Biblia inasema askofu anapaswa awe mume wa mke mmoja! Je! Wale wasiooa kwa ajili ya injili hawawezi kuwa maaskofu?

by Admin | 1 September 2019 08:46 pm09

1 Timotheo 3:1 Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema.2 Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja,..” 


JIBU: swali zuri, na pia wengi wanachanganyikiwa kuhusu hilo, wakidhani kuwa mtu yeyote anayeitwa askofu ni lazima aoe…lakini unapaswa uelewe kuwa hapo Mtume Paulo alisema hivyo kwa mantiki ipi?, hakuwalenga wale ambao hawajaoa bado hapana, bali aliwalenga wale ambao wanao wake zaidi ya mmoja..kwamba hao ndio hawapaswi kuwa maaskofu, kwasababu ni lazima waonyeshe kielelezo kwanza wao wenyewe katika nyumba zao na ndio waje kuchunga wa nje, sasa kama mtu alikuwa na wake 6 kabla hajaamini na akaingia kwenye ukristo na ukristo unasema mtu anapaswa awe na mke mmoja, sasa unadhani wale atakaowachunga yeye kama askofu atakuwa anacho kielelezo gani? 

Na ndio maana haipaswi mtu yeyote anayeitwa askofu au mchungaji awe na mke zaidi ya mmoja…Lakini haikumaanisha pale kwamba ni lazima kila anayetaka kuwa askofu awe na mke, huo ni uelewa hafifu wa maandiko. Kumbuka mtume Paulo naye hakuwa na mke, lakini alikuwa mwangalizi wa makanisa yote, Kristo naye hakuwa na mke lakini yeye ndiye Askofu wa maaskofu. Hivyo hapo maneno hayo yaliwalenga wale ambao tayari wanao mke zaidi ya mmoja. 

1Wakoritho 7:32 Lakini nataka msiwe na masumbufu. Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana, ampendezeje Bwana;

33 bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe.

34 Tena iko tofauti hii kati ya mke na mwanamwali. Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu mwili na roho. Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mumewe

Ubarikiwe.

Maran atha


Mada zinazoendana:

MATOWASHI NI WAKINA NANI?

JE! NI VIBAYA KUTAJA HUDUMA KWA KUJIPA CHEO? MFANO MIGHTY PROPHET, CHIEF APOSTLE N.K.?

NITAMJUAJE NABII WA UONGO?

MLINZI, NI HABARI GANI ZA USIKU?

BIDII YA MFALME YOSIA.


Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/09/01/biblia-inasema-askofu-anapaswa-awe-mume-wa-mke-mmoja-je-wale-wasiooa-kwa-ajili-ya-injili-hawawezi-kuwa-maaskofu/