Je wana wa Israeli waliofia jangwani, walienda mbinguni au jehanamu?

by Nuru ya Upendo | 19 February 2026 08:46 pm02

JIBU: Wakiwa jangwani wana wa Israeli walitenda  makosa  ya aina mbili.

  1. Makosa yaliyopoteza Ahadi
  2. Makosa yaliyopoteza Uzima wa milele.

Makosa yaliyopoteza Ahadi ndio yalikuwa yale ya kutokuamini. Mfano Mungu alipowatoa jangwani, na kuwavusha, mara nyingi walionyesha hali ya kutoamini, Kosa ambalo liliwafanya Mungu aghahiri kuwafikisha kule alipowaahidia, ambapo ni nchi ya Kaanani ibubujikayo maziwa na asali, Na kilele cha kosa hilo kilikuja  pale wale wapelelezi waliporudi katika kuichunguza nchi, na kutoa ripoti za kule, kwamba wao wanaonekana kama mapanzi, hivyo wote wakaanza kulia na kutaka kurudi Misri, Ndipo Mungu akakasirika sana na kuapa kuwa wote  hawataiona hiyo nchi ya Kaanani isipokuwa Kalebu na Yoshua, kwasababu wao hawakuonyesha kutokuamini.

Hesabu 14:21-24

21 lakini hakika yangu, kama niishivyo, tena kama dunia hii nzima itakavyojawa na utukufu wa Bwana;
22 kwa sababu watu hawa wote, ambao wameuona utukufu wangu na ishara zangu, nilizozitenda huko Misri, na huko jangwani, pamoja na haya wamenijaribu mara hizi kumi, wala hawakuisikiza sauti yangu;
23 hakika yangu hawataiona hiyo nchi niliyowaapia baba zao, wala katika hao wote walionidharau hapana atakayeiona;
24 lakini mtumishi wangu Kalebu, kwa kuwa alikuwa na roho nyingine ndani yake, naye ameniandama kwa moyo wote, nitamleta yeye mpaka nchi hiyo aliyoingia; na uzao wake wataimiliki

Lakini hiyo haikumaanisha kuwa hawatakwenda mbinguni, kwasababu wapo waliotubu,hata wakati ule ule

Kwahiyo kusema adhabu ile ndio iliwapelekea moja kwa moja kupoteza mbingu si sahihi.

Kwasababu Mungu aliendelea kutembea nao kwa wingu lake, baadaye akawainua viongozi, wa kuwaaamua na Pamoja na wazee, akawamwagia  Roho wake, (Hesabu 11:25). Hivyo kama Mungu kasingekuwa nao, basi hayo yote yasingefanyika, kwasababu Mungu hawezi kuwaongoza wafu.

Lakini yapo makosa ambayo yaliwagharimu adhabu ya kupoteza kabisa uzima wa milele. Na makosa kama hayo ndio yale ya makusudi kabisa, mfano wa hayo ni yale ya kuvunja amri za Mungu, kama vile kutengeneza sanamu ya ndama  na kuiabudu, Kuzini, kuwa na miungu mingine, na kuhalifu sabato za Mungu .

Makosa kama hayo ndio yaliyopelekea  kupoteza uzima wa milele, ndio maana ukichunguza utaona watu kama hawa walipokea adhabu za moja kwa moja.     Hivyo ni kuwa makini sana na neema ya Mungu.

Hata sasa, zipo dhambi za aina mbili zinazozungumziwa kwenye maandiko, dhambi za mauti, na dhambi zisizo za mauti.

Kwa urefu wa maelezo yake, pitia hapa>>> DHAMBI YA MAUTI

Mungu akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Je shauri la kuipepeleza Kanaani lilitoka kwa wana wa Israeli au kwa BWANA?

Kwanini Roho Mtakatifu amzuie Paulo kuipeleka injili Asia? (Matendo 16:6-7).

WhatsApp
DOWNLOAD PDF

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2026/02/19/je-wana-wa-israeli-waliofia-jangwani-walienda-mbinguni-au-jehanamu/