Mtume Paulo aliyathibitishaje Makanisa na Wanafunzi? (Matendo 15:40-41)

by Nuru ya Upendo | 5 January 2026 08:46 am01

Jibu: Turejee..

Matendo 15:40 “Lakini Paulo akamchagua Sila, akaondoka, akiombewa na wale ndugu apewe neema ya Bwana.

41 Akapita katika Shamu na Kilikia AKIYATHIBITISHA MAKANISA”.

Tunasoma pia akiwathibitisha Wanafunzi katika Matendo 18:23

Sasa maana ya “kuyathibitisha Makanisa na Wanafunzi”  ni Ziara za kuwatembelea wanafunzi/waamini ambao tayari wameshapokea Injili, na kuwatia Nguvu katika Imani, kwa njia ya kuwafundisha na kuwakumbusha kanuni za Imani ya kikristo na kudumu katika misingi huo.

Vile vile katika kutatua changamoto zilizokuwa ngumu kutatulika na pia na kuwateua Maaskofu na Mashemasi katikati ya waamini hao, watakaowachunga na kuliangalia kundi..

Kwa mfano tunasoma katika Matendo 14:21-22, Mtume Paulo na wenzake wakirejea Listra, Ikonio na Antiokia kufanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika ile Imani..

Matendo 14:21 “Hata walipokwisha kuihubiri Injili katika mji ule, na kupata wanafunzi wengi, wakarejea mpaka Listra na Ikonio na Antiokia,

22 wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika ile Imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi.

23 Na walipokwisha kuwachagulia wazee katika kila kanisa, na kuomba pamoja na kufunga, wakawaweka katika mikono ya Bwana waliyemwamini”

Utasoma pia katika Matendo Tito 1:5, akiagiza uteuzi wa viongozi watakaoliangalia kundi.

Tito 1:5 “Kwa sababu hii nalikuacha Krete, ili uyatengeneze yaliyopunguka, na kuweka wazee katika kila mji kama vile nilivyokuamuru”

Mambo kama hayo pia tunapaswa kuyafanya sasahivi,  Katika siku hizi za mwisho ambapo shetani anafanya kazi kwa nguvu kuyaharibu makanisa, hatuna budi kusimama kwa nguvu na kuyathibitisha makanisa yetu kwa msaada wa MUNGU.

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Kwanini Roho Mtakatifu amzuie Paulo kuipeleka injili Asia? (Matendo 16:6-7).

Je Paulo, alihimiza kusikiliza nyimbo za kidunia kulingana na Matendo 17:28

Paulo aliwapaje watu karama ya rohoni?

Kwanini Roho Mtakatifu amzuie Paulo kuipeleka injili Asia? (Matendo 16:6-7).

Uchambuzi wa kitabu cha pili cha Paulo kwa Timotheo (2Timotheo).

WhatsApp
DOWNLOAD PDF

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2026/01/05/mtume-paulo-aliyathibitishaje-makanisa-na-wanafunzi-matendo-1540-41/