Matendo 17:28 Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake.
29 Basi, kwa kuwa sisi tu wazao wa Mungu, haitupasi kudhani ya kuwa Uungu ni mfano wa dhahabu au fedha au jiwe, vitu vilivyochongwa kwa ustadi na akili za wanadamu.
JIBU: Paulo alipofika Athene, na kuona jinsi mji ule ulivyojaa sanamu nyingi, maandiko yanatuambia moyo wake ulichukizwa sana, hivyo kama ilivyo desturi yake kuhubiri injili, alijua njia mojawapo ya kuwavuta watu ni “kujiungamanisha nao”, kwa kuwagusia kwanza yale mambo mema waliyoyafikiri au kuyatenda.
Ndio maana utaona kabla ya kuwagusia kuhusu huyo mtunga mashairi, aliwaambia kuhusu madhabahu waliyoijenga, ambayo waliipa jina la “MUNGU ASIYEJULIKANA”
Matendo 17:23 Kwa sababu nilipokuwa nikipita huko na huko na kuyaona mambo ya ibada yenu, naliona madhabahu iliyoandikwa maneno haya, KWA MUNGU ASIYEJULIKANA. Basi mimi nawahubirini habari zake yeye ambaye ninyi mnamwabudu bila kumjua.
Paulo akaanza kuwahubiria Kristo kwa kupitia huyo wanayemwabudu kimakosa, Lakini tunajua Paulo, hakuwa na ushirika wowote na mifumo yao ya kipagani, wala hakuwahimiza waendelee kumwabudu Kristo kwa njia yao hiyo hiyo.
Tunaona katika kuendelea kujiungamanisha zaidi ya wenyeji wale wa Athene, Paulo akagusia tena habari nyingine za mtunga mashairi, ambaye alikuwa maarifu katikati yao, nyimbo zake zilivuma na kila mmoja alikuwa anazijua, na ndani ya mashairi yake, aliweka vina vinavyoeleza kuwa sisi sote ni wazao wake, au kusema sisi sote ni watoto wa Mungu.
Hivyo akatumia tena fursa hiyo, kuwaeleza uhai wa Mungu, ikiwa sisi tumezaliwa na yeye, basi haiwezekani Baba yetu akawa mfano wa sanamu, ni lazima tu atakuwa mwenye akili, ufahamu, na uelewa kama sisi na zaidi, na sio kama kipande cha mti.
Kwa njia hiyo Paulo akawapata watu wengi, kwa Kristo.
Lakini hatuoni mahali popote akiwaambia wawe wafuatiliaji au mashabiki, wa nyimbo za kidunia.Hiyo ilikuwa njia ya kuwapata wapagani, wamjue Kristo.
Kinyume chake Paulo katika nyaraka zake, anahimiza, waamini kutofuatisha namna ya dunia hii (Warumi 12:1). Na kuhimiza uimbaji unaomtukuza Mungu na kutujenga sisi nafsi zetu kwake ndio unaopaswa kwa wakristo.
Waefeso 5:19 mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu;
20 na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo;
Wakolosai 3:16 Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.
17 Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.
Hivyo hatuoni mahali popote Paulo akikubaliana na usikilizaji wa nyimbo za kidunia, wala sisi kama wakristo, hatupaswi kujikita huko, kwasababu tumeshajua ni nani hasaa wa kumwimbia na kumsifu, na wa kumburudikia.
Mungu akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Kuharimishwa ni nini, na kwanini Paulo aombe hivyo?(Warumi 9:2).
Ni kwa namna gani Bwana YESU alikula Siagi na Maziwa? (Isaya 7:15)
About the author