by Nuru ya Upendo | 26 March 2026 08:46 am03
Mathayo 8:29
[29]Na tazama, wakapiga kelele, wakisema, Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja kututesa kabla ya muhula wetu?
Mashetani yanajua kila jambo lipo katika mpangilio wa muda wake, yanajua kuwa tayari hukumu ilishatolewa ya wao kutupwa katika ziwa la moto lililo hatma yao ya milele..
Lakini utekelezaje wake, utakuja baadaye, ambao utakuwa ni mwisho wa dunia, utakao asisiwa na Bwana Yesu Kristo mwenyewe.(Mathayo 25:41)
Wengi tunadhani mapepo, hushindana na sisi, kwa kutuonea wivu, hilo ni kweli kwa sehemu, lakini sababu kubwa ya mapepo na shetani kushindana na sisi…ni wao kujilinda…na adhabu ijayo.
Na wanajua mwanadamu ndiye anayeweza kuiharakisha hiyo siku au kuikawiisha hiyo siku. Ndio maana yanafanya kazi kubwa sana kuwaharibu wanadamu ili siku hiyo isifike upesi.
Hizi ni njia tatu mapepo, hufanya kwa watu ili kukawiisha muhula wao usiwafikie haraka.
1) Kuchochea maovu.
2) Kukengeusha Imani za watu
3) Kukawisha injili
Maovu mengi, humsukuma Mungu kuwa mvumilivu na wanadamu, ili wafikie toba wasiangukie hukumu ya mapepo..Kama wanadamu wasingekuwa na shingo ngumu, mwisho wa dunia na hukumu yao ingeshafika zamani sana.. hivyo mapepo wanabuni kazi mbalimbali ili kuwafanya wanadamu wazidi kupotoka.
2 Petro 3:9-11
[9]Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.
[10]Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.
[11]Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa,
Luka 18:8
[8]Nawaambia, atawapatia haki upesi; walakini, atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani?
Kristo anatarajia kanisa lake kusimama katika msingi wa imani kamili ambayo haijaharibiwa wala kuvurugwa na mapokeo na mafundisho ya uongo.. hii ndio sababu ya shetani kuinua makundi ya manabii wa uongo, kufundisha injili nyingine ambayo Kristo hajaileta duniani. Matokeo yake ndio kuwa na kundi kubwa la wakristo lakini dhaifu wasio tayari kumlaki Bwana mawinguni.
Mathayo 24:14
[14]Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.
Injili ya kweli adui huipiga vita vikubwa..Na wanajua ikihubiriwa ulimwenguni kote, basi ushuhuda wa Mungu utakuwa umefika na hakuna atakayekuwa na udhuru.
Sasa mimi na wewe hatuna budi kusimama katika utakatifu lakini pia imani na injili kuisambaza ili watu waokolewe…
Kumbuka tayari tupo kwenye siku za mwisho, Amka simama na Bwana.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
MAPEPO YANATAFUTA HIFADHI NDANI YAKO KWA BIDII SANA.
Je mkristo anaweza akawa na mapepo?
Shetani anaishi wapi, Je! Amefungwa au yupo kuzimu?
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2026/03/26/fupisha-muhula-wa-mashetani/
Copyright ©2026 Wingu la Mashahidi unless otherwise noted.