULA
Kula kila wakati kwa kipindi kirefu bila kuwa na vipindi vya KUFUNGA kunaathiri ukuaji wa kiroho na kuna mambo ambayo hayatatokea, kwani Biblia imesema mambo mengine hayawezekaniki isipokuwa kwa kufunga na kuomba..
Mathayo 17:19 “Kisha wale wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha wakasema Mbona sisi hatukuweza kumtoa?
20 Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.
21 [LAKINI NAMNA HII HAITOKI ILA KWA KUSALI NA KUFUNGA.]”
Kwahiyo Mtu mwenye desturi ya kufunga mara kwa mara na kuomba anakuwa anautesa mwili wake lakini anakuwa anapata faida kubwa rohoni
2. USINGIZI.
Mtu anayejizuia kulala kwa lengo la kuutafuta uso wa Mungu kwa Maombi, pia anahesabika kuwa anautesa mwili, na faida yake pia ni kubwa..
Marko 14:37 “Akaja akawakuta wamelala usingizi, akamwambia Petro, Je! Simoni, umelala? Hukuweza kukesha saa moja?
38 Kesheni mwombe, msije mkaingia majaribuni, roho i radhi ila mwili ni dhaifu”.
Na mwisho kumbuka, kujizua kufanya dhambi kama uzinzi, ulevi, sio kuutesa mwili, bali ndio kuupa mwili pumziko..kwasababu dhambi ni sumu ya mwili pia, dhambi inauharibu mwili… Mtu anapojiuzuia kutenda dhambi katika mwili, mwili wake hauteseki badala yake ndio unajengeka zaidi, kwahiyo usichanganye kutotenda dhambi na kuutesa mwili.
Ukiona dhambi kama Ulevi au Uzinzi au nyingine yoyote inakufanya mateka, kiasi kwamba usipoifanya mwili wako unateseka basi ni dalili ya kuwa bado utakaso kamili haujaingia maishani mwako, hivyo ni wakati wa kumgeukia Bwana kwa moyo wote kwa kutubu, kubatizwa kwa ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Bwana YESU na kisha kupokea Roho Mtakatifu,
Na ile sheria ya Roho wa uzima itakuweka huru mbali na dhambi, BUREEEEE kabisa..
Warumi 8:2 “Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti”.
Bwana atusaidie tuitese miili yetu kwa kufunga na kuzuia usingizi, ili tupate muda wa kukesha na kuomba kwa faida ya roho zetu.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
TOFAUTI KATI YA SHERIA YA ROHO WA UZIMA NA SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI!
Nini maana ya “Andiko huua, bali Roho huhuisha (2Wakorintho 3:6)
SI KWA UWEZA WALA KWA NGUVU BALI KWA ROHO YANGU, ASEMA BWANA.
Sheria ya uhuru ni ipi? (Yakobo 2:12)
Je kuna haja gani ya kuamini biblia iliyoandikwa na watu?
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/12/04/nini-maana-ya-ninautesa-mwili-1wakorintho-927/
Copyright ©2026 Wingu la Mashahidi unless otherwise noted.