by Nuru ya Upendo | 27 March 2026 08:46 pm03
Swali: Katika kitabu cha Matendo 13:33 tunasoma pakitajwa “Zaburi ya Pili” je hii zaburi ya Pili ni ipi, nay a kwanza ni ipi na ya mwisho ni ipi?
Jibu: Tuanzie kusoma ule mstari ule wa 32..
Matendo 13:32 “Na sisi tunawahubiri habari njema ya ahadi ile waliyopewa mababa,
33 ya kwamba Mungu amewatimizia watoto wetu ahadi hiyo, kwa kumfufua Yesu; kama ilivyoandikwa katika ZABURI YA PILI, Wewe ndiwe Mwanangu, mimi leo nimekuzaa”.
Andiko hilo ni Mtume Paulo alikuwa akilirejea kutoka katika kitabu cha Zaburi ule mlango wa Pili, ambapo ndipo tunaposoma maandiko hayo..
Zaburi 2:7 “Nitaihubiri amri; Bwana aliniambia, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa”.
Kwahiyo tafsiri rahisi ya “Zaburi ya Pili” anayoizungumzia Mtume Paulo katika hiyo Matendo 13:33 ni “Zaburi Mlango wa PIli au Zaburi sura ya Pili”.. ndipo unabii huo unapotokea.. Na Zaburi ya Tatu ni Zaburi mlango wa tatu… na Zaburi ya mia na hamsini ni Zaburi mlango wa mia na hamsini (150).
Lakini pia tunasoma mahali pengine, mwandishi wa kitabu cha Wabrania akinukuu Zaburi hiyo ya Pili..
Waebrania 1:5 “Kwa maana alimwambia malaika yupi wakati wo wote, NDIWE MWANANGU, MIMI LEO NIMEKUZAA? Na tena, Mimi nitakuwa kwake baba, Na yeye atakuwa kwangu mwana?”
Na tena akarudia katika ule mlango wa tano.
Waebrania 5:5 “Vivyo hivyo Kristo naye hakujitukuza nafsi yake kufanywa kuhani mkuu, lakini yeye aliyemwambia, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa.”
Je umempokea YESU?.. kama bado unasubiri nini?. Fahamu kuwa hizi ni siku za mwisho na YESU amekaribia sana kurudi.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Fahamu mana ya Zaburi 48:14 Yeye ndiye atakayetuongoza
Mafuta mabichi ni mafuta ya aina gani? (Zaburi 92:10)
Fahamu maana ya Zaburi 125:3 “ Kwa maana fimbo ya udhalimu Haitakaa juu ya fungu la wenye haki.
Uele ni nini katika biblia? (Zaburi 91:6)
Nini maana ya neno kumwamba (Zaburi 78:19)
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2026/03/27/zaburi-ya-pili-ni-nini-matendo-1333/
Copyright ©2026 Wingu la Mashahidi unless otherwise noted.