Je tumepewa kujua nyakati na majira ya kurudi kwa Bwana au la?.

Je tumepewa kujua nyakati na majira ya kurudi kwa Bwana au la?.

Swali: Katika Matendo 1:7, tunaona Bwana anasema si kazi yetu kujua nyakati na majira ya kuja kwake,

Lakini katika 1Wathesalonike 5:1-2 tunasoma Mtume Paulo akisema kuhusu nyakati na majira kuwa hana haja ya kutuandikia kwasababu sisi wenyewe tunajua…je hii imekaaje?..je kuna mkanganyiko hapo?


Jibu: Awali, tuirejee mistari hiyo…

Matendo 1:6 “Basi walipokutanika, wakamwuliza, wakisema, Je! Bwana, wakati huu ndipo unapowarudishia Israeli ufalme?

7 Akawaambia, Si kazi yenu kujua NYAKATI WALA MAJIRA, Baba aliyoyaweka katika mamlaka yake mwenyewe”.

Tusome tena habari ya Paulo…

1 Wathesalonike 5:1 “Lakini, ndugu, kwa habari ya NYAKATI NA MAJIRA, hamna haja niwaandikie.

2 Maana ninyi wenyewe MNAJUA yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku”.

Ni muhimu kufahamu kuwa hakuna mkanganyiko wowote kwenye biblia, na wala haijichanganyi,

Sasa Paulo aliposema kuwa “hana haja ya kuandika kuhusu nyakati na majira kwasababu tayari wameshajua”.. hakumaanisha kuwa tayari wameshajua/tumeshajua siku na tarehe za kurudi Bwana YESU, LA! Hakumaanisha hivyo, vinginevyo angekuwa ameenda kinyume na maneno hayo ya Bwana YESU aliyosema kuwa “Si kazi yetu kujua majira na nyakati” na tena aliposema “hakuna ajuaye siku wala saa”.

Sasa ni kitu gani Paulo alichomaanisha kuwa tayari wameshakijua, au tumeshakijua kuhusu nyakati na majira?.

Kitu ambacho tayari Wathesalonike pamoja na sisi tumeshakijua kuhusu Nyakati na Majira ya kurudi kwa YESU sio ile tarehe atakayokuja, hapana!.. bali tulichokijua kuhusu Nyakati na Majira ya kurudi kwa YESU ni kwamba “ATAKUJA KAMA MWIVI”… Hicho ndicho Paulo alichokimaanisha.

Na ni lini tulijua hilo?…tulijua kupitia maneno ya Bwana YESU mwenyewe..
Mathayo 24:40 “Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa;
41 wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa.
42 Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu.
43 Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angaliijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa.
44 Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja”

Ndio maana tukiendelea mistari ya mbele kidogo mpaka ule mstari wa tatu tutaona Paulo analielezea zaidi…

1 Wathesalonike 5:1 “Lakini, ndugu, kwa habari ya NYAKATI NA MAJIRA, hamna haja niwaandikie.

2 Maana ninyi wenyewe MNAJUA yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.

3 Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa”.

Kwahiyo biblia haijichanganyi popote, wala Paulo hakusema kitu chochote tofauti na BWANA YESU.

Je umempokea Mwokozi YESU?..Je wajua kuwa dakika yoyote parapanda italia, na watakaonyakuliwa ni wale tu waliojitaka, je utakuwa wapi siku ile ikiwa leo hii hutaki kubadili njia zako?.

Jibu unalo!

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments