Biblia ituambia tusalimiane kwa busu takatifu. Hili busu ndio lipi?

by Admin | 2 September 2019 08:46 pm09

SWALI: 1 Petro 5:14 Biblia inasema …“Salimianeni kwa BUSU LA UPENDO. Amani na iwe kwenu nyote, mlio katika Kristo. ”….Hapo ana maana gani? Mfano Binti mtakatifu akikutana nami anibusu shavuni kisha anisalimu au Mimi nikionana na Mke wako barabarani kwa kuwa ni mtakatifu kama mimi nimbusu kisha nimsalimu SHALOM?..


JIBU: Ukisoma mstari huo kwa makini utaona biblia inasema ‘BUSU LA UPENDO’ Sehemu nyingine biblia inataja kama BUSU TAKATIFU..Unaweza kusoma hiyo katika Warumi..Warumi 16: 16 “Salimianeni kwa busu takatifu. Makanisa yote ya Kristo yawasalimu.”.. Na Pia katika 1Wakorintho16:20 inasema: “Ndugu wote wawasalimu. Salimianeni kwa busu takatifu.”…Na mistari mingine utakayoweza kukutana na hilo neno ni 2 Wakorintho 13:11, na 1 Wathesalonike 5: 24…Mistari yote hiyo inathibitisha kuwa kuna kitu kinaitwa Busu Takatifu. Sasa zamani kipindi cha Bwana wetu Yesu Kristo, na hata kabla ya hapo, kulikuwa na utaratibu wa kubusiana kama ishara ya salamu ya heshima kidogo, salamu ya kubusiana ndio ilikuwa salamu ya msingi kabisa kwa wakati huo, kama sasahivi ilivyo salamu ya kupeana mkono…kwahiyo watu walikuwa wakikutana walikuwa wanabusiana kwa nia ya kuonyesha upendo,shukrani, uthamani wa mtu n.k…Na kumbuka haikuwa busu la mdomo kwa mdomo hapana! Bali busu la mdomo kwa shavu au ubavu wa shavu. Na sasa tukirudi kwenye biblia inasema kuwa tusalimiane kwa BUSU TAKATIFU, ikiwa na maana kuwa sio Busu la mapenzi, wala sio busu la ubaya kama lile Yuda alilomsaliti nalo Bwana katika.. 

Mathayo 26: 48 “Na yule mwenye kumsaliti alikuwa amewapa ishara, akisema, Nitakayembusu, huyo ndiye; mkamateni.

49 Mara akamwendea Yesu, akasema, Salamu, Rabi, akambusu”. 

Bali busu linalotajwa hapo ni BUSU LA HERI, NA BARAKA na UPENDO..Yaani mtu anambusu ndugu yake katika Kristo kwa nia ya kumtakia heri na Baraka kutoka kwa Mungu, kama mwamini. Lakini huo ulikuwa ni utamaduni wa zamani za wakati huo, ambapo Busu lilikuwa halina tafsiri nyingi tofauti tofauti kama ilivyo leo…Lakini leo hatuna utaratibu huo wa kubusiana..tuna utaratibu wa kupeana mikono…ambao huo unaweza kubeba maana kubwa zaidi au pengine hata sawa na kubusiana…Leo hii mwanamume akikutana na mwanamume mwenzake na kumbusu mbele za jamii haileti hiyo tafsiri Mtume Paulo aliyokuwa anaizungumzia hapo ya BUSU TAKATIFU, bali inaleta tafsiri nyingine…

Ingekuwa ni kwa kipindi cha wakati wake ingeweza kueleweka..Kwa wakati huu Busu takatifu linalokubalika katikati ya kanisa ni Busu kati ya dada na dada, au kati ya mzazi na mtoto na si kati ya kaka na dada ambao si ndugu, au kaka na kaka…Busu kati ya kaka na kaka inaleta tafsiri nyingine na maswali mengi,… 

Kwahiyo hapo ni muhimu kutofautisha tu salamu zinazotumika kulingana na nyakati..Mtume Paulo hakusema kuwa hilo ni agizo toka kwa Mungu, kwamba ni lazima kila tukutanapo tusalimiane kwa kubusiana..hapana! kwasababu salamu zinabadilika kulingana na nyakati…angekuwepo katika wakati huu ambao tunapeana mikono au kukumbatiana kama salamu badala ya kubusia, angeshauri tusalimiane kwa kupeana mikono ya Utakatifu, nk. Kwahiyo ukikutana na mwamini mwanamke, msalimie tu kwa kumpa mkono hiyo ni sawa na kumsalimia kwa busu takatifu haileti tofauti yoyote. 

Ubarikiwe.


Mada Nyinginezo:

NINI MAANA YA MSTARI HUU: (MTU AMBARIKIYE MWENZAKE KWA SAUTI KUU ASUBUHI NA MAPEMA; ITAHESABIWA KUWA NI LAANA KWAKE.MITHALI 27:14 )?

TOFAUTI KATI YA SHERIA YA ROHO WA UZIMA NA SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI!

MEZA YA BWANA, NA KUTAWADHANA MIGUU.

UZAO WA NYOKA.

FASHION! NI DHAMBI KWA BINTI ZA MUNGU.


 

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/09/02/biblia-ituambia-tusalimiane-kwa-busu-takatifu-hili-busu-ndio-lipi/