by Nuru ya Upendo | 19 February 2026 08:46 pm02
Mithali 29:20
Je! Umemwona mtu mwenye kuhamaki katika maneno? Afadhali kumtumaini mpumbavu kuliko yeye
Mtu mwenye kuhamaki.
Ni mtu anayezungumza maneno kwa haraka, yaani anayezungumza bila kufikiri, au kujizuia.
Vitu kama mizaha, ugomvi, hasira, uongo, na mafarakano, huzaliwa na tabia kama hii ya watu kunena bila kufiriki.
Kwamfano, mtu anaweza kukutukana, na wakati huo huo hasira ikawaka ndani, sasa kwasababu huwezi kujizuia, unajikuta unarudisha majibizano, hatimaye na wewe unafungua kinywa chako unatukana.
Au labda unatambua jambo Fulani ambalo si jema, na pengine ukilisema linaweza lisiwe na maana yoyote, kinyume chake likazua ugomvi, au kumuabisha mwingine, au sintofahamu, lakini wewe kwasababu huwezi jizuia unalisema, mwishowe matatizo yanazuka makubwa yasiyokuwa na lazima.
Watu wanaoapa, ni matokeo ya kunena bila kufikiri, mafarisayo ambao walitenda dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu ni kwasababu ya maneno ambayo hayana hekima nyuma yake.
Mathayo 12:36 Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu.
37 Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa.
Mpaka hapo unaweza kuona ni kwanini mpumbavu anaweza kuonekana ana afadhali kuliko mtu mwenye kuhamaki.
Mstari huu unatukumbusha nguvu iliyopo katika maneno, biblia inasema ulimi ni kama moto ni kiungo kidogo lakini kinawasha misitu, hivyo hatuna budi kuwa wazito katika kunena, tukifiri kwanza ndipo tuseme. Yakobo 1:19
19 Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika;
Maneno yana nguvu, kila siku yatupaswa tujifunze kudhibiti vinywa vyetu.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
SHUGHULIKA NA HASIRA INAYOKAA KIFUANI
KARAMA TUZIPATAZO KWA MSAADA WA WATU WENGI.
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2026/02/19/maana-ya-mithali-2920-je-umemwona-mtu-mwenye-kuhamaki-katika-maneno/
Copyright ©2026 Wingu la Mashahidi unless otherwise noted.