Mithali 14:4 ‘Zizi ni safi ambapo hapana ngombe;

by Admin | 1 September 2019 08:46 pm09

SWALI: Nini maana ya huu mstari? Mithali 14:4 ‘Zizi ni safi ambapo hapana ngombe;bali nguvu za ngombe zaleta faida nyingi’.


JIBU: Hiyo ni hekima ya kidunia Sulemani aliiona ambayo pia inafananishwa na mambo ya rohoni. Ni wazi kuwa zizi lisilokuwa na ng’ombe au mfugo wowote, huwa ni safi ikiwa na maana kuwa hakuna mnyama atakayeweza kulichafua kwa kinyesi, au mikojo, au majani, hivyo kama ni mtu analimiliki hatateseka kwa namna yoyote ile kuligharamia, hatapoteza muda wake mwingi kulitunza, yeye atalifunga tu kwasababu litaendelea kuwa safi daima na kukaa pasipo na taabu yoyote, lakini mtu kama huyo kipo kitu atakikosa..

Lakini zizi ambalo lina mifugo, kama ng’ombe n.k. tunafahamu zizi kama hilo haliwezi kuwa safi kwasababu ng’ombe watakuwa wanajisaidia huko kila saa, mikojo itakuwa inafagiliwa mara kwa mara, kadhalika zizi nalo litapaswa liwe linapigwa dawa za kuuwa wadudu kila wakati vinginevyo mifugo haitaweza kukaa, zizi pia ni lazima liwe na majani ya kutosha, kama tunavyofahamu Ng’ombe ni mnyama anayekula sana hivyo mmiliki itampasa awe maporini muda mwingi kutafuta majani ya mifugo…Hivyo mmliki wa zizi hilo atapata dhiki na taabu nyingi zaidi ya yule ambaye zizi lake halina mfugo wowote isipokuwa huyu taabu yake haitakuwa ya bure, kuna wakati ataona taabu ya kuhangaika kwake.

Na ndio hapo tukirudi kwenye mithali anatumbia “bali nguvu za ng’ombe zaleta faida nyingi”…Hii Inamaana gani?.


Inamaana kuwa yule ng’ombe atakwenda KUMLIMISHA katika shamba lake, na kumletea faida nyingi kwa nguvu zake, tofuati na yule aliyeona ni taabu kumlea ng’ombe, siku ya ukulima wake itampasa sasa yeye mwenyewe akalime au aajiri kibarua.

Kadhalika katika roho, wengi wanapenda kuwa na mavuno mengi kwa Bwana, lakini hawapendi kuingia gharama za kuyafikia. Bwana Yesu aliwaambia makutano waliokuwa wanamfuata, wale waliopendezwa na njia ya Bwana lakini hawakuwa tayari kuingia gharama..soma

Luka 14: 25 “Makutano mengi walipokuwa wakifuatana naye, aligeuka, akawaambia,
26 Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, HAWEZI KUWA MWANAFUNZI WANGU.
27 Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
28 Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia?
29 Asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki,
30 wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza.
31 Au kuna mfalme gani, akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine, asiyeketi kwanza na kufanya shauri, kwamba yeye pamoja na watu elfu kumi ataweza kukutana na yule anayekuja juu yake na watu elfu ishirini?
32 Na kama akiona hawezi, hutuma ujumbe kutaka sharti za amani, mtu yule akali mbali.
33 Basi, kadhalika kila mmoja wenu asiyeacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu”.

Hivyo na sisi pia tunapashwa ili tuwe na mavuno mengi Bwana anatuagiza tuwe tayari kuingia gharama za kuyapata mavuno hayo..Na gharama zenyewe ndio hizo Bwana alizozitoa hapo juu.


Amen.

Ikiwa utahitaji msaada zaidi ya mafundisho ya kila siku/maombezi/ubatizo/ushauri basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi +255693036618/+2557890001312

Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP


Mada zinazoendana:

KANUNI RAHISI YA KUFANIKIWA.

TWEKA MPAKA VILINDINI.

UMEFUNGWA KATIKA GIZA NA UVULI WA MAUTI?

NJIA YA BWANA INATENGENEZWA WAPI?

KITENDAWILI CHA SAMSONI

JINA LAKO NI LA NANI?


 

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/09/01/zizi-ni-safi-ambapo-hapana-ngombe/